Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha,Akili Mpwapwa akionyesha silaha ambazo majambazi watatu waliouwawa na wananchi wenye hasira kali walikutwa nazo.

Na Woinde Shizza,Arusha

WATU watatu ambao ni majambazi wameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kuwapora wafanyabaishara watano waliokuwa wakielekea kwenye mnada wa soko la ng'ombe uliopo Meserani wilayani Monduli.

Majambazi hao wakiwa na silaha za moto, walikuwa wakitumia gari lenye namba T785 ACM aina ya Toyota Mark II ,walifyatua risasi nne hewani baada ya kuwavamia wafanyabiashara hao eneo hilo la Meserani na kuwapora kiasi cha sh. milioni 4.2 na simu mbili za mkononi.

Majambazi hao wametambulika kuwa ni,Obeid Erasto(30),Florence Basili(27) na Rafael Patrick(37) wote wakazi wa mjini Arusha.

Wafanyabishara hao wametajwa kwa majina kuwa ni, Jackson Kisyokii (47) Kijenge, Lembris Bikoto(60) Kisongo, Jackson Kalaine (35) ,Gregory Joseph (39) Kijenge na Silas Sayolo(40) Sokon 1ambao kwa pamoja walikuwa wakielekea kununua ng'ombe katika eneo hilo la Meserani wakitumia gari nambaT 744 BMX aina ya Hyundai.

Akizungumza na waandishi wa habari , Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 7 mchana katika eneo la Kisongo barabara ya Arusha- Babati ambapo majambazi hao waliwateka wafanyabiashara hao na kuanza kufyatua risasi hewani .

Mpwapwa alisema kuwa,wafanyabiashara hao walitii amri na kuwakabidhi majambazi hao kitita hicho na simu za mkononi,hata hivyo baada ya kufanikiwa kupora waliamua kurudi mjini Arusha.

Walipofika eneo la Olmatejoo walihisi kufuatiliwa kwa nyuma na polisi ndipo walipolitelekeza gari walilokuwa wakilitumia na kuanza kukimbia kwa miguu .

Alisema kabla hawajafika mbali wananchi waliwazingira na kuanza kuwashambuliwa kwa mawe kiasi cha kupoteza fahamu ndipo polisi walipofika eneo la tukio .

Kwa mujibu wa kamanda Mpwapwa ,polisi kabla hawajawachukua majambazi hao walipekuliwa na kukuta wakiwa na bastola aina ya Brown ikiwa na risasi tatu yenye namba 069082 ,Bunduki aina Shortgun yenye namba R 253578 ikiwa na risasi 14 zikiwa zimefishwa kwenye gari walilokuwa wamelitelekeza.

Aidha pia,walikutwa na silaha iliyotengezwa kienyeji yenye namba 458 ikiwa na risasi tatu ,baada ya upekuzi huo polisi waliwachukua kwa ajili ya kuwafikisha hospitali ya Mount Meru wakiwa mahutihuti .

Aidha majambazi hao walifariki dunia muda mfupi wakiwa njiani kabla ya kufikishwa katika hospitali hiyo na uchunguzi juu ya tukio hilo bado unaendelea na kwamba polisi hawakufanikiwa kuokoa fedha zilizoporwa na majambazi hao .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2011

    hapo kwenye kushindwa kuokoa fedah kuna walakini...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 14, 2011

    kama polisi walilikuta gari pamoja na silaha walizokuwa wakitumia na majambazi walikuwa hawajapitia mahali pengine popote baada ya kufanya ujambazi inakuwaje polisi wanasema hawakuwakuta na hizo fedha walizoiba? kuna jambo hapo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2011

    kama hajatueleza fedha walizoiba ziko wapi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 14, 2011

    Mh; 'Walipofika eneo la Olmatejo ''walihisi'' , nasisitiza 'WALIHISI' kufuatiliwa nyuma na polisi'.HAPO PATAMU HAPO!!!
    Ama kweli kuna maswali mengine ukijiuliza majibu yanakuja yenyewe; wala hutakiwi kuumiza kicha. Bongo inahitaji UBONGO; si mchezo. Fedha haijaokolewa; lakini silaha za moto zimepatikana; siyo visu wala mapanga; ila bastola. Hela je??? Zimeota mbawa baada ya kufa hao majambazi au zilihisi polisi watazirudisha; na kwa ki-intelijensia zikachukua cover. INTERESTING TZ

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 14, 2011

    Huyu afande anaonekana ndio kwanza ameanza kukaimu atapokua mkuu wa polisi ndio afya yake itakua nzuri. Mbona hanenepi kama wenzie? Naona hiyu sio fisadi

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 14, 2011

    ah! ah! jamani magitaa haya ya kina ras..huyu afande alivyoyashika yasije yakaliza sebene..!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 15, 2011

    Jamani nimewapenda wananchi wa Arusha, umoja ni nguvu polisi wana silaha wanashindwa kuwauwa majambazi wananchi wanawauwa tena kwa mawe, jambazi yeyote akishikwa auwawe tu,mkipeleka polisi wanahonga wanaachiwa wanawamalizia hasira wale walio wakamata hiyo ndo Tz hata ukiwa na 2000 Pound 1 unamalizana na polisi tena kwa furaha tu.
    Hongereni wananchi na endeleeni na umoja huu Arusha iwe mfano wa kuigwa na mikoa mingine. Good job, well done

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 15, 2011

    hiki ni kitu kibaya sana. mbona kuna jina la mwanamke hapo. hawa wanaonekana ni watu wa kutoka nje ya mikoa ya kilimanjaro na arusha. inawezana kuwa wanatoka majimbo mengine.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 15, 2011

    Jamani Polisi wa TZ! Mbona wanavyosema kuhusu tukio nzima ni kuwa na pESA zilipatikana? kwa mtiririko wa TUKIO hili lazima polisi wajue na pesa zipo wapi! Acheni ubabaishaji wenu! Mnageuka kuwa 'WAPORAJI'?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 15, 2011

    hela zilianguka wakati wanakimbia lol..........................hahahaaaaaaaaaaaaaaaaa! uzalendo TZ.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 15, 2011

    Sawa! Wafanyieni operetion ya tumbo watakuwa walizimeza baada ya kugundua wanafuatiliwa na polisi.Ila msiwatese pesa wanazo polisi waliokuwepo kwenye tukio.Poleni mlioibiwa ndo imetoka hiyo.Hiyo browning ndo no.yake inaanza hivyo au mmekosea? lazima no.ianze na A or any alpherbet.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 15, 2011

    ukweli unauma,poleni mlio ibiwa.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 15, 2011

    changa la macho hao waliuawa kwa bahati mbaya wasingeonwa na raia gari isingekuwa imetelekezwa na polisi wangekuwa bado wanawasaka.WALIVYOHISI kufuatiliwa na polisi pesa zikayeyuka.kalagabahoooooo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 15, 2011

    Jamani kwani hamuoni inasema wazi kuwa "POLISI HAWAKUWEZA KUOKOA FEDHA ZILIZOPORWA"? Mnataka wawaeleze zaidi kivipi? Hawakuweza kuziokoa zilichukuliwa na waliokuwa karibu zaidi na majambazi...yaani Polisi wenyewe...!! Hata wao walishindwa kuziokoa...unadhani ni rahisi kuokoa pesa bila kuzila??? Mdau-USA

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 16, 2011

    Pesaa pesaa!!! Sasa imekuwaje pesa pekee ndio hazikupatikana,wananchi tukimbilie wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...