Walezi wa timu za vijana toka nchi nzima zinazoshiriki Copa Coca Cola 2011
ITV na Radio One Stereo wanaonesha michuano hiyo na kuitangaza live. Hapa Maulid Baraka wa Kitenge akiongoza kikosi kazi cha utangazaji huo wakati wa mechi ya ufunguzi
Mpiganaji Jamal Rwambow (kulia) akiwa na MC wa shughuli hii Ephraim Kibonde (shoto) na mdau
![]() |
| Sehemu ya uwanja wa Karume wakati wa mchezo wa ufunguzi |
![]() |
| Mkurugenzi mtendaji na mtangazaji wa Sport FM Abdallah Majura akiwa kazini kwenye ufunguzi wa michuano hii |
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi, amezindua rasmi msimu wa Tano wa michuano ya Copa Coca Cola kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ulioanza jana katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani katika viwanja vinne tofauti.Uzinduzi huo umefanyika Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam.Mikoa yote 28 ya Tanzania Bara na Visiwani inashiriki katika michuano ya mwaka huu. kila siku kutakuwa na mechi mbili kwenyeviwanja vyote. Mechi ya kwanza itaanza saa 2.30 asubuhi wakati ya pili itachezwasaa 10 jioni.
Mechi maalumu ya uzinduzi ilikuwa kati ya bingwa mtetezi Kinondoni na Dodoma. Viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo ni Tamco na Nyumbu vya Mkoa wa Pwani, na Karume na Tanganyika Packers (Kawe) vya Mkoa wa Dares Salaam.
Jana pia kulikuwa na mechi zingine za uzinduzi kati ya Temeke na Ilala katika Uwanja wa Tanganyika Packers, Kigoma imemenyana na Pwani kwenyeUwanja wa Nyumbu wakati Mjini Magharibi ilicheza na Morogoro katika Uwanja wa Tamco, Kibaha saa 2.30 asubuhi.
Hatua ya awali inachezwa katika makundi manne ya timu saba saba ambapo nne zakwanza katika kila kundi ndizo zitakazoingia hatua ya 16 bora.









Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...