HABARI ZA LEO MDAU?
NATUMAINI UNAENDELEA VIZURI NA MAJUKUMU YA KUJENGA TAIFA HEBU NAOMBA UWAANDIKIE WADAU KWA WALE WANAOHITAJI KWENDA LOLIONDO KWA BABU KWA USAFIRI WA ANGA KAMA NDEGE AU HELIKOPTER WANAWEZA KUWASILIANA NA MIMI
HUWA NA ARRANGE SAFARI ZA HUKO.HIVYO KWA YEYEYOTE AMBAE ATAPENDELEA ASISITE KUWASILIANA NA MIMI NIMPE TARATIBU ZOTE HUSIKA,AU KWA KIFUPI UKIONDOKA ASUBUHI UTAFIKA KULE UNAPITA VIP ROUTE MPAKA SAA TANO ASUBUHI MNAKUWA MMESHARUDI.SHUKRANI MDAU KWA MAWASILIANO MSISITE KUNIPIGIA KWENYE NO ZANGU NI
0787 415 145.
Hivi habari za Babu wa Loliondo mbona zimepotea kwenye Magazeti na vyombo vingine vya habari? Kikombe kieishiwa nguvu? Waandishi vipi kama hicho Kikombe ilikuwa zuga ya Babu si mtuambie? Na kwa nini msifanye utafiti wa kutujuza wagonjwa wanaendeleaje ili na wengine tuhamasike kwenda? Maswali ni mengi. Bongooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteKWA MAONI YANGU, HUU NI UNYANYASAJI KWA WALE WATU WA CHINI WASIO NA UWEZO NA AMBAO WAMEKAA FOLENI KWA MUDA MREFU KUSUBIRI HUDUMA YA BABU. KAMA MAHOSPITALI MAKUBWA WALALAHOI HAWAPATI NAFASI KWA SABABU YA WATU WA JUU NA WENYE UWEZO KUPITA NJIA YA 'VIP'..SASA JAMANI HATA HUKU KWA BABU TUNAKOENDA KUPONEA WATU TUSIOJIWEZA MNATAKA KUTAKATIZIA? MUNGU HATA PENDA NA HATA HIYO DAWA HAITAFANYA KAZI KWA MWATU WA NAMNA HIYO. NATOA SAMAHANI LAKINI HAYA NI MAONI YANGU NA NAOMBA UYAWEKE NA WADAU WENZETU WENGINE WACHANGIE MAWAZO.
ReplyDeleteBY ANONYMOUS ALLEN NATAI ;)
Bongo tamabarare!!!
ReplyDeleteEti VIP Route, ufisadi mpk kwenye foleni ya kikombe cha Babu. Na alishasema ukienda kitajiri huponi, Bongo kweli Tambarare !!
ReplyDeletesasa ni wangapi waliopona? tunaomba ushuhuda
ReplyDeleteUsizungumzie wangapi waliopona ulizia wangapi wameisha kufa. waliopona ni zero na waliokufa ni kwa maelfu. na bado watu wanatafuta biashara ya kwenda kuua wengine kwa njia ya VIP.
ReplyDeleteHamna UVIP kwa babu na alisema wakati mie nilipokuwa huko nikasikia kwa masikio yangu. tena akasisistiza kwamba ukifanya hivi utakuwa umekunywa juice. Msidanganye watu jamani. Utakwenda KIVIP ila utarudi na magonjwa yako mana utakuwa umekunywa juice.
ReplyDeleteIsitoshe sasaivi kule hakuna foleni mie niliunganisha siku hiyo hiyo toka dar na sikulala Arusha nikafika loliondo kumi usiku na saa nne nikawa nishapata kikombe nikageuza kuridi Arusha mda huo nikafika kumi jioni. Tena nilienda kwa usafiri wa jumuiya (public Trans). So msidanganye watu.