Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mama Hillary Clinton akiongea baada ya kutembelea mtambo wa kufua umeme wa kampuni ya Kimarekani ya Symbion Power Ubungo, jijini Dar es salaam. Shoto ni Bw, Daniels Yohannes, mkuu wa ,mfuko wa MCC na kulia ni mtendaji Mkuu w Symbion Power Bw. Paul Hinks
Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja akifafanua jambo baada ya ziara ya Mama Hillary Clinton ya mtambo wa kufua umeme wa Symbion Power uliopo Ubungo, Dar es salaam
Mama Hillary Clinton akisalimiana na Bw. Mohamed Saleh, mmoja wa mabosi wazalendo wa Symbion
Mama Clinton akiwa katika mtambo wa kufua umeme wa Symbion Power huko Ubungo jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Bw. Paul Hinks na kushoto wapo Mkuu wa mfuko wa MCC Bw. Daniel Yohannes na Waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, Mh Bernard Membe.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA




Waheshimiwa kupendeza wamependeza. Lakini UMEME wa uhakika sie wanyonge tutapata?:-(
ReplyDeleteTANESCO
ReplyDeleteJE UMEME WA MGAWO NDIYO UMEKWISHA AU HAYO NI MANJONJO YA KUMUONA
HILALY CLINTON
MAANA DUH KESHO TU UMEME HAKUNA
JE TUTAFIKA?
Ahh kumbe ndo mana iliwashwa, coz boss anakuja? Ngoja aondoke mwezi mmoja tutaanza kusikia hamna mfuta ya kuendeshea mitambo....bongo tambarare!
ReplyDeleteHuu mradi ni wa akina Clinton au?, maana kutembelewa na Secretary of State wa marekani nchini ni ujio mkubwa. Halafu kaja kimya kimya. Ajabu hii interest inaleta maana fulani ndani au ndio wanaanza kidogo kidogo kuingia katika hema, kichwa kwanza. Watanzania amkeni.
ReplyDeleteMMMMmmmmh kama naota vile!
ReplyDeleteAaaahh! Watanzania kazi yenu ni porojo tu, matumizi ya maarifa na uono wa mbali kimanufaa hakuna kitu!! Hii Symbion si dio ile iliyokuwa Dowans ambayo Mtaalam fulani akapendekeza inunuliwe na serikali ili kuinusuru nchi? Baada ya hapo kukawa na kelele nyingi kuwa eti Mtaalamu kala kitu kidogo, na ndio pale aliposema kuwa wagonjwa mahospitalini wakifa na wanafunzi vyuo vikuu wakashindwa kufanya revision kwa kukosa umeme lawama zisimrudie yeye, Mheshimiwa sana mmoja nae akapendekeza kuwa huyo mtaalamu aadabishwe kwa maneno yake (ambayo kimsingi ni ya ukweli, si wagonjwa walikufa wengi tu?).
ReplyDeleteCha ajabu wenye maendeleo makubwa kuliko wote duniani wamekuja kuinunua mitambo hiyo ambayo sisi tulijidai eti ni michakavu!!!! Procuremeny Act yetu ilikataa!! Hivi hao Wamarekani ni wajinga kununua mali chakavu yenye manufaa makubwa? Tuache kujifanya wajuaji kumbe hamna kitu.