Mkutano wa Kidunia juu ya Elimu ya Watu Wazima na Haki ya Kujifunza umefunguliwa mjini Malmo, Sweden Juni 14, 2011 ukiwa na washiriki kutoka karibia nchi 80 duniani. 

Huu ni mkutano wa kwanza kufanyika baada ya Mkutano Mkuu wa sita wa Dunia juu ya Haki ya Elimu na Kujifunza (CONFINTEA VI) uliofanyika mjini Belem, Brazil Desemba 2009.

Mkutano wa kwanza wa Kidunia ulifanyika nchini Tanzania mwaka 1976 chini ya uwenyekiti wa Mwl. Julius Nyerere heshima iliyotunukiwa nchi kutokana na juhudi zake kuhakikisha elimu kwa wate ikiwemo watu wazima.

Miaka ya karibuni Tanzania inaelekea kupoteza sifa hii katka safu ya kidunia kwani Elimu ya watu wazima inapata ruzuku ndogo mno na pia miundo mbinu yaliyowekwa kuiendeleza mengi imeterereka ikiwemo vyuo vya wananchi (Folk Development Colleges) ambavyo vingi vimekufa kwa kukosa ruzuku au kubadilisha mwelekeo ili kukidhi mahitaji ya uendeshaji.

Mkutano wa Kidunia juu ya Elimu ya Watu Wazima na Haki ya Kujifunza utakoma kwa kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kimatiafa la Elimu ya Watu Wazima. Mkutano Mkuu wa mwisho ulifanyika mjini Nairobi mwaka 2009.

Mkutano Mkuu wa mwaka huu una umuhimu wa kipekee kwani unataraji kuchagua wajumbe wapya katika nafasi mbalimbali za uongozi. Tanzania inawakilishwa na Mtandao wa Wanawake wa Sahiba Sisters Foundation na Karibu Tanzania Association.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...