Mgambo wa Jiji wakiwa wamemkamata mwanamama ambae jina lake halikuweza tambulika mara moja aliekuwa akiza bidhaa zake katika mtaa wa Aggrey,Kariakoo mchana huu mara baada ya kupambana na mmoja wa wanamgambo hao bila mafanikio.
 Hapa ilikuwa ni Purukushani ya vuta nikuvute ikiwa ni katika hali ya kuzuia mali zake zisichukuliwe na wanamgambo hao.
 Hali hii ilimfanya kila aliekuwa akipita jirani na tukio hilo kushangaa na kutojua cha kufanya.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa mchana huu katika mtaa wa Aggrey,Kariakoo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2011

    Tanzania tambarare. mtu anatafuta risiki kihalali mgambo na serikali inamuonea. Mfilis wa mali ya umma mwenye kitambi kilo kumi na fedha nyingi kisicholingana na mshahara wake wanamgambo na serikali wanawalinda.

    Na ni nini kinachowafanya wapita njia kuona hili jambo ni la kuchekesha?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 28, 2011

    hivi hawa MGAMBO wamekosa kazi ya kufanya nini????? ndio nini kuwatesa mama wa watu wanajifanyia biashara wao kila kukicha kuwasumbua tu.embu nyie WAGAMBO punguzeni huo upuuzi mnaoufanya maana sio haki kabisa!!!
    MTANZANIA HALISI-KIWANJA.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 28, 2011

    Huyo mama huo ndio mtaji wake wote. Kama sheria mngeanza kwa mafisadi, huyo mama hakumuibia mtu, anawatoto pengine wanne, mume hana, kazi ndio hiyo auze vitumbua apate kula yeye na watoto, pengine anapango lake Segerea. Sheria na ubinaadamu, serikali inatakiwa iwalipe wananchi wake wasiokuwa na kazi na wana watoto. Siku kuwazalilisha mitaani na kuwamwagia vitumbua vyao.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 28, 2011

    Jamani wahurumieni hao watu, mnawapora mali zao waende wapi, wakaibe? Zisimamie sheria mlizotunga kwa kuwashitaki katika vyombo husika lakini msipore mali zao!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 28, 2011

    MTAJI WA HUYO MAMA HAUFIKI HATA GHARAMA YA MAFUTA YA GARI LA MBUNGE KWA SIKU, LAKINI ANANYANYASIKA MBELE YA UMAAAA. LAANA YAKE NI KUBWA KULIKO INAVYODHANIWA.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 28, 2011

    duh!! hawa watu wakale wapi lakini?? mbona malofa wanaonewa kiasi hiki?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 28, 2011

    Haya ndio mambo yalivyoanza Tunisia. Huyu mama anatafuta kula lakini masikini mgambo ndio hao... I bet you huyu lost all her merchandise,

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 28, 2011

    Hii ni aibu kwa jamii ya kistaarabu..hivi kwanini nchi ya demokrasia ina mgambo na kazi yao ni nini hasa na polisi kazi zao ni zipi.. na sheria ziko wapi..na hiyo ndio hali halisi ya watanzania kunyanyasana kama nyani mwituni..sijui afanye kazi gani mama wa watu aweze kulisha watoto nyumbani.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 28, 2011

    Fukuza, Fukuza , Fukuza wananchi wote waliowatanzania, haswa wale weusi, achia wahindi waarabu na wachina wafanya biashara hapo kariakoo. Hili ndilo jibu la meya wa mji wa Dar-esa -salaam. Kwa nini watanzania wenzetu weusi wananyanyasika namna hii, hii ni nchi yao waache wafanye biashara wantafuta pesa ya kulisha watoto. Mkoloni hajarudi vizuri, tusubiri tu kila kiwanda na kila offisi ya watu waliotoka nje ta Tnaznia tutaanza kuwa watumwa na hatuna sauti tena, viongozi wetu wameshalewa vijisenti wanvyopewa na uanza kunyanya wannchi wao wenyewe. Kumbuka Hata wakoloni walipokuja Babu zetu walidanyanywa na kioo, shanga na n.k, leo hii tunakwenda kuita watu kuja kunyanyasa wannchi wetu wenyewe na hakuna sheria ya kutetea wannchi. Wengine mnaotaka wafanya biashara wanatafuta pesa ya kupeleka kwao walikotoka na siyo kwa ajili ya kuliendeleza taifa letu.
    Michuzi usibanie hii, siku moja utajikuta na wewe na wajuu zako manynyasika hivi, hili ni sala la kila mtu, najuwa wanvunja sheria lakini wantafuta pesa ya kulisha familia na hakuna kingine, sasa wafanya nini hawa watu wapo kwa mamilioni hapo mjini hawawezi kuacha familia wakafa njaa.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 28, 2011

    It's a matter of days Arab Spring itatinga kwetu. Watawala wasiyapuuze haya!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 28, 2011

    huyu mama anaeteswa hivyo akiuza mwili wake anaambiwa anafanya umalaya anashtakiwa yupon kariakoo na bidhaa za elfu kumi ananyang'anywa sasa akale wapi kwa Nape mnauye

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 29, 2011

    Sheria Tanzania hazitakaa zitekelezwe....inamaana hawa mgambo wameamriwa kunyang'anya bidhaa za maskini? Hivi kweli hakuna utaratibu mwingine wa kufuatilia hali hii? Mnazidi kujenga maghorofa hapo k/koo kwa nini msitafute utaratibu mkawapa hata leseni za kuuzia vitu vyao...na muwapatie maeneo maalum na kwa ustaarabu hapo kariakoo? yaani mnazidi kujenga mighorofa tu, hata magari hayawezi kupita tena! Jiji ovyo kabisa la Dar. Waziri Nyalandu, Mayor wa jiji na viongozi wengine, hamuyaoni haya??

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 29, 2011

    Mi kuna siku nitawapiga mgambo tena kwa fimbo, nawanunulia vijana unawalipa cha juu hao vijana then wanawapiga mgambo hadi ambulence ifike wamekufa maana siwapendi, niwaonevu, na ni waoga ndo maana ya bakora. Au kwanini wamachinga msijiunge mkawamaliza? Iweni kitu kimoja sisi tutawaunga mkono tena tutaenda kujiburudisha later, eti nchi ina rais, wabunge, mawaziri na meya wa jiji, halafu wote ni wacha Mungu tena kanisani na misikitini wamejaa, WANAFIKI wakubwa nyie mnadhani walalahoi ni wa nyama au miti? Ole wenu kabla Yesu hajarudi mtavuna tena sisi walalahoi tukishangilia, ndo maana pressure, kisukari na ukimwiya hauondoki kwenu. Eti wachina ndo wamachinga, i hate you all who arranged and welcomes Chinese in my Country while our people are strugling eti leo hii picha ya mtoto wa Tanzania masikini mwenye njaa ndo inatumika kuombea hela huku ulaya kusaidia watoto wenye shida akiwepo wa ki-Tz tangu tupate uhuru na wabunge wanatesa na marada hivi ni akili au maji???. Embu jamani tufikirie kuwasaidia maskini na hawa wazazi na dada zetu wanaonyanyaswa na hii sirikali. Michuzi please usinibanie acha wasome labda watasoma wahusika even thou i don't scare them, ingekuwa mandela aliogopa nchi yake isingekuwa hapa. Wamepata uhuru juzi tu but their all far more than Tz. Na wako mbali sisi ushuru kila kona wanakula Wenye midomo ina elekea Mafisadi ndo walalahoi kwani kila shs wanataka hata za laana kwao. Olee wenuuuuu

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 29, 2011

    Hata kama tutawalaumu mgambo lakini tukirudi kwenye sheria, je ni haki machinga kuvunja sheria eti kwa vile mtaji wao ni mdogo? Kwa mfano ukienda machinga complex, pale uwanja wa karume utakuta wamachinga hawataki kupanga bidhaa ndani ya nyumba waliyotengewa badala yake wanatoa bidhaa nje na kuzipanga kandokando ya barabara. Matokeo yake waenda kwa miduu wanakosa pa kupitia inabidi wapitie barabarani ambapo magari yanapita kitu ambacho ni hatari kwa usalama wao. Saa zingine wanadiriki hata kupanga bidhaa zao barabarani na kusababisha foleni. Mimi ningeomba tujifunze kufuata sheria kwani si kila sheria imewekwa kumkandamiza mtu.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 29, 2011

    Hivi mgambo kazi yao ni kuwanyanyasa wamachinga tu? KUSIMAMIA USAFI WA JIJI KUMEWASHINDA, ndo maana mnabaki hamna hata maendeleo binafsi. Kazi yoyote halali MUNGU anayokujalia fanya kwa haki.

    Dar es Salaam ni kubwa sana, ingepaswa hawa mgambo wasimamie sheria za mazingira na kuwaadhibu wale wanaotupa taka hovyo, wanaojisaidia barabarani n.k. Pia kuna wachina kibao wanaofanya biashara bila vibali halali au wanaishi nchini bila vibali sasa mbona hamuwakamati hao mnaishia kukamata wazawa?

    Hiyo yote ni kutaka hongo kutoka kwa hao mnaowaharibia mitaji yao.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 29, 2011

    We mdau unayewalaumu Wahindi kwani wamekosea nini? Au sio binadamu? Kila kitu wahindi tu? Kwani wanamgambo hao wametumwa na wahindi au waswahili wachache ambao wameshiba na hawataki wenzio wapate? Acha ubaguzi rafiki yangu. Mimi ni mhindi na nikiona picha hizo zinanisikitisha pia maana huyo mama anatafuta rizki badala ya kujihusisha na umalaya au madawa ya kulevya. Ni hawa mafisadi wanatuharibia sote sisi na kutuchonganisha. Tupige vita ufisadi kwa njia zote!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 29, 2011

    We mdau unayewalaumu Wahindi kwani wamekosea nini? Au sio binadamu? Kila kitu wahindi tu? Kwani wanamgambo hao wametumwa na wahindi au waswahili wachache ambao wameshiba na hawataki wenzio wapate? Acha ubaguzi rafiki yangu. Mimi ni mhindi na nikiona picha hizo zinanisikitisha pia maana huyo mama anatafuta rizki badala ya kujihusisha na umalaya au madawa ya kulevya. Ni hawa mafisadi wanatuharibia sote sisi na kutuchonganisha. Tupige vita ufisadi kwa njia zote!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 29, 2011

    Ukiangalia hizo picha utaona madukani bidhaa zengine zimepangwa barabarani mbele ya hayo maduka. Kisheria hawa pia ni wakosa na bidhaa zao zichukuliwe. Wamezidisha eneo la maduka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...