Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha unalenga katika kupanua wigo kwa watu wengi zaidi kutumia huduma za Fedha Tanzania. Umuhimu wa biashara ndogondogo na za kati katika ushindani na ukuaji wa uchumi, utengenezaji ajira na upunguzaji umasikini unatambulika sana. Upatikanaji duni wa fedha unaendelea kuwa kikwazo kwa biashara ndogo ndogo na za kati. Kiasi cha bidhaa za kifedha zinazoingia sokoni ni kidogo na kuna upungufu mkubwa wa ubunifu kukabili changamoto hii.
‘Mfuko wa changamoto za ubunifu kifedha katika biashara ndogo na za kati’ unatoa changamoto hii kwa taasisi zinazotoa huduma za kifedha (benki na zisizo benki ) kujaribu kutumia ubunifu na kutengeneza mifumo tofauti ya kibiashara itakayotoa bidhaa mpya za kifedha na huduma bora kwa biashara ndogo na za kati ambazo hazihudumiwi ipasavyo na taasisi za fedha.
Mfuko huu unatumia utaratibu wa kushirikiana uthubutu wa kibiashara. Kwa kugharamia kiwango kinachofikia nusu ya gharama za kuanzisha bidhaa na huduma mpya za kifedha zinazolenga kufikia na kuhudumia biashara ndogo na kati zilizoko pembezoni mwa mfumo wa huduma za kifedha, FSDT inalenga kukuza ubunifu katika sekta ya fedha.
Kupitia utaratibu huu, taasisi ya fedha inayothubutu kuibua na kutekeleza mawazo ya biashara ambayo katika hali ya kawaida si rahisi kukubalika kwa taasisi za kifedha kugharamia, inapata afueni.
Ubunifu na bidhaa mpya za kifedha zinazolengwa zinaweza kuwa ni bidhaa mpya zinazolenga wafanyabiashara wadogo na wa kati, teknolojia mpya, mfumo fanisi zaidi kupima ustahili wa kukopesheka, kutengeneza mfumo wa kuunganisha kimkakati watoa huduma ili kufikia biashara ambazo awali hazikuwa zinahudumiwa ama kifikiwa na huduma za fedha, kufungua mianya mipya ya huduma na kubuni mbinu mpya za kujitangaza na mikakati ya kuhudumia wateja.
Walengwa
Fursa za mfuko huu zinalenga taasisi za kifedha na si biashara ndogo na kati zenyewei. Taasisi hizi za kifedha zinaweza kuingia ubia na taasisi nyingine za watoa huduma zilizo nje ya taasisi za kifedha na hizi zinaweza kustahiki kusaidiwa. FSDT inalengo la kusaidia miradi ama mipango inayolenga kufanya majaribio yenye ubunifu katika mbinu, dhana, teknolojia, na mifumo ya biashara; na si kusaidia utaratibu wa kawaida wa kibiashara au katika kukopesha.
Tuzo na Kutuma Maombi
Tuzo zitatolewa kwa mchakato wa ushindani wenye hatua mbili, na zitakuwa kati ya kiwango cha dola za kimarekani laki tano ( 500,000) na laki moja (100,000). Maamuzi yatatolewa kwa muongozo wa waamuzi huru.
Kwa ufafanuzi zaidi, kupata fomu za maombi pamoja na maelekezo kwa waombaji nenda katika tovuti hii http://www.fsdt.or.tz/index.php/jobs ama tutumie barua pepekwenye anuani hii: info@fsdt.or.tz
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...