Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa zinduzi wa Sherehe za maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani, zinazofanyika kitaifa mjini Songea Mkoani Ruvuma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibonyeza kitufe kuashiria kuzindua rasmi maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika kitaifa mjini Songea mkoani Ruvuma. Sherehe hizo zimeanza leo Juni 01, katika Uwanja wa Majimaji. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal na (katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Christine Ishengoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea Moa wa Ruvuma kwa ajili ya kuzindua rasmi sherehe za maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma ujumbe kuhusu zoezi la kuzuia uchomaji wa misitu katika mabango yaliyokuwa yameshikwa na vijana, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, zilizozinduliwa leo Juni 01 kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea Mkoa wa Ruvuma. Kulia ni mkewe Mama Zakia Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Mkoa wa Ruvuma, Methord John, kuhusu uzalishaji wa matofali yanayochomwa kwa kutumia Makaa yam awe, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani zilizoanza mjini Songea mkoa wa Ruvuma leo Juni 01, kwenye Uwanja wa Majimaji.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Songea (Songea Girls) wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo za maadhimisho kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea Mkoa wa Ruvuma leo Juni 01.Picha zote na Muhidin Sufiani wa OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2011

    Mkuu ongeza umakini kidogo, Muheshimiwa anapata maelezo kuhusu ufugaji wa Mamba na sio uzalishaji wa matofali kama unavyosema

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2011

    HAPA TUNAWAONA SONGEA GIRLS'WAKIMEREMETA,HONGERA KWENU,NAKUMBUKA ENZI ZETU ZA MIAKA YA 80 TULIWAITA "TAMSALA"SIJUI KAMA HADI SASA WATUMIA NICKNAME HIYO.
    MIMI NI "BOX TWO"(SONGEA BOYS')WA ENZI HIZO,NINA UHAKIKA KUWA WATOTO WETU WAPO HAPA.KILA LA KHERI TAMSALA AU "TAMSO".
    MDAU.USA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...