Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akifunga Mkutano wa Kumi wa Bunge na Wabunge wa Afrika Mashariki mjini Arusha jana. Pamoja na mambo mengine Tanzania imeshauri kuwa muungano wa soko la pamoja na sarafu ya pamoja visiharakishwe ili baadaye visijekuwa matatizo kwa baadhi ya nchi washirika.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Africa Mashriki Dkt. Richard Seibera (kushoto) na Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Mutinda Mutitso wakifuatilia kwa makini hotuba hiyo.
Maspika watatu wanawake wa mabunge ya Afrika Mashariki: kutoka kushoto ni Mhe. Rose Mukantbana wa Bunge la Rwanda, Mhe. Anne Makinda wa Tanzania na Mhe. Rebecca Alitwala Kadaga wa Uganda.Picha na Prosper Minja-Bunge


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...