HABARI MKUU,

NAOMBA UNIFIKISHIE KILIO CHANGU KWA WADAU WA BLOGU HII KWANI NIMEPATWA NA KIHORO BAADA YA WALE WATAALAM WA KUVUNJA VIOO VYA MAGARI NA KUIBA KUVAMIA GARI LANGU, KUVUNJA KIOO CHA UBAVUNI NA KUIBA MKOBA WA LAPTOP AMBAO ULIKUWA NA VITABU VYA SHULE NA DOCUMENT MBALIMBALI MUHIMU.

NAWAOMBA WANA BLOGY HII KAMA KUNA YEYOTE ALIYEWAHI KUIBIWA ANIPE MBINU NI JINSI GANI NAWEZA KUZIPATA HIZO DOC HATA KWA KUTOA MKWANJA
KWANI NI DOC. MUHIMU

NAPATIKANA KWA NAMBA HII 

0713 777-404

MDAU PROSPER. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2011

    Duh! Pole sana mdau. Kwa vile hizo document ni muhimu sana na uko tayari kutoa mkwanja kuzipata. Basi cha kufanya urudi maeneo hayo hayo ulipoibiwa utangaze dau kwa vijana wa maeneo hayo. Maana yake ni kuwa hao vibaka hawatoki mbali ni wa mitaa hiyo hiyo. Mara nyengine usiacha mkoba ndani ya gari. Sasa TZ vibaka wakiona tu mkoba ndani ya gari basi hatafunja kioo na kuchukua huo mkoba. Dah! Hatari. Vibaka banaaaa.

    ReplyDelete
  2. Prosper.
    Kwanza pole sana kwa tukio hilo. hakika inauma sana jinsi wanavyofanya hao wezi wa mtindo mpya wa siku hizi unaofanywa na vijana wa kipemba na wengineo. Mimi pia niliwahi kuibiwa kwa mtindo huu na ilibidi ninunue tena vitu vyangu vyote na nilishukuru kupata kila kitu.
    Nenda pale msimbazi pembeni ya BIGBON / kona ya mtaa wa mafia. Ulizia vijana wa pale kuna mmoja anaitwa TALL, mwelezee uliibiwa wapi na huyo anaweza kukutafutia kama utamuahidi dau nzuri kulingana na umuhimu wa vitu vilivyoibiwa.
    Tunatarajia utazipata tu.
    Pole sana.
    Mdau Naushad.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2011

    Bongo bwana eti mdau anaamini kuwa vioo vya gari vikifungwa vinaweza kuzuia wizi!

    Ulaya wenye kuendesha gari kama hapa Uingereza hakuna mtu anayebakisha hata koti ndani ya gari lake, kila kitu huwekwa ktk buti la gari kuanzia makoti ya mvua, baridi mpaka vitu vya gharama kama laptop au dokumenti muhimu ili kuzuia kuwapa tamaa wahalifu.

    Jifunzeni kuwa vioo vya magari siyo 'sefu boksi' ya kuzuia uhalifu bali huchangia wahalifu kujaribu bahati kirahisi.

    mdau
    jijini London.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2011

    Hapa tunaona wezi wanajulikana kwa majina mapaka wanapopatikana! Inakuwaje bado wanadunda?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2011

    wewe Anonymous Mon Jun 13 03:27 badala ya kutoa solution wewe unaleta habari za wabongo bwana kama huna la kuongea nyamaza kaa huko london beba maboksi tu achana na discussion za watu ambao hawajakata tamaa. Hio sio ishu ya bongo wala nini wezi hawatakiwi kuwepo popote.

    Wewe hiyo sefu boksi unayo acha ushamba usio namaana toa solution au funga bakuli.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 13, 2011

    Mdau wa pili sijui inakuwaje mpaka unawataja wapemba ktk suala hili.Sidhani kama ni sahihi kuzungumzia jambo baya na kutaja kabila fulani hebu tuwe na utu jamani.Hizo ni mentality mbovu zisizo na sifa nzuri hasa ktk karne hii ya 21.Usidhani kama utakuwa unaukabila na ikawa ni jambo la kujipongeza,nadhani ni kupoteza malengo mazuri kwa jamii.Ustaarabu haununuliwi ila ni kitu cha bure.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 14, 2011

    wewe mdau wa London semea watu wa london na sio Uingereza yote.naishi nje ya london na ninaacha koti na documents kwenye back seat all the time na haviibiwi. sasa unaposema ulaya wakati hata uingereza yenyewe hujaimaliza unadanganya uma. kwanza haikuwa na haja kuanza kuelezea ya ulaya sijui uingereza wakati jamaa aliyeibiwa yuko Bongo..
    nways, mdau uliyeibiwa documents,siku nyingine jifunze kuondoa vitu vya maana kwenye gari lako manake bongo wote twaijua, hakuna kisichoibiwa..kila la heri.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 14, 2011

    jamani pole kaka naomba mtoe hoja za kumsaidia mwenzenu malumbano yaninai

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...