Ankal Mithupu,
Asalam alaykum, jana nililkua navuka narudi kwangu kule kwenye beach mwanana za Kigamboni, nikakutana na hizi mashine za tozo ya kivuko, mie sijui kwa kidhungu zinitwaje! Nikajiuliza hizi si alipewa mtu zabuni kuleta toka huko kwa wadhungu na kuziweka pale kwa kodi za wavuja jasho wadanganyika, sasa ni miaka kadhaa hata kazi hazikjafanya, hivi hawa TAKUKURU wanafanya kazi gani?, jamani hata hili linahitaji uchunguzi!? CAG fuatilia ubadhilifu huu.

Pili ankal, siku hizi kumekua na foleni kubwa mpaka inakera, hawa jamaa wa miundombinu sijui wanafanya kazi gani, JK kaleta kivuko kazi wanafanya wanavyotaka wao, asubuhi ukitoka Kigamboni, inabidi ufike kivukoni kaba ya saa 12 asubuhi ili uwe na uhakika wa kuvuka mapema uwahi kazi saa 1.30 asubuhi mjini, tatizo kubwa ninaloliona mimi hapo ni kuwa kuna foleni tatu za magari, ya kwanza ni wale wenzangu na mie tusiotaka kujikweza tunapanga foleni na kulipa hela ya kivuko, ya pili ni wale wanaopita njia ya NO ENTRY ambayo hutumiwa zaidi kwa dharura kama ambulance, sasa nashangaa njia hii hutumiwa hata na mbunge, madiwani na wengine ambao hujiita mashuhuri huko kwetu kigamboni, na ya tatu ni lile mlango wanaotumia jeshi, huku napo kuna kaufisadi kidogo, gari za raia hupita huku pia, kwa kumuona kinamna muuza magazeti pale unamwachia buku then muuza magazeti anamstua askari jeshi ambaye anafungua geti kwa  huyo mteja, kwa hiyo hii hali inakera sana.

Sina Mengi niwekee hii wadau wachangia maana Bongo kila mtu ana lake
Asante ankal usiniweke kapuni.

Mdau Mbegu, Kigamboni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2011

    KWAKWELI HALI YA FOLENI KGAMBONI SASA HIVI INABORE SANA, WATU WA PANTON WANAAMUA TU LEO PANTONI ZOTE MBILI ZIANZE KAZI PAMOJA MAPEMA AU WAKIJISIKIA PANTONI MOJA IANZE NYINGINE IANZE SAA MOJA!! KWAHIYO HUWA NI KERO TUPU,TUNATAKA SERIKALI ITUAMBIE LINI DARAJA LITAANZA KUJENGWA,TUNAPATA SHAKA KWAKUWA PESA NYINGI INAINGIA KUPITIA KIVUKO LABDA NDO SABABU INAYOPELEKEA KULEGALEGA KWA KUJENGWA KWA DARAJA. IKUMBUKWE KUWA KWA SASA WATU WENGI SANA WANAJENGA NA KUHAMIA KIGAMBONI HAITAKIWI KUTEGEMEWE KIVUKO TU.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 02, 2011

    Hongera Mdau kuweka wazi dhuluma unazoziona. Tuige hivi watanzania wenzangu, kufichua kila ufisadi/ujanja ujanja/uzembe/kero/ukwepaji kodi nk. Hii ndiyo njia pekee ya kurekebisha mambo, tuchukue hatua wenyewe!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 02, 2011

    Ankal salamu aleko !

    Huyu mdau hapo juu amenena KERO ambayo kwa kweli sisi wakazi wengi wa kigamboni tunayo! kwa kweli tokea mwenzi May uingie ni foleni kuja mjni na kurudi nyumbani unachukuwa kama masaa matatu mpaka manne kwenye folen! na ukienda siku nyingine kunakuwa hakuna foleni, saasa mtu utajiulza iweje jana kulikuwa hakuna folen leo namna hii? ukiuliza sana unaambiwa WANA MGOMO BARIDI ....juzi tu tumesikia kuwa wamejiwa juu na wizara baada ya mhishimiwa mgufuli kutembelea kivukoni, wameambiwa kuwa mapato yanayopatkana ni madogo kuliko uhalisia wenyewe! nasikia ndio wanayaendesha mapantoni kwa mwendo wa taratibu "tara ra ra ra" taratiiiibu na kama hiyo haitoshi na magari yanayopakiwa yanakuwa machache ili folen iwe kubwa! wanasema ili safari ziwe nyingi na ijulikane mafuta yanatumika sana na ifkie ile hesabu yao ya kukusanya million 7 kwa mwenzi kama walivodai NIMESKIA yote hapo nanukuu , maana ukiwa mle ndani ya panton mmebanana kila mmoja utamsikia anasema lake! lakini kwa kweli hawa watu wana makusudi sana sana sana ! inafikia wakati mpaka unaliza hvi hii nchi ina RAIS kweli ??? ina waziri wa miundo mbinu ??? ina wizara??? maana wale watu wanajifanyia watakavo ! na wale ma askari walowekwa wote wanasalimu amri za wakubwa wa pale wanavoamrisha!

    tukija kwenye suala la mageti ! mdau hajaongopa! kuna njia tatu, moja ya kina sisi PATA SOTE , kuna njia ya ma askari ambayo inatokea kwenye vituo na kuna njia ya emergency kama kuna mgonjwa ! utashangaa sasa hivi hakuna utaratibu maalum, kila mtu awe nani au nani anapita mradi unamtipu askari anakupisha! jamani inakera pale wewe wa kawaida unaposimamishwa lakni yule alotoka geti la emergency ametishwa! ukiwauliza wale wakata ticket WANALALAMIKA na wanasema hata wao hawapendi lakini ni amr ya wakubwa zao! wanasema kuna watu wa intelligencia wanapita kule wana kazi maalum, lakini hapo hapo wanasema hata WAKE ZA HAO watu mume amelala nyumbani yeye wala si mfanyakazi wa huko anapita hapo! STK , DFP , SU na kadhalika! sasa sisi pata sote tunajiuliza je kama wafanyakazi wa serikali wakihamia kigamboni ! sisi pata sote tutavuka saa ngapi??????? maana mpaka kwanza waheshimiwa wa serikali waanze kuvuka , ndio sisi wengine tena tunaingia! pili labda tuwe tunaamka alfajiri sana kuvuka!

    Hoja:

    Kama wao watu wa serikali ni muhimu wanahitaji kuwahi nadhani nassi wafanyakazi wa kawaida ambao tunalpa KODI za kuwalpa wao pia tuna umuhimu wa kuwahi kazini! sisi tunalipa kodi nyingi sana kulipia serikali iweje nasisi tusiwe muhimu???? pili tunalipia kivuko cha kuweka mafuta ! kwa hyo sisi pia tuna umuhimu wetu! jamani Ankal TUNAOMBA UTUFIKISHIE UJUMBE WETU KWA MHISHIMIWA RAIS hali kigamboni ni mbaya! na wale watu wanafanya makusudi! na tokea umeanza mwenzi huu wa MAy!

    mapantoni mawili yanatosha sana kama watasimamia vizuri! mbona wakati mwengine wanawahi???? na pia tunaomba geti la dharura wapte wagonjwa tu na mbunge! wengine wote tupange folen.

    Upande wa pili kusimamiwe na askari katika kila baada ya hatua fulani! yaani upande wa dar huku ferry, maana mnakaa folen wanakuja watu ambao wao siku zote hawataki kukaa folen wanajichomeka mbele! matokeo yake nyie mlokaa folen tokea saa kumi na moja mnajikuta mnafika nyumbani saa tau mpaka nne usiku! kwahiyo wakamatwe na warudishwee nyuma wakaanze folen!

    kuna tabia imeanza sasa hivi huku kituo cha police ferry, wanaenda police kujifanya kupark , sina hakika wanaongea nini na police mara police anakuja anawazuia ili mumpishe yule mtu alokatiza folen! jamani tusadiwe watu wa Kigamboni

    ankal usitie kapuni ...tafadhali tufikishie ujume wetu huko Mbele , nna imani unaweza....Allahu Barik

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 02, 2011

    wazee wa yale yaleeee na teknohama!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 02, 2011

    Ankal nimeandka comment ndefu sana nimesahau hli swala muhimu sana!

    Siku za Jumamosi! ni KARAHA TUPU!!!! siku za jumamosi pantoni linakuwa moja! mpaka saa nne au waone fujo zimezdi ndio wanaanzisha la pili! ukifika pale saa moja kuvuka kuja mjini WALLAHi UNAFIKA SAA NNNE!!!! ni vurugu vurugu vurugu! waheshimiwa wanakuja kwa gate la emergency! waheshimiwa wanajeshi nao kweny geti lao la wanajeshi! ss pata sote tusubri! wanaona kuwa watu wana jaa ! wenye mikokoteni, baskeli na tuk tuk! nyomi ya watu nayo ! lakini THEY NEVER CARE!!! na wale ma askar wa kukodi ndio wanataka siffa! wanaona raha sana nyie mnavolalamika wao WAMEVAA MIWANI YAO MEUSI !!!! WANAKERA!!!! UNATAMANI USHUKUE UWAZIBUE MAKOFI!!!! AAAAAh karaha kaka michuzi ! tufikishie na huu ujumbe sku za jumamosi madude yale yaanze kwa wakati mmoja jamani! Kigamboni ya zamani S YA SASA! sasa tunashangaa na hivi viwanja vinavopimwa je huduma ndio hii hiii? kama ni hii basi tumekwisha! tutafukuzwa kazi! hebu imagine wafanyakazi binafsi wafukuzwe kazi kwa kuchelewa kazini ! SERIKALI ITAPATA WAPI KODI YA KUWALIPA WAFANYAKAZI WAKE HAO WANAOTAKA KUWAHI MAOFISINI ????! kodi ya kuwalipa wabunge???? jamani kuna vitu inabidi viangaliwe !!! na visahihishwe!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 02, 2011

    Mimi ni mkazi wa kigamboni na natumia kivuko hiki kwa muda mrefu sasa. Kwa kweli aliyeleta mada hii amenigusa sana. Mashine zile wakati zinafungwa tulikuwa tunaziona tukafikiri tumepata ufumbuzi wa foleni hapa kigamboni na sasa serikali itakusanya mapato yake kwa uhakika. Kinachoshangaza tangu mashine hizi zifungwe, hazikuwahi kufanya kazi. Utafikiri kwa kuwa hazikuwa kufanya kazi, mkandarasi aliyezifunga hakuripwa. kumbe tunaambiwa alilipwa asilimia zaidi ya tisini. Ukiuliza unaambiwa kama asingelipwa wakubwa wangepata ten pasenti zao wapi? Kwanza ilikuwa walipwe, zikifanya kazi zisipofanya kazi shauri yao!
    wakatihuo tulijaribu kudodosa tukaambiwa hata takukuru walikuwa wanafuatilia tukasema tusubiri tuone matokeo. Lakini uzuri wa nchi yetu kula na wenzio usile peke yako, jambo limezimwa watu waliotufungia kanyaboya wanakula nchi lakini cha ajabu zaidi wanazidi kuula kila kukicha. Mlalahoi mwenzangu, hakuna aliyewajibishwa kwa ufisadi uliofanyika karibu na Ikula zaidi ya watu kuzidi kuula.
    Aliyesema ukishangaa ya mussa utayaona ya firauni mnafikiri alikosea?

    Ukiachana na hilo lingine linalonikela ni hili la watu wazima wenye nyadhifa zao kuvunja sheria za usalama bara barani badala ya kuzilinda. Hakuna asiyejua pale magogoni na kigamboni nimwisho na mwanzo wa bara bara.Njia moja ni no entry. lakini wakati tumejipanga kwenye foleni tena tukiwa tumeshalipa pesa zetu, unaona magari ya serikali, na watumishi wengine waotumia magari yao binafsi wanavyotutimulia vumbi kwa kupita no entry.Sasa tunashindwa kuelewa sisi tunaonunua mafuta ya kivuko hicho tunanyanyaswa na wale wasiolipa bado wakubwa wamekaa kimya. Naapa hii sio halali.

    Mheshimiwa John Pombe Magufuli, tembelea hapa kwetu jioni na asubuhi uone jinsi sheria za nchi zinavyovunjwa na wale wanaotakiwa wazilinde.Tunaambiwa kuna vibali tunataka na sisi tuende tuka chukue kwa sababu hata sisi raia tunaharaka zetu huko tunakoenda kubangaiza.

    Mh Magufuli, foleni nyingine husababishwa na hawa wanaopita no entry pale wanapoziba njia na hivyo kufanya magari yanayotoka kwenye feri yakose njia ya kutokea.

    Kama unavyosimamia sheria za uhifadhi wa bara bara tunaomba usimamie na hii ya usalama bara barani inayokataza kupita no entry. Ikiwezekana trafiki wawekwe wawakamate na wapewe notifikation. Lakini hili linaugumu kwa kuwa wanaovunja sheria ni wakubwa zao.

    Tufike mahali kila mwananchi awe na haki kwenye nchi yake

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 02, 2011

    KWA KIFUPI TU NI KWAMBA NCHI HAINA DIRA WALA UELEKEO. KIBAYA ZAIDI NI KWAMBA VIONGOZI WAMEITELEKEZA NCHI NA WANANCHI WALALAHOI. TAKUKURU YENYEWE INATAKIWA KU TAKUKURIWA MAANA RUSHWA HUMO NDANI IMEZIDI. PIA MUUNDO WA TAKUKURU NI MBOVU KWANI INAKUWA VIGUMU TAKUKURU KUFANYA LOLOTE KWANI WATUHUMIWA WAKUBWA WA UHALIFU NI WALE WALIOWAWEKA TAKUKURU MADARAKANI. UKICHUNGUZA, UTAAMBIWA KUWA HIZO MASHINE ZIMETUMIA MILIONI LABDA HATA 200. MTU KAWEKA PESA MFUKONI AKALETA MASKREPA TOKA INDIA AU CHINA AKIJUA HAKUNA ATAKALOFANYWA NA TAKUKURU. KWAKWELI INATIA KICHEFUCHEFU NA WATANZANIA TUSIPOINUKA NA KUONGEA WALAHI TUTAFANYWA VIBAYA ZAIDI. KILA SEKTA UKIICHUNGUZA NI KICHEFUCHEFU. MDAU HAPO JUU KAULIZA..HIVI HII INCHI HAINA RAISI? WAZIRI MKUU? MAWAZIRI? WATENDAJI?...SA WANATENDA NINI???

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 02, 2011

    Ili kutatua hiyo kero ni kuruhusu sekta binafsi hapo Kigamboni. Kama tatizo la usafiri lilivyotatuliwa Zanzibar. Gharama zitaongezeka lakini usafiri utakuwepo na wa uhakika.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 03, 2011

    Watanzania tumezidi kuwa na uvumilivu bila kiasi na ndiyo maana yote hayo yanatukuta sababu ya uvumilivu wetu na woga uliotujaa!na tunashindwa kushirikiana na tusema sasa tumechoka tuandamane twendeni kwa mkuu wa mkoa au ofisi ya waziri wa miundombinu,Lakini la tumebaki tunanyanyasika na tunafanyiwa wanavyotaka wenyewe sababu ya uwoga wetu!Watanzania tuamke sasa ili tupiganie haki zetu,tusibaki kuendeshwa kama gari bovu!Tuangalie nchi za wenzetu hawaogopi kuandamana kwa kutaka haki zako!Je sisi tutavumilia hadi lini?

    ReplyDelete
  10. Nitabisha sana mtu akisema Tanganyika/Tanzania bara ni masikini,sikubaliani kabisa,inasikitisha kuona viongozi wao ndio wanaonufaika na rasilimali za tanganyika/tanzania bara,hapa ughaibuni sijawahi kuona muakilishi/mbunge baada ya kupita katika uchaguzi serikali ina mpa usafiri au pesa kama Euro 45,000 kwa kunua gari,upumbavu huu hakuna kabisa.

    Jengine Mishahara yao,mshara ya mbunge wa tanganyika/tanzania bara ugawe mara mbili ndio anapewa muwakilishi wa europe,Wanatumia gari zao wenyewe wakilishi,na mafuta juu yao,isipokuwa katika kazi za serikali tu,Hivi bado tunaambiwa masikini tanganyika/tanzania bara ? Mimi sikubaliani kabisa,naamini kama serikali itamuwa na kuwa na democracy kweli,basi mtanganyika/mtanzania bara tafaidika.

    Serikali iano uwezo wa kujenga Tunel ya under ground hapo kigamboni ili kuepuka msongamano wa wananchi wanaovuka,serikali inayo uwezo wa kutoa elimu bure kwa kila mtanzania,serikali inayo uwezo wa kutoa hudumua ya afya bure,Barabara za kisasa,sio hizi tulizonazo kama nyoka,kila siku ndugu zetu wanapoteza maisha kwa accident.

    Hujui wapi inapita roli,wabi gari ya abiria,wapi taxi,wapi baiskeli,wapi pikipiki,alimuradi msongamano tu,jamani watanzania tuamkeni,serikali miaka karibia hamsini imeshindwa kutumalizia matatizo sugu kama haya,viongozi wao wametulia hawana wasi wasi tunategemea nini ?

    Tuacheni mapenzi ya vyama vya siasa tudaini haki zetu,tuekeni wapi madai yetu,kama haya muliweka,ikiwezekana kwa action,sio tunapiga domo tu,serikali kila siku inajivua gamba mpaka lini ? Watendaji wako wapi ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...