Dear,
Hope you are doing well today?I’m sorry I didn't inform you about my traveling... am presently in Madrid,Spain as I write to you now,Iam writing to ask you to please loan me €2900 today! I had traveled to Spain for official Emergency program which I got myself stranded after I was robbed in a hotel where I lodge and all the money I have was stolen including my phone And other valuable things were taken away from me. However, I spoke to the hotel management to know if they can allow me go out and make calls but they refused due to the fact that I have not paid my bills but they only gave me internet access so that I could contact whom ever that can help me.Now I need €2900 to settle my bills and get a flight ticket back home. I will appreciate any amount you can quickly arrange and send to me now if you are not buoyant enough via Western Union with the details below I will return the money back to you as soon as I get home
Please.

Name: Isaac Mruma
Address: Princesa de Kapurtala 16. 28003 Madrid. Spain
Text Question: What is receiver's date of birth?
Answer: 1955

Please remember to send me full details of the transfer such as MTCN (money transfer control number) or scan copy of the transfer receipt so that i can get the money here without any delay or problem.  I will pay back the money to you including the transfer charges on my arrival. I will check my e-mail again later to have the western union transfer details. Please  use my name and the address above and  make the payment.

Thanks
Mruma

========================
Globu ya Jamii inapenda kutahadharisha wadau wote kwamba upatapo email ya aina hii achana nayo kwani ni Wapopo ambao hadi leo wanadhani ubwege huu wa kuibia watu kijinga haujastukiwa. Aidha, kama ni kweli Mmatumbi atakuwa amekwama popote pale duniani atumie lugha ya Kimatumbi nasi tutamuelewa. Pia ukipata email kama hii muulize kwa kiswahili na kama atakuwa na kwikwi mpe bonge la tusi kisha achana nae.


-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2011

    HAWA WAPOPO WAJINGA SANA ...KATIKA USAWA HUU KUNA MJINGA GANI ATAMTUMIA PESA BWEGE KAMA HUYU, MAANA HATA KUDANGANYA HAJUI UKIISOMA VIZURI YEYE ANASEMA HARUHUSIWI HATA KUTOKA NJE YA HIO HOTEL ALIYO HAPO SPAIN..JE UKIMTUMIA HIZO PESA WESTEN UNION ATAZIFUATA VIPI MSAHAMBA HUYU NA YEYE HARUHUSIWI KUTOKA NJE

    AMA KWELI WAPOPO WAMEISHIWA SANA HATA KUPANGA UONGO UNAWASHINDA SASA HIVI

    ReplyDelete
  2. MATANGALUJuly 09, 2011

    Kwanza hii tabia ya kuwaita "west africans brothers" wapopo ni ujinga na ni ishara ya waafrika kupenda kujichukia.

    Pili, kama wewe umeshtukia utapeli, basi usiibiwe, na huna sababu ya kuamua/kuhisi kwamba huyu tapeli ni mu-west african kwa vile hakuna uthibitisho wa hilo.

    Tatu, hivi hawa ndugu zetu tunaopenda kuwachukia wanawafikia wazungu kwa utapeli? Kwanini wazungu hatuwachukii kwa sababu hizohizo? Kuna mnigeria yoyote mwenye hisa katika EPA, RICHMOND, BAE NA RADA YA CHENGE AU BARICK GOLD?

    Peter Tosh said, "arise blackman arise, arise and know thyself."

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 09, 2011

    "Kama atakuwa na kwikwi mpe bonge la tusi kisha achana nae"..unajua michuzi wewe unaheshimika sana kwenye jamii na ni mtu mzima??so kitendo cha kushabikia matusi kwa mtu mzima kama wewe unataka kuwapa picha gani watoto na watu wenye heshima zao wanaopita humu??ungekuwa karibu yangu ningekunasa vibao akili yako ikae sawa..Baba Rama (Najua utaibana but ujumbe umekufikia!!)

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 09, 2011

    Mambo ya wa-Nigeria hayo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 09, 2011

    ni kweli kabisa kuna watu imewatokea nawafahamu kabisa,tena yule mzee alihamaki kweli,yupo bongo uzuri watoto wake wapo uk walishtukia kama ni kamcheo cha kutaka kutapeliwa wakamuambia mzee wao..tena kingine inaweza kuja kwa jina la mtu unaemfahamu tuwe makini wajameni..m/mungu akuidishie ankali

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 09, 2011

    HAYO YOTE NA NYIE WABONGO MMEZIDI TUMIENI MUDA WENU MWINGI KWA LUGHA YENU YA TAIFA ILI MUONDOKANE NA MAMBO KAMA HAYO NYIE MMEKAZANIA KIMOMBOOO TU MPAKA LINI PENDA TAIFA LAKO NA LUGHA YAKO NI MUHIMU KWA VIZAZI VYENU VYA BAADAE,mdau bwegenaz

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 09, 2011

    Inasikitisha kwa mtu kama huyu kudanganya watu ili aweze kuiba.Asante Michuzi kwa kuwaelimisha watu wasipotoshwe na udanganyifu kama huo,kwani katika mtandao kila mtu ana mbinu zake za kulaghai ili afanikiwe.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 09, 2011

    mdau wa kwanza, ingawa hawa wapopo ni wezi lakini hapa kidogo umekosea na point yako. Mimi sipendi kumumuita mtu mjinga kwani wote tunafanya makosa some how. Anyway Kuzuiliwa kwake (kama tuseme kweli mtu yamemfika haya)hakutosababisha wenye hoteli kutopata pesa zake western union. Kwani akishakabidhi hizo details za kutumiwa pesa kwa management hapo hotelini, wao wanaweza kwenda kuchukua huko western union. Kwani western union humpa yeypte yule anaeleta data zilizo sawia. Umefahamu hapo?

    Kwa hivyo hapo wapopo hawakufanya ujinga kwa walichosema, ila wewe mdau umekosa kufahamu point yao :)

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 09, 2011

    Kuna mtu bado anaibiwa kwa hii Staili?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 09, 2011

    yaani hawa watu wanapenda sana kutumia western union,sijui huko kuna wezi wenzao,maana hapa kuna wakati nilikuwa natafuta nyumba ya kupanga katika web!Eti yeye akasema anayo iko London aliachiwa na wazazi wake walifariki na yeye anakaa katika nyumba nyingine,eti akasema nimtumie pesa ndugu yangu yeyote kwa kutumia western union kisha nimtumie detais katika Email yake aone kweli kama pesa ninayo nisimsumbue kwenda kunionyesha wakati sina pesa ya kupanga,,nilivyopiga simu kizungu chake ni cha kinigeria,,,au ghana lakini alikuwa ni mnigeria ndo wamebobea kwa wizi wa Western Union,,Ukimwambia umtumie Money Gram anakataa anataka mpaka western union,Mimi niliongea na mwenzangu nikasema hawa watu kukamatwa ni njia tu ndogo maana,unaweza ukatumia mtu pesa pale pale kisha akaitoa haraka kabla hujamtumia details huyu mwizi,,,kisha ukisha mtumia unapanga na askali kwenda katika western union hiyo ya mji huwo ulioandika unatoa taarifa katika westen zote,mtu yeyote atakae kuja kuchukua pesa kwa jina hilo pesa atiwe mbaroni,,nahisi hata wakiwa nchi yoyote wanaweza kuiba kwa njia hiyo,,,,hawajafatiliwa tu hao wangenyakwa kirahisi mno,,,Wanalaana wameisha waibia watu wengi sana hapa UK wamejaa kila sehemu ya biashara magari nyumba n.k huyo hayuko spain yuko saa nyingine nchi nyingine,,,,ee mjinga kweli kweli na ukapa huu eti I will return your Money back,,,yaani anahisi sisi wabongo ni washamba kumbe mshamba ni yeye,,,Hujaongea kiswahili mbongo hajakufeel wewe!!!!!Acha ujinga kwetu TTTZZZZDDD!! Kaibie wengine,,,,Mruma!why you bother with Swahili blog(Bongoland blog)Ahlam UK!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 09, 2011

    we ahlam uk unaingia na kushinda humu halafu unapoonda swahili blog. nyooo. usikute demu wewe

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 09, 2011

    Kwa mdau ULOMKOSOWA MDAU WA KWANZA, wewe sijui unazungumza maneno hayo ukiwa wapi katika dunia hii, pengine inawezekana kwa BONGO au huko uliko wewe, ila mimi nazungumzia hapa nilipo ULAYA hii sidhani kama ipo sehemu western union watatowa pesa ya mtu kama mwenyewe hajaenda pale na kitambulisho chake tena valid,

    sasa wewe unasema hao wapopo wawape data na kitambulisho kwa management ya hotel wakamchukulie pesa zake huku tuliko sisi hicho kitu hakuna

    ndio nikasema rabda hio inafanyika kwa BONGO na sina ukakika sasa tufafanulie wewe uko wapi unakoweza kumtuma tu akakuchukulie pesa zako western union,

    kwani hapa ulaya usifananishe na kwengine na hao wapopo wanasema wako spain, na kitendo cha kuchukuliana pesa hapa sijakisikia kienyeji hivyo naomba ufafanuzi wako na mimi nitume watu wakanichukulie pesa zangu western union kwani mara nyengine huwa na kazi nyingi

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 09, 2011

    Muongeaji mmoja hapo juu amezungumzia suala la kumtuma mtu akakuchulie mapesa yako western union, wewe ulonamawazo hayo uko wapi tanzania ndio unaweza kumtuma mtu au....


    kwani kama ni TANZANIA siwezi kukukatalia ila kama tunaongelea ulaya hilo suala halipo kwahio unapotowa maoni tafadhali tueleweshe kuwa western union, mbeya au iringa au kilwa, unaweza kumtuma mtu akakuchukulie mapesa yako western union, ila huku kwa watu jeuri hio hakuna na sahau kama hujaenda wewe mwenyewe ukaonesha kitambulisho chako halali na picha yako hayo mapesa hupewi

    na kama huamini kama uko ulaya basi jaribu ukiwa hapa UK, au nenda holland utumiwe mapesa umtume mtu akakuchukulie mapesa western union, usiongee vitu ikiwa hujawahi kusafiri kwenda nje ya nchi ukaona watu wanavyohudumia watu, na usiwe na fikra za ki bongo kuwa wewe tajiri mtume mtu akakuchukulie mapesa yako

    nilikuwa na hamu sana kutaka kujuwa wapi unaishi wewe na mawazo hayo finyu kwani inaonesha hujatoka nje ta tanzania umeshazoea kwenda ofisini kwa watu ukatoa HABARI ZENU, na watu wote munajuwana unapewa mapesa yako hata kitambulisha hawakiangalii kama kiko valid au laa
    ila napenda kukuelimisha kuwa hapa uk, germany, holland, hivyo vitu hakuna kwani nchi zote hizo mimi nishakaa na nishatumiwa pesa na bila kwenda mimi mwenyewe pesa hawanipi na nikifanya ukaidi ningeitiwa polisi na usisubutu kutumwa wewe ukamchukulie mtu pesa kwani ukimkuta mstaarabu atakwambia mwambie mwenye kitambulisho aje achukuwe pesa zake

    laa umekutana na mwengine anakuitia polisi ukawaeleze zaidi kituoni sasa inategemea uko ok kimakaratasi ya kuishi watakuachia laa kushaoza ndio safari ya kinondoni siku ya pili

    kwahio mdau hio mada yako kuwa western union wanatowa pesa ya mtu ukiwapa kitambulisho tu na mwenyewe yuko nyumbani kalala, HUO ni uongo na kama kinafanyika ni huko BONGO sio SPAIN

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 09, 2011

    Wabongo tumezidi vijisenti hivyo ndio makelele lukuki. Basi mimi kesho nitamtumia huto tuela hata kama asiponilipa basi mungu atanilipa.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 09, 2011

    Kuna mtu nimeona humu mtandaoni anawatetea hawa wa nijeria,namuomba asiwatetee kabisa watu hawa hatari,Linalo zungumziwa humu ni kweli kabisa,watu hawa ni hatari na ni matapeli wa kutisha,Tamaa ya utajiri mkubwa kwa haraka ndiyo maisha yao,na kwao Nigeria mtu kukamatwa au kufungwa ni sifa.Mimi kama mtanzania niliyeishi Japani kwa karibu miaka
    20 sasa,ninawajua vizuri nduli hawa maana nimeshaishi nao na kufanya nao kazi pamoja kwa muda mrefu.Huu mtindo wa kutaka pesa katika mitandao hasa hasa ni wao tu,Wanijeria hawa ndiyo walio sababisha Western Union kufungwa hapa Japan,pia wanatusababishia matatizo mengi sisi weusi kila tunapotaka huduma mbali mbali maana kila pahali wameharibu,hii yote ni tamaa yao,kwa hiyo namshangaa mdau anaye watetea watu hawa nina uhakika hawajui vizuri,nadhani hata ukimuuliza mtu yeyote aliyewahi kuishi Japan atakubaliana nami,na idadi kubwa wa foreighners waliopo katika jela zote za Japan ni hawa wapopo.Pia wanaongoza kwa idadi kubwa ya watu weusi Japan.
    mdau Tokyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...