Hi braza Michu!
 
Kwa kifupi mimi ni mdau wa blog yako na haipiti siku bila kuisoma blog yako. Sasa bro naomba unitolee tangazo langu kwenye blog yako kama ifuatavyo:
 
Mimi ni Mtanzania lakini nina Uraia wa Kijerumani, Kidini  ni Mkristo ,kwa jina naitwa Andrew, nina umri wa miaka 43, nimezaliwa Kinondoni na kusoma hapo Bongo Tambaza na hatimaye Old Moshi. Kwa sasa naishi Ujerumani kwa muda wa miaka 25 na nafanya kazi Berlin kama Enginer wa design wa Mashine, baada ya kukaa kwa muda mrefu na mke wa kizungu na kushindwa kupata mtoto nimeamua kutafuta mke wa kutoka Tanzania lakini  ambaye yuko hapa Ulaya(European countries) katika nchi yoyote ile, awe si chini ya umri 28, asiwe na watoto zaidi ya mmoja, awe radhi kuishi na mimi , kuzaa na mimi,na kuoana na mimi na kujenga familia ya kimapenzi  ya ukweli. Awe na uwezo wa kuongea walau Kiingereza na sio chini ya kidato cha nne.Awe mkweli na muwazi, mtulivu na heshima,
 
Kwa maelezo zaidi na mazungumzo ya karibu  naomba mwanamke yeyote mwenye  nia kama yangu na kukubaliana na hayo niliyoandika awasiliane na mimi kwa email hii:
 
 
Simu namba nitatoa baada ya kujibu barua pepe!!! na email isio na picha haitajibiwa na mimi picha zangu zitaletwa na majibu ya email yake.
 
Natanguliza asante zangu na naomba tu wale wasichana au wanawake walio serious na maisha  wanijibu!
 
Kazi jema!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2011

    mimi nipo ENGLAND, kidato cha nne sijafika ila naongea english mpaka utakoma mwenyewe, na kazi yangu napiga box, umri ndio naingia 28 sijaolewa wala sina mtot sasa vipi tuyamalize au mpka niwe na certificate atleast ya f4?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2011

    sasa kweli utanipenda mimi au kwa sababu ni baby mashine, shida yako mtoto tu, na mtoto anetoa na kukujaalia ni M'Mungu peke sasa kama sitojaaliwa kwa kipindi amabcho nitakuwa na wewe jee itakuaje itabidi uniache utafte mwengine si ndio.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2011

    usisahau kupima.....

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2011

    Mdau rudi bongo ukaowe, wanawake wa kibongo wanaoishi EU hawana heshima, ukweli wala utulivu. Wanataka maeuro tu kwa kwenda mbele. Umnunulie gari mpya na umlipie mortgage. Je utaweza hayo?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2011

    Wewe mapenzi unayajua? Kwahiyo ina maana na huyo mwingine akishindwa kupata mtoto naye utamwaga kama ulivyomwaga huyo mzungu? Au usikute wewe niye una matatizo? maana saa zingine wanaume unakuta "Paka hashiki Panya" halafu wanawasingizia wanawake...kipare tunasema "Mnyawi teugwira ngoswe"....!! Mimi simshauri mwanamke yeyote amkimbilie huyu jamaa..labda kama ni kwenda kumchuna tu....!!

    ReplyDelete
  6. Miaka 43? nyama kala mzungu halafu makombo unawaletea dada zetu. Kina dada kuweni makini sana na watu kama hawa. Watu wa dizayni hii ni "majhnuuni" au "wehu". Hawa ndiyo watu walipokuwa vijana walikuwa wanasema "mwanamke mweusi wa kazi gani bana....?" kwa sababu alikuwa na nguvu za kufanyishwa kazi na mwanamke wa kizungu. Sasa nguvu zimemwishia ndiyo akili zinamrudia na kuanza kuuona umuhimu wa watu wake. Kama una njaa na unadhania mtu kama hii itaondoa matatizo ya njaa yako, then YES, he is your ideal man. Lakini kama unataka mpenzi wa kuogelea naye kwenye ulimwengu wa mapenzi basi huyu mtu muogope kama ukoma.

    Na kama shida yake ni mtoto tuu, kwa nini asijaribu na mjerumani mwingine?
    Isitoshe amekaa ulaya miaka 25, jee amewahi kwenda kupima kama yeye mwenyewe anao uzazi? au bado ana zile akili za kale kwamba mgumba ni mwanamke tuu?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 06, 2011

    kaka nichukue mimi ninakizazi acha kabisa. Umri wangu ni 30 nina watoto 6. Nitawaacha watoto 5 home nitakuja na mmoja tu ili kukidhi mahitaji yako. nakwambia hutajuta kunioa maana shida yako itatimizwa mara moja. Elimu usitie hofu nina degree 2 na sasa namalizia ya 3. Kiingereza, kijerumani, kizaramo, kikwere na kiswahili ni lugha ninazoongea kwa ufasaha. Mdau hutajuta kuwa na mimi. Mama Xoli. Mtanzania Original

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 06, 2011

    Na huyo bi mkubwa ushampa taarifa kuwa umeamua kutafuta jiko lingine au atakayekuja atakuwa nyumba ndogo? Anayekuja naye asipokuzalia mwana je?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 06, 2011

    je kama wewe ndo mwenye matatizo mimi niko hapa ujerumani na nina mtoto mmoja lakini kama nikiwa na wewe na sitofanikiwa kupata mtoto na wewe itakuwaje? utaniacha kama mzungu wa watu ambae unamuacha bila sababu za msingi. maana kama unamuacha kisa hana mtoto kweli hata ukipata mwingine hutapata huyo mtoto. na ataolewa na mwanaume mwingine na mungu atawajalia watoto. Acha ushamba NDOA SIO WATOTO

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 06, 2011

    kwa hiyo utakapokosa wa kukupatia mtoto unaachana nae? na ukumbuke kwamba mtoto ni zawadi itokayo kwa Mungu hivyo unapaswa kumwomba Mungu kabla ya yote.mimi nina miaka thelathini na nimemaliza form four na sijui kiingereza itakuwaje utanikubali?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 06, 2011

    pole sana kaka, vp unahitaji wakristo tu?? maana mi ni muislam lakini sina tatizo kuishi na mkristo. nina mastaz na nipo bongo.nipe invitation basi, nina miaka 34. chukua e-mail kwa kaka michuzi basi...!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 06, 2011

    Na wasiwasi tu na sababu uliyotoa kuachana na huyo uluekuwa naye kwamba hamkupata mtoto. Tatizo lililuwa nini? Wakati mwingine kupata mtoto ni majaaaliwa na huko germany uliko kuna njia nyiiiiingi za kisasa kutatua hiyo shida. Je, ukipata mke mpya na msipopata mtoto itakuaje? Hii itamfanya utakayempata awe na stress kupata mtoto ili aendelee kuwa na wewe!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 06, 2011

    sister wangu anatafuta mchumba, ana umri kama 35 hivi, anataka kuolewa na mtu mzima alie tulia. English kidogo anajua, kajiendeleza anaishi Dar yupo tayari kupima.
    Anawatoto 3 ila wapo kijijini kwa bibi yao, wa mwisho anaishi nae mwenyewe.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 06, 2011

    Haloooooooooooooooo Habiri ZENYU bANNAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...