Serikali imeombwa kuangalia uwezekano wa kutunga sheria za mavazi ili kusaidia kuwadhibiti wale wote wanaojihusisha na uuzaji na uvaaji wa nguo zisizozingatia maadili, silka na utamaduni wa Mzazibari. 

Taarifa ya Afisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, imesema kuwa ombi hilo limetolewa na wananchi shehia mbalimbali wakati wa ziara ya Maafisa wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi za kuwaelimisha wananchi juu ya Polisi jamii na Ukamataji salama wa watuhumiwa. 

Wakizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Nyerere eneo la Sebleni mjini Zanzibar, Viongozi hao wamesema kuwa nguo fupi na zinazobana maungo kwa mabinti na zile za kuvaliwa chini ya makalio kwa vijana wa kiume zimekuwa zikiwazalilisha na kupotosha maadili ya wakazi wa visiwa hivyo. 

Akijibu hoja hizo, Msaidizi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar SP Mukini Mohamme Ali, amesema kuwa pamoja na ombi hilo lakini ipo haja ya wazazi na walezi kudhibiti nyendo, liugha chafu na tabia mbaya zinzofanywa na watoto wao wakiwemo mabinti na wavulana ili wasipotoke na kuipotosha jamii. 

Naye Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Mjini Magharibi SSP Ahamada Abdallah Khamis, amewakumbusha wananchi kutochukua sheria mkononi kwa kuwaadhibu watuhumiwa na hata kuwaua kwa vipigo wanapowakamata. Mkuu huyo wa Upelelezi amesema kuwa kwa siku za hivi karibuni kumezuka tabia ya wananchi kuwapiga, kuwatesa na hata kuwaua watu wanaowatuhumu kufanya makosa ya kihalifu kwenye jamii zao. 

Maafisa hao wakiongozwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, tayari wameshazitembelea shehia 53 kati 74 zilizopo katika mkoa hua kwa lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya mpango wa ulinzi shirikishi na Ukamataji Salama wa wahalifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2011

    NApenda wwazanzibari walivo na msimamo! na kwa mantiki hii hakuna atakaeweza kuibadili Zanzibar ...kazeni buti InshaALLAh ntafanikiwa ! wamezoea kubadili maadili ya watu, dares salaama a sasa si ile tunayoijua! roho mpaka inauma ! lakini MSIKUBALI MSIKUBALI na mkumbuke ile aya inayosema " hawataridhia mpaka mfuate mila zao " basi msikubali

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 16, 2011

    Hapo ndipo nawakubali wazanzibar, jamaa wanajua kuenzi maadili yao sisi huku bara tunapenda kuiga watu wasio na tamaduni na kujifanya tunaenda na wakati

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 16, 2011

    Hoja hii ya wazanzibari naiunga mkono 100 kwa 100. Zanzibar ni nchi ya kiislam tukitaka ule ukweli, bara wana-enforce mila na desturi zao kule unguja na pemba, mimi binafsi nilishangaa sana nilivyo kwenda Zanzibar nikakuta makanisa yalivyo shamiri, huu ni uchokozi wa hali ya juu na ni dharau kwa wazanzibari, haishangazi kuona wazazibari kukataa muungano, angalia pwani ya bara ilivyotekwa na watu wa kuja na maadili kuharibika. Zamani ulikuwa humuoni mtoto wa kike kutembea nusu uchi, sasa ni kawaida haya si maadili ya pwani.

    ReplyDelete
  4. MUANZE KUTUNGA SHERIA ZA WATU KUTEMBEA USIKU WAVAE NGUO KAMA WANAZOVAA MCHANA NA KWENYE SHEREHE ZA USIKU WATU WAVAE KAMA MCHANA.
    NA WALE MASHOGA WANAOVAA NGUO ZA KIKE USIKU NAO ITUNGWE SHERIA ILI HIWE SAWA NDIO MIMI NITAKUBALI ZANZIBAR NI NZURI KWA MAADILI

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 16, 2011

    pumbavu nini?!!!there is a term called freedom jamani..eeeh

    ReplyDelete
  6. Tanganyika guwezi kufanya kuwa nchi ya kislamu kwa sababu ina makabila mengi sana na dini zao tofauti,kuweka sheria za kislamu kwa tanganyika naona itakuwa ni vita dini ya waislamu na madhehebu mengine.

    Kama munakumbuka uchomaji wa moto kwa yale mabanda ya watanganyika kule pwani mchangani ni kwa sababu ya maadili,walivuka maadili ya wana kijiji,lakini watu walilichukulia kisiasa.

    Ukweli utakuwepo pale pale. Na utadhihirika.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 16, 2011

    Kwanza nani kakwambia Zanzibar ni nchi ya ki Islam we Anon hapo juu,nyinyi ndio wachochezi wenyewe.
    Zanzibar inategemea sehemu ya pato lake kutokana na utalii,sasa ukianza ku limit watalii wavae nini itakuwa shida.Watalii wanatoka ndani na nje ya Tanzania,hivyo yatupasa kuwa makini sana na sheria tunazozitunga ili zisituumize wenyewe.Kama wewe hauwezi kuvumilia ukimwona mwanamke kavaa short pants basi fumba macho au jifungie chumbani.Tanzania is the free country with both Muslim and christians and people with different cultures.Tuiache nchi yetu jinsi ilivyo na ndugu zangu Waislam acheni uchochezi.Nawapenda wote.Mtanzania.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 17, 2011

    maadili gani hayo? ndio nyinyi mkiona watu waliovaaa nguo za kubana mnawamezea mate toeni unafiki hapa.wengi hapo wanao kubalian na hayo maoni ni wanafiki na mafuksa. zanziba ni ni jimbo, sio nchi na haita kaa iitwenchi. Zanzbar inategemea mapato ya bara ilikulipa misharahara ya wafanyakazi wao. sasa kama wajanja wavunje muungano waone moto wao. kama munataka kuvaa hayo makazu yenu na baibui nendeni uarabuni sio mnakimbilia bara au huku ulaya. nendeni middle East tujue moja. wengine tunafurahia kusafisha macho kwa kuona mungu alivyo umba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...