Habari iliyoifikia Globu ya Jamii muda mfupi uliopita toka katika chanzo kimoja cha habari inaeleza kuwa, kundi la watu wanaodaiwa kuwa ni Majambazi wakiwa na Pikipiki wamevamia na kupora Mamilion ya fedha katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Tukio hilo la ujambazi limefanyika leo asubuhi ambapo inadaiwa kuwa askari Juma Mangungu wa Kampuni ya Full Time Security aliyekuwa analinda katika Idara ya Uhasibu amepigwa risasi Kifuani na majambazi hao na kusababisha kifo chake.
Studio za Radio Uhuru Fm zimeueleza mtandao huu kuwa Afisa uhusiano wa Hospitali ya Taifa,Ndugu Aminiel Aligeisha ameiambia Uhuru FM kuwa tukio hilo limetokea leo saa mbili asubuhi ambapo wahasibu wawili wa Hospitali hiyo walikuwa katika zoezi la kuzipeleka fedha Idara kuu ya Uhasibu wakiwa na gari ndipo kundi hilo la Majambazi likatokea na kuwavamia.
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano huyo,gari hilo lenye namba za usajili SU-36713 aina ya Nisani ikiwa na watumishi Wanne wa Idara ya Uhasibu walivamiwa na kundi hilo la watuhumiwa wa ujambazi wakiwa na Bastola moja.
Kulingana na Afisa Uhusiano huyo Ndugu Aligeiisha alisema kuwa zaidi ya shilingi Miloni-13 zinasadikiwa kuibiwa na majambazi hao na kutokomea.


Inside job!!Hela ndogo sana kuua mtu. Je, kuna CCTV cameras around Muhimbili? CSI guys, work the scene!
ReplyDeleteWabanwe hao ao wahasibu, hawezi kutoka mtu kuota mtu kuwa muda hela zinahamishwa toka point A kwenda B kama hakuna mtu wa ndani aliyewapa taarifa. Tuanze kuchunguza simu zao za mikononi.
ReplyDeleteDUH YAANI KATIKATI YA JIJI, HEBU WEKENI KAMERA WAJAMENI majambazi yamezidi, yakamatwe....sasa saa 2 asubuhi hata kupiga simu mpate usaidizi yakamatwe hayo majambazi hamjaweza!!...Duh inaniuma sana, ningekuwa Rais nisingeruhusu hali hii inayotishia usalama wa raia kila kukicha!
ReplyDeleteaaarrrg inakera jamani hapo sio bure ni mpango mzima huo kuna mtu kati ya hao hao wanaojua pesa zinahamishwa akachonga mchongo na majambazi sababu wanajua kuwa majambazi hawakamatwi bongo...maskini askari wa watu alale pema peponi..
ReplyDeleteWahusika ni hao hao wahasibu, mtu wa nje atajuaje kwmba leo Muhimbili wanahamisha pesa.RIP Askari uliyeuliwa. Wahasibu na watu wengine wa ofisi iyo wawe wahusika number moja.
ReplyDeleteMimi ninashangazwa sana na huu utaratibu tulionao hapa kwetu Tanzania .Wakati wa miaka ya 70 hadi 80 , ilikuwa bado tuko nyuma sana kielimu , mambo ya Internet ilikuwa sio wengi walikuwa nazo au wanaojuwa kuzitumia, Mabenki yetu pia yalikuwa na utaalamu mfupi wa kutunza mahesabu na kurekodi .
ReplyDeleteMambo mengi yalifanyika kwa kuweka kumbukumbu kwenye vitabu, Mishahara ilikuwa kwenye mabox ya sigara, Bwana Fedha alikuwa ndio mtu pekee anae juwa kuwalipa Wafanyakazi ,sio kila mtu
Leo hali hiyo haipotena tunayo Mabenk mengi tu na ya kutosha, tunao wataalamu wazuri waliobobea kwa Computer wanaweza kuweka kumbukumbu vizuri na pesa zote zikawa ziko Salama BANK . Ni haki ya kila Raia kuwa na Account Bank , kuwa na kitambulisho ,kama passport, kitambulisho cha Kazi ,Uraia Na hata kutumia Account ya Ndugu yake kama bado ya kwake haijatoka .
Sasa sisi watu tuliokuwa hatukusoma , Tukiuliza pesa hizo zilikuwa zinakwenda wapi , itakuwa tumekosea? Na kwa nini zisafirishwe kwa gari na ulinzi usiokubalika ? . Kwa nini hizo pesa zisiwekwe BANK , na KAMA ZINATAKIWA HAPO UKATUMIKA UTARATIBU WA KUHAMISHA BANK TO BANK?
Huu ni wizi wa mafisadi wala sio wa ujambazi, Kwanza wakamatwe wahasibu wote, wafuatiliwe nyenzo zao kwa mwezi uliopita na wanyanganywe simu zao kuona njia walizowakitumia siku za nyuma.
HUU WANGU USHAURI.
Msiwazingishie bure hao wahasibu, hizo ni pesa ndogo sana kwa malipo ya kawaida yanayochukuliwagwa na hao wahasibu. Wangekuwa ni wao ndiyo wana nia ya kuchonga dili kama hiyo wangesubiri wakati wakuchukua big cash ya over 50 million, malipo ambayo ni ya kawaida kuhukuliwa kila wiki kwa mazingira ya hapo muhimbili. BANK ZA NBC AU NMB ziko ndani ya eneo lenyewe la muhimbili, so wahasibu huchukua cash kama hizo karibu kila siku na siyo siri kwa wafanyakazi wote wa muhimbili wanalijua hilo, so siajabu kwa majambazi au yeyote mwenye nia mbaya kujua kwamba wahasibu au mhasibu ameenda bank wakati fulani. Taasisi yenyewe ina watu zaidi ya elfu sita wafanyakazi na wanafunzi, huku wakichanganyika na wagonjwa na watu wengine mbali mbali wanaofika hospitalini hapo kila siku, kutakuwa na siri kweli hapo, ya watu kutokujua pesa zinaenda chukuliwa wakati fulani!!! na benki zikiwa hapo hapo pua na mdomo. Just a walking distance
ReplyDelete