Msanii Francia (kulia) akiwa na Meneja wake Shelamina(kushoto), pamoja na Mtarajiwa Bi Lilian Saidi
 Muandalizi mkuu na Mlezi wa Bi harusi mtarajiwa Bi Anande Daniel
 Ma MC wa sherehe ya Jikoni Bi Susan Mzee na Makrina Kalinga
Wageni ktk Sherehe ya jikon
 Bi harusi mtarajiwa na Mpambe wake, wakimeremeta
 Dada Maureen na Mariam nao walikuwepo ktk kumfunda mwali huyo
Mtarajiwa na mpambe wake wakisikiliza kwa makini mafundisho kutoka kwa wanawake wengine


Wanawake wa mji wa Reading, UK jana walikusanyika pamoja ktk Kumpa mawili matatu Mtarajiwa  Lilian Saidi, anaetegemewa kuolewa hivi karibuni na Bwana Paul Mhando.


Kama kawaida yao wanawake hawa wenye ushirikiano mkubwa sana, walichanga pesa na kufanya sherehe hii ya jikoni, ili kuongea na binti huyu mrembo kuhusu maswala ya ndoa.

Ama kweli wanawake hawa wana mafindisho mazuri, kama hauamini basi hudhuria siku moja kwenye sherehe hizi za jikoni. Na kwakweli tunaona matokeo, kwani ndoa nyingi huko Reading ni moto wa kuotea mbali. Tuige mfano huo.



-Imetolewa na Mdau Mlondoner

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2011

    kaazi kweli kweli.....

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 14, 2011

    Je hao maharusi ni wabeba boksi au watoto wa wabeba boksi?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2011

    Bi harusi mtarajiwa ni mrembo kweli! tunategemea atafuata maadili ya ndoa, mji wa kusoma ni mji wa wana ndoa waliodumisha ndoa zao!big up!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...