Benjamin Sawe na Beatrice Mlyansi - Maelezo,Dodoma

Serikali imemwagiza Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya ukaguzi maalumu kwenye maeneo ambako utaratibu wa vocha za pembejeo za kilimo unatumika ili kuwachukulia hatua wale watakaobainika kuhujumu utaratibu huo

Akibu Swali kutoka kwa Mbunge wa Mbozi Magharibi Mheshimiwa David Silinde la ni hatua gani itachukuliwa kwa wahusika wanaotoa pesa kwa wanacnhi badala ya Vocha,Waibi Waziri wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Injinia Christopher Chiza alisema hatua mbalimbali zimechukuliwa dhidi ya wanaokiuka taratibu hizo.

Injinia Chiza alisema Serikali imewafutia mawakala 168 kutoka mikoa ya Rukwa,Mbeya,Morogoro na Ruvuma pamoja na kufungua jumla ya kesi 22 katika mikoa ya Rukwa,Mwanza,Mara,Morogoro,Manyara,Kilimanjaro,Iringa na Mbeya.

Aidha Injinia Chiza alisema mfumo wa ugawajiwa vocha za pembejeo za kilimo uliopo kwa sasa unaonekana ni mzuri zaidi ukilinganisha na utaratibu wa zamani ambapo serikali iliingia mikataba na makampuni binafsi ya pembejeo za kilimo ili pembejeo hizo kwa wakulima.

Alisema kwa utaratibu huu wa sasa Vocha zinafika hadi vijijini na kugawiwa kwa wakulima walengwa kupitia kamati za vocha.

Alifafanua kuwa wauza pembejeo kwa sasa wanalazimika kufikisha pembejeo za kilimo hadi vijijini ambapo wanunuzi wanapatikana ukilinganishwa na wakulima kufuata pembejeo Wilayani kabla ya utaratibu wa sasa kuanza.

Alisema mapungufu yanayojitokeza hivi sasa ni kutokana na usimamizi hafifu katika ngazi husika za kamati za vocha ambapo Wizara yake inazisisitiza kamati za vocha za Wilaya,Kata na Vijiji kuzingatia maelekezo yaliyotolewa katika waraka wa usimamizi wa utekelezaji wa mpango wa ruzuku ya pembejeo za Kilimo kwa utaratibu wa vocha katika msimu wa 2010-2011.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...