Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema kwamba,tunzo mbalimbali zinazotolewa kwa wasanii zinalenga kuthamini mchango wao katika tasnia na kujenga hali ya ushindani miongoni mwao katika kubuni kazi zilizo bora.

Msanii H-Baba akichangia mada. Shoto ni Bw. Lawrence Hinjuson
Hayo yamesemwa na Afisa wa Sanaa wa Baraza hilo,Bw.Lawrance Hinjuson wakati akiliahirisha Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu makao makuu ya BASATA eneo la Ilala Sharif Shamba,Dar es Salaam. Alisema kwamba,tunzo kama zile za muziki zimekuwa zikitolewa miongoni mwa wasanii kwa kuzingatia vigezo mbalimbali vya kitaaluma ambavyo mara kwa mara vimekuwa vikitangazwa na Baraza katika kuhakikisha kweli wale wanaoshinda ndiyo wanaokuwa wanastahili na wenye kazi bora.


“BASATA imebuni tuzo za muziki  kwa lengo la kuthamini mchango wa wasanii na kujenga ushindani miongoni mwao.Tuzo inaweza ikawa cheti au kitu chochote lakini Baraza kwa kushirikiana na mwendeshaji limeona liwe linatoa tuzo hizo maalum inayoambatana na fedha taslimu” alisema Bw.Hinju

Aliongeza kwamba,kulingana na idadi ya maeneo yanayoshindaniwa si rahisi kwa wasanii wote kupata ingawa kuna kila sababu ya wao (wasanii) kujikita katika kutengeneza kazi zenye ubora, zenye maadili ndani yake na zilizo na uhalisia ndani ya jamii ili mchango wao uonekane na kutuzwa.
Awali akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa kuhusu Umuhimu wa Kubuni Vitu vipya kwenye Muziki wa kizazi kipya,Msanii Khamis Ramadhan aka H-Baba alisema kwamba,wasanii wa kizazi kipya wanatakiwa kubadilika na kupendana kwani kumekuwa na tatizo sugu la kuhujumiana na kufitiniana miongoni mwao.
Mkongwe Kassim Mapili akichangia
“Nasema wazi kabisa wasanii hatupendani,tunatakiwa kubadilika ili kuweza kupata mafanikio.Haiwezekani  kufika kokote kwa hali hii” alilalamika H-Baba.

Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa BASATA limekuwa ni eneo huru kwa wasanii, waandishi wa habari na wadau wa sanaa kuelimishana na kupashana habari kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo tasnia hiyo.
Copyright 2007 ©MICHUZI JR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2011

    Asante sana mzee. "TUZO NI KUTHAMINI MCHANGAO WA WASANII"

    Mchango wa wasanii wa kizazi kipya:
    1. Kukaa uchi majukwaani kama alivyfaya Wema na wengine wengi
    2. Wengine kufanya mapenzi hadharani na wengine kutetea kuwa ni uhuru wa mtu.
    3. Kuimba nyimbo ambazo zaidi ya asilimia tisini ni za mapenzi.
    4. Kuwa chanzo cha ugomvi ai kushiriki kupigana kama alivyowahi
    kufanya Dudubaya Vs Mr. Nice na Wema Vs Kanumba
    5. Kuiba nyimbo za wasanii wengine kama alivyofanyiwa Diamond
    6. Kushiriki katika kupiga kampeni za siasa kwa maslahi ya vyama vya siasa hata kama viongozi wake hawafuati maadili ya uongozi n.k.

    Je kwa mchango huo msanii bado anastahili kuitwa ni kioo cha jamii!!!!!!?????????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...