Ndugu. Kwa mara nyingine nawakilisha ombi la kunisaidia kutangaza (wakati wowote upatapo nafasi) kuhusu Dada mdogo RENATHA BENEDICTO ambaye tumepoteana kwa takriban miaka 12 sasa.    

Renatha alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar kati ya mwaka 1998 - 2001 na baada ya hapo alienda Songea TTC kujiunga na masomo ya ualimu.    Pia alikuwa kati ya wahanga wa ajali mbaya ya Tawfiq iliyotokea tarehe kama ya leo mwaka 1999 ambapo alikuwa msaada mkubwa saana kuokoa maisha yangu. (Maelezo kamili yako http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/04/namtafuta-renatha-benedicto.html

Niliwasiliana naye kwa miaka miwili iliyofuata mpaka alipoenda chuoni Songea nami nikaondoka nchini mwaka 2003 na kwa miaka mingi sasa nimekuwa nikijitahidi saana kumtafuta bila mafanikio.   Naomba kama anaweza kusoma ama kuna anayesoma na kumfahamu anisaidie kuwasiliana naye.   

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2011

    POLE SANA.NAELEWA NI KWANN INAKUWA NI VIGUMU KUMPATA HUYO RENATHA.UMESEMA ALIENDA KUSOMEA UALIMU,KWA HIYO INAWEZEKANA KABISA KWA SASA ATAKUWA ANAFUNDISHA MAHALI FULANI.KIPINDI HICHO UNACHOKITAJA NAAMINI SERIKALI ILIKUWA IKIWAPANGA MWALIMU AKAFUNDISHE WAPI BAADA YA KUHITIMU.NJIA RAHISI KWAKO NI KWENDA WIZARA YA ELIMU WATAKUSAIDIA KUFAHAMU MKOA ALIOPANGWA ANGALAU KWA KUANZIA,UKIPATA JINA LA MKOA ITAKUBIDI UWASILIANE NA WAHUSIKA.WATAKUAMBIA KM YUPO HAPO MKOANI AU ALIPANGWA WILAYANI.NI ZOEZI GUMU NA SIO RAHISI KM INAVYOWEZA KUFIKIRIKA KWA SABABU WALIMU WENGINE WAMEPANGWA MAENEO YA PEMBEZONI SANA NA HAWANA NJIA RAHISI YA MAWASILIANO.NAKUMBUKA SIKU MOJA NILIENDA MAHALI FULANI TULIMWACHA MWALIMU KATIKATI YA MSITU AKATEREMKA NA KUPOKELEWA NA WENYEJI WAKE,,,NI NGUMU SANA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2011

    Mimi ni mpenzi wa Renata kwa sasa na tafadhali nisingependa uendelee na zoezi hili. Kama alikusaidia wakati huu sawa, binadamu kusaidiana wakati wa shida ndio jambo zuri. Kwasasa wewe endelea na shughuli zako huko ughaibuni ni sisi tunaendelea na maisha yetu ya ndoa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2011

    jamani sijui kwanini huyu dada asipatikane tu huyu kaka anamtafuta siku nyingi sana inaonekana amemtendea mema sana ndio maana hawezi kumsahau anataka kumlipa fadhila lakini kwa kuwa amesambaza habari hii katika blog nyingi anaweza akapatikana kama bado atakuwa hai pole sana unamoyo sana MUNGU atakusaidia utampata siku moja na ukimpata usiache kutuabarisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...