Habari ya kazi Michuzi,
nilikuwa na dukuduku naomba uliweke hadharani ila naomba tu usiweke hadharani na email address yangu.
Katika kipindi cha michezo cha clouds nakumbuka miezi 2 iliyopita walikuwa wanauliza maswali na kuwaambia watu wanaotaka kujibu watume ujumbe kwenda namba 15556. Sasa baada ya lile zoezi la maswali kuisha ikatokea wiki iliyopita nimetumiwa ujumbe na SHAFII kuhusu michezo ya ulaya na wakatuma ujumbe jinsi ya kujitoa.nikatuma ujumbe wa kujitoa sababu sihitaji kuendelea kupata ujumbe wa michezo ya ulaya au tetesi zozote kuhusu michezo ya ulaya na hata ya hapa nyumbani kupitia simu.Baada ya kutuma ujumbe wa kujitoa PUSHMOBILE wakanirudishia ujumbe kuwa wanashukuru kwa ujumbe wangu na nitaondolewa baada ya masaa 24. Lakini tangu nitume ujumbe huo bado nimekuwa napokea SMS toka kwa SHAFFI kuhusu michezo,ilihali nimeshajitoa na pesa yangu inakatwa.
Sasa naomba uweke hii hadharani ili PUSHMOBILE wafanyie kazi dukuduku hili. Wale waliotaka kujitoa kupokea ujumbe wawatoe wasiwang'ang'anie kwani pesa imekuwa ngumu na vocha tunaweka ya Tsh 500.
PUSHMOBILE naomba sana mnitoe nisiendelee kupata ujumbe.
Ni mimi mdau mlalamikaji.

Uncle usiweke wazi email address yangu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2011

    Ninaungana na mdau moja kwa moja maana hata mimi yamenikuta kiasi cha kufikia kubadili mtandao kwaajili ya kubana matumizi. Nikweli nilijiunga kwa hiari yangu na pia kujitoa ni hiari yangu na matakwa yangu. Sioni kwanini hawa push mobile wawe na uhuni wa kiasi hiki hata kufikia hatua ya kupitishia uhuni huo clouds fm. ninapata wasiwasi kwamba hawa push na clouds ni kitu kimoja kwa maana ya kwamba wananufaika pande zote. ni mbaya kwa kituo kinachojiita redio ya watu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2011

    Dah! Jamaa wanachukua pesa hata kama unataka kujitoa, hawataki usijitoe! Dawa yao ni ubadili simcard, najua jamaa zako wengi wanatumia hiyo namba, lakini hawa pushmobile ni wezi sana. Huyo Shafii yeye mwenyewe anazisoma kwenye internet, yanini kulipia?

    ReplyDelete
  3. GODWILL AKILIMALIJune 11, 2011

    Jamani watanzania kwa hali hiyo tutaweza kupigana na umaskini kweli! au ndo kuongezeana umaskini!!!!!! Kwa sisi wenye mitandao walaa hata haitusumbui kupata habari. ya nini kujitesa na hizo sms. saiv mambo ya mtandao banaaaa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 11, 2011

    Yaani nimecheka huyu mdau halo leta hili swala la Push Mobile eti wanamuibia ee ana maneno ya kufurahisha sana,na waliotoa comments utafikiri wote darasa moja,yaani baada ya kuwaoneeni huruma nimecheka sana,inaonyesha hao watu wa push mobile na clouds wamewafika kooni,,,,eeh poleni sana mimi nakumbuka zamani nilikuwa nakatwa kuhusu milio ya music,na kuulizwa maswali ya ajabu katika mtandao wa tigo,,nilikuwa nikiwatumia sms kuwa jamani sasa nyie mnanitafuta mimi sitakisitakiacheni kunikata pesa,,naona hiyo ni biashara ya kulazimishana,,ee heshima ya clouds itaisha ongeeni na wakurugezi wa clouds kuwa sasa mtawatangaza katika magazeti kuwa ni wezi,,sasa sijui hiyo push mobile ni mtandao gani?,,,ee mmenichekesha sana nyie watu!Ahlam UK,,,,,,Nimemiss sana home

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 12, 2011

    hiyo kitu ni ndogo sana rafiki uwe na kadi mbili, moja tigo ni ya kupigia simu ya pili ni hiyo usiweke vocha ila ya ya kupokelea, ukiwajulisha tumieni number mpya ukishaona wote wameshajua unavunja kadi kisha unawaacha kwenye mataa watu wa Push.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...