habari gani mwanajamii unayefanya kazi nzito ya kijamii.
aslan mkuu mi napenda uiweke hii habari yangu kwenye blog yako kidogo watu wapate kutafakari na kuelimika kidogo.
mi ni mfanya kazi wa umma na ninafanya kazi katika ofice za umma lakin kuna tabia moja inanikera sana. tukizingatia sisi tunaishi katika nchi ya kisecular basi lazima tuheshimiane katika tofauti zetu ndio tuweze kusonga mbele.
kwa nini nasema hivi inaweza tokea mpo ofice moja watu wawili dini tofauti lakin unakuta mtu mmoja anafungulia kwaya kwenye computer yake ambayo ni ya umma lakin anatumia yeye. hivi na upande wa pili na yeye akiamua kufungulia quran au kwaswida kazi zitafanyika kweli.
lakin kwa nini ukasikilizie kwaya oficine? wakati mwingine ukienda nyumbani kwake hata siku moja huwezi kusikia kwaya? kwanini basi usiwe mstaarabu. mi nasema haya kwa ushahidi kabisa na hapa kwetu udom hii tabia imekidhiri na inakera sana.
asante
Pole sana ndugu yangu. Mimi ni Mkristo lakini sifurahishwi na mtu asiyeheshimu imani ya mtu mwingine. Tabia hiyo inanikera hata mimi. Hata mimi sifurahii kaswida na adhana hivyo nisingefurahi mtu wa dini hiyo kuweka sauti kama hizo kwenye ofisi tunayoshea. Lakini nakuomba umweleze aache na ikishindikana mpeleke kwa ngazi husika. Huku kwenye blog hakutakusaidia kitu zaidi ya kuchochea wengine nao wachukie hali kama hiyto wakati wapo hata waislamu wanaosikiliza nyimbo za injili.
ReplyDeleteKatika uislam tunaita "UNAFIKI". MNAFIKI ni mtu ambaye ana tabia mbali mbali ikiwemo kuwa muongo, kutotekeleza anachoahidi, kuwa kigeougeo kwa maana leo akiwa na waislamu anakuwa msalihina akiwa na wakiristo anakuwa mkiristo. MNAFIKI mbele ya watu anakuwa na tabia ya ukarimu lakini wakiwa wale watu hawapo anakuwa na tabia ya uroho na uchoyo. Hao wafanyakazi wenzio wanawenzio wanaitwa WANAFIKI lengo lao kubwa waonekane watu wa dini ili wapate vyeo au vinafasi vya masomo kwa kupitia mgongo wa dini!!!
ReplyDeletenadhani hiyo sio hoja unaweza kusikiliza lakini kwa utulivu yaani bila kelele lakini swala lakusema eti na mtu wa kuran naye apige kwani anakatazwa!!??huo nikutaka kuweka swala la udini maana nilitegemea kuwa ungesema hairuhusiwi kusikiliza nyimbo za dini hapo sawa.
ReplyDeleteWakati wa sasa si wa malumbano wala kugombana. Ni wakati wa ukweli na uwazi na maelewano kwa faida ya nchi yetu. Mimi nakushauri mweleze ukweli tu, bila jazba, kwamba ofisi inawatu wa dini mbali mbali hivyo kama anataka kusikiliza anunue headphones/earphones asikilize mwenyewe. Na huu ndio ustaarabu wa kuishi na watu wa tabia na mienendo mbalimbali.
ReplyDeleteUkiwa unahofia kwamba jamaa atakuelewa vibaya (kwa sababu katika dunia ya leo kumekuwa na kasumba mtu akitaka kutetea haki yake ya kidini anachukuliwa tofauti na kuitwa majina yasiyotoa melekeo mzuri kwa jamii) mwambie kukiwa na mziki unalia hauwezi kuconcentrate na kazi zako hivyo muombe kistaarabu atumie headphones/earphones. Natumaini kwamba atakuelewa na atatekeleza.
- Mdau Ulaya
Hapa umeongea jambo la maana sana, hii tabia ipo maofisi mengi sana ya UMMA, mimi mwenyewe nimekuwa nikipata tabu hiyo na inapobidi tumekuwa tukiwaleleza wahusika lakini baadhi yao hawaelewi. Hili jambo nadhai linahitaji kutizwa kwa kina kabisa vyengevyo maofisi uya umma yatakuwa hayana tofauti na viwanja vya biafra au pale jangwai watu wanapotangza neno. Hata kuweka miti ya X-Mas ayo inakera maana taasisi i kwa ajili ya umma wote na wala sio dii fulani tu, mbona siku za iddi au sherehe za watu wa dini nyengine hutuweki hayo mapambo?
ReplyDeleteOhhhh! Hoja ya nguvu sanaaaa, nakuunga mkono maana kila mtu akifungulia cha kwake wengine wanapenda juwata, kasheba, sembuse kwaya na kaswida. Huu siyo ustaarabu. Mtu asilazimishie starehe yake mwingine aipende na bado kazini kunageuka sokoni. Mwenye kutakahayo anunue hedifoni aweke masikioni. Kama ni mlokole vitendo ndiyo vitaonyesha kuwa yeye ni mlokole kama ni swala tano ni mwenyezi Mungu ndo mtoa hukumu siyo kujionyesha kwa wengine. Huu ni mchango mkubwa kwenye kupanda ngazi kimaendeleo na ninahisi kuna watakao pinga hoja yako hapa ukumbini. Degelavita.
ReplyDeletePole sana hukutakiwa hata kusema kama uko UDOM manake nadhani kutakuwa na wafanyakazi wengi maofisini wana pata adha kama ya kwako..Siyo lazima nyimbo nyimbo za dini..mimi nasemna muziki wowote ule-Ni bora kama unachangia ofisi au hata uko peke yako ukanunua "HEADPHONE" ukaendelea kusikiliza muziki wakati unafanya kazi!!Hata majumbani mtu anafungulia muziki 'mkuuubwa' na kusumbua majirani.'Noise polution' hiyo inaitwa.
ReplyDeleteDavid V
Wadau wenzangu wote hapo juu; Naona sentensi ndefu ndefu na maandiko ya kila aina lakini sijaona point hata moja: Point yangu kwa mdau mwenye hoja hii(aliyenung'unika) ni kuwa: Kwanza kabisa umesema upo ofisi ya Umma na siyo binafsi, na hata kama ni ofisi ya binafsi: Inabidi umweleze mkuu wa ofisi yako kuwa huyo (au yeyote) anayesikiliza nyimbo ziwe za dini yeyote au bendi yeyote kuwa ANAVUNJA Policy ya kampuni kwani hapo yupo kazini na anatakiwa ashughulike na shughuli za kikazi na siyo binafsi.Hivyo kwanza angetakiwa achukuliwe sheria za kikazi (Disciplinary Action). Pili, kama mkuu wako (unaye ripoti kwake) hatofanya lolote kukusaidia hilo; Basi fikisha katika ngazi ya juu yake: Tatizo litakuwa tu kama Ofisi yako ya UMMA haina Policy za namna hiyo, yaani kuzuia matumumizi ya vifaa (na muda) vya ofisi kwa matumizi binafsi; basi u-campaign ili Policies ziwekwe au unitafute kwa kujibu maoni yangu ili tuwasiliane niweze kushughulikia suala hilo kama ni culture inayowakera wengi kwani pia ni moja ya mambo yanayorudisha uchumi wetu nyuma. Wakati wa kazi ni kazi, na kama kuna anetaka kusikiliza mambo nje ya kazi basi muda wake wa mapumziko (Lunch break) aende Internet Cafe au anunue Ipod asikilize nje na maeneo ya kazi.
ReplyDeleteNadhani unaweza kupitisha hoja kwa wakuu huko CENTRAL BANK na ikatungiwa kautaratibu kwani nakuunga mkono kwamba si sawa.Sio tu kupiga mziki lakini mziki wowote haitakiwi kama huna simukichwa
ReplyDeleteBosi wangu anapiga bolingo kwa fujo ofisini, nilalamike kwa nani?? Wakati naanza kazi aliniuliza "mimi napenda sana kusikiliza muziki wakati nafanya kazi, utamaindi?" Of course nikiwa kama mtafutaji na opportunity ndio ilikuwa mbele yangu, ikabidi nijibu "hapana mkuu, simaindi", na kumbe yeye zake ni bolingo na mchiriku tu. Ila kwa kweli huwa nasubiri wikiendi kwa hamu sana nipumzishe masikio na kichwa changu, hata TV siipendi tena, bora angekuwa anapiga R&B, ila bolingo na mchiriku, bajeti haiandikiki kirahisi kwa kweli!!!!
ReplyDeleteMdau swala lako la leo ni bomba!Jamani Imani huwa iko katika roho yako na matendo yako mema tu ndo Mungu anakuandikia si kukera wenziwe kwa kwaya au Qaswidah au kuwasikilizishia wakristo Qur'an!Hiyo ni ya kutoitendea haki Dini yako kwani kama ingekuwa hivyo basi Imam angeenda kutoa Hutbah juma pili kanisani au padri angeingia Msikitini Ijumaa kutoa neno la Bwana,,,Mimi ni mwislam lakini nachukia mtu anaelazimisha watu wasokuwa wa dini yake kufata matakwa ya Dini yake!Kuna baadhi ya mambo unaweza ukatangaza kuwa niya Haramu kwa kuwa katika dini zote yanakatazwa kama ulevi maeneo ya kazi,usherati wa wazi wazi,wizi dhurma,usengenyaji,uchonganishi,na mengi ambayo ni kweli Dini zote mbili katika Uislam na Ukristo yanakatazwa!lakini kufungulia kwaya au Qur'an kwa fujo maeneo ya kazi ya watu mchanganyiko,huwo ni ukosefu wa akili na nina imani hao si wacha Mungu ni vujo tu!kwani muda wa kusikiliza maneno ya Mwenyezi Mungu unao sana ukirudi nyumbani au kweli vaa headphones uburudike wewe mwenyewe!Mifano tunayo ya Yesu kristo na Nabii Muhammad(S.A.W)hakuna uliyesikia ana kasheshe ya munkali huwo!Achani kuwasumbua watu!Kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe!Kafungulie hizo nyimbo nyumbani kwako kama mwenye nyumba hatakutimlia mbali kwa kuwakera wapangaji wenziwe!Au kama ni nyumba yako basi majirani watakulipoti kwa M/Kiti wa nyumba 10,,10!Ahlam UK
ReplyDeleteDawa ni headphone tu hata kama unasikiliza ndomboro unajuaje kama jirani yako anapendaaaa???? Tena kama ni nyimbo za dini ndio unakuta hata customer hakikosa huduma bora anasingizia ofisi ile ina ubaguzi wa dini kumbe ni hizo nyimbo mnazopiga kama vile ofisi ni kanisa. Anyway hamkatazwi kusikiliza mziki ila kuweni wastaarabu tumieni headphones. Mimi ni mkristu na sifagilii hiyo tabia na ni kweli ipo hata hapa ninapofanya kazi
ReplyDeletehili si suala la ofisini tu. ustaarabu unahitajika popote.utaona mtu kaweka mziki mpaka nyumba ya 5 watu wanasikia,au anaendesha gari mpaka kila mtu ajue kama spika zinatoa au jamaa labda masikio yake yana matatizo
ReplyDeleteKazi kwelikweli, hawa ndiyo wanaoshinda jamii forums kuutukana utendaji kazi wa viongozi wa serikali iliyopo madaraki. Unasikiliza kwaya kazini?
ReplyDeletepole sana, hii kweli ni kero. wakati mwingine unakuta mtu anaanza kuleta maada za kidini kazini. hii haipendezi jamani, tuchape kazi kwa maendeleo ya taifa hili na vizazi vyake vijavyo. dini kila mtu ajue moyoni mwake lakini pia kuna muda na sehemu zake sio ofisini ama sehemu za kazi...
ReplyDeleteMIMI PIA NAOMBA MSAADA WENU WADAU WA BLOG HII, MAANA NINA TATIZO NATAKA NILIPOST HUMU NISAIDIE MSAADA KWENYE TUTA LAKINI SIJUI NAWEZA KULIPOST VIPI HUMU KWENYE BLOG HII. TATIZO LENYEWE NI LA KISHERIA, HIVYO NAHITAJI MSAADA WA KISHERIA, EMAIL YANGU NI loptz@yahoo.co.uk AU +255 777 968 813...ASANTENI SANA
Ukweli ni kwamba wakristo ndio waanzilishi wa migogoro mingi km si yote yakidini Bongo.Mimi nilisoma Ilboru from O level to A level ukweli ni kwamba walimu asilimia 90 ilikua ni walokole na mm sisi waislam ilikua km vile twasoma seminary yani ofisini ni kwaya kwakwenda mbele.Kuna baadhi ya walimu walifikia hadi kutaka tuombe kikristo kabla yakuanza kufundisha jambo ambalo waislam tuliligomea ni tukaonekana Mujahidina.Huu ni ukweli ambao kila muislam aliesoma Ilboru Sec. anaujua.Yani wagalatia wanaona serikali na maliza za umma ni zao.Lkn ipo siku watakuja kujutia matendo yao.
ReplyDeleteNdugu yangu naona bado hauko makini na imani yako.Ktk usilam tunafundishwa kuzuia munkar aidha kwa mkono,kwa ulimi au kwa moyo.Mi nadhan dawa ya hawa jamaa ni kwenda nao pua kwa pua tu,simaanishi na ww ufungulie Quran bali mwambie bila kumuogopa hata kama ni mkuu wako wakazi.Hio ni ofisi ya Umma.Kua na imani thabit na hakuna kisichowezekana.
ReplyDeleteWHOEVER WISHES TO BE THE STRONGEST AMONG MEN,LET HIM PUT HIS COMPLETE TRUST IN ALLA(S.W)
Wote mliochangia hamjaangalia upande wa pili wakristo wakiweka nyimbo za injili shida, je na wale waislamu wanaotembea na mikeka na kufanya vyumba vya ofisi kuwa vyumba vya sala mtasemeje mbona sisi hatujawahi kulalamika na wapo kila mahali, vyuoni, shuleni, ofisini tena za serikali ndo usisema. Unaenda kwenye ofisi fulani unakuta mtu anayehusika amefunga chumba anasali na inabidi usubiri hao je mbona hamsemi? Hata few weeks tuliona kwenye blog hii hii ofisi inatangazo la vua viatu. Kweli kila mtu angeheshimu muda wa kazi kwa customers na asiyecustomers kazi Tz ingekuwa shwari. Unapewa njoo kesho, keshokutwa, mwezi, miaka kwa huu huu uvivu, kusikiliza kwaya si kuonyesha ukristo, kubeba mikeka kila mahali si uislamu vyote vinaweza kuwa unafiki. Vile hata ukiwa kazini ukajifungia na kuomba na baada ya sala ukapokea rrushwa hiyo ni dhambi na jehanamu inakuhusu. ukisikiliza kwaya 24hrs na huku huendi kanisani na humjali mwenzako pepo inakuhusu kwa sana. Huu wooooooote wa mikeka na nyimbo za kwaya maofisini ni Uvivuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu tu ambao umekidhiri na unaleta umasikini kwa nchi na kutupotezea muda kufuatilia mambo yetu ofisini hasa za serikali miaka na HAWA niliowataja hawajali maana wanalipwa kwa mwezi na sii kwa masaa kama huku ughaibuni hata simu kazini haturuhusiwi. Mnaweza kufanya kimoyo moyo huku mnafanya kazi.
ReplyDeleteWakristo ni wachokozi kwa kusiliza kwaya? Mi siogopi asikilize kwaya au asome quran poa tu ilimradi mtu afanye kazi.Na kama una mind business zako mtu hajakusemesha we unamind nini uvivu tu unakusumbueni,
ReplyDeleteKwa wenzenu huku hata simu haturuhusiwi na radio ukitaka kusikiliza unalipia, so wewe ukiwa unafanyakazi kwa moyo wako hata hutajali mtu wa pembeni licha kusikia anachoongea
Katika ofisi moja idara ya Computer ilikuwa na watu watatu, bosi wa Idara hiyo alikua mlokole na ofisi yake, na wasaidizi wake walikuwa vijana wa Kiislamu na ofisi yao na tena watu wa Ibada hasa.Ukienda ofisi ya bosi wao unakuta kwaya masaa yote ya kazi, na ukienda ofisi ya wale vijana hakuna hata wakati wa swala uliokuwa ukivunjwa! Cha ajabu katika ofisi nzima idara hiyo ndio iliyokuwa bora kuliko idara zote za shirika! Safari za kikazi bosi wao alizipanga kwa zamu, siku ya Ijumaa vijana hao wanapokwenda msikitini bosi wao alikuwa tayari kufanya kazi zao! Bosi aliposafiri idara haikuyumba! Hiyo idara ya walokole na wajahidina ndio ilikuwa na ufanisi mkuu! Sijui siri yake.....lakini walijifunza kuchukuliana kuheshimiana na waliitumia imani zao kutuonyesha wengine tusiokuwa na dini kuwa Dini ni matendo zaidi kuliko maneno!Ukiona mwenzio hafurahii Kwaya acha kupiga muziki wa dini! Ukija na wewe na Kaswida haitakuwa dawa! Muziki wa dini au Kaswida hauwezi kumbadili mwenzio Imani!
ReplyDeleteMie nakerwa na wanaonihudumia wamevaa kininja! haswa maofisi ya umma yasiyo na dini! sijui utanisaidiaje? Pia nikirudi home nakerwa na mihadhara na azana zinanipigia kelele kweli sijui utanisaidiaje Nathani katika zama hizi za teknologia simu zinaweza tumika kuita waumini na si ma-speaker yanayoamsha watu usiku! Michuzi be fair to post this
ReplyDeleteDuh, wengine wanaongelea dini, wengine musiki. Sasa hoja ni dini au music ndo shida? Mimi nilivyoelewa, Mtoa hoja anakerwa na Music wa dini, ila bolingo, chiriku, R&B, msondo, pekecha, kiduku vyote kwake ni sawa isipokuwa music wa dini!!....duh, hapo hakuna msaada, tafuta ofisi wanayopiga Kaswida tu ndugu yangu!
ReplyDeleteKama Mungu wetu aishivyo hatuna haja ya kulumbana kabisa wala kupandishana hasira,sheria si zimewekwa ili zifuatwe?kuna haja gani ya kukejeliana na kusemeana lugha za kuumizana?ukweli wa dini ipi ni sahihi na inayompedeza ALLAH yeye mwenyewe aliye juu anajua,
ReplyDeleteMUHIMU ni kuepuka kuumizana bila sababu na fuata taratibu zote kumueleza huyo bwana juu ya tabia hiyo na ikishindikana uongozi ufahamishwe ili ashughulikiwe,utemi na umaarufu huo akaufanyie nje ya ofisi ambapo hakuna sheria za kumbana,lakini kwa kazini hakuna nafasi kwani hapo watu wanakuwakikazi zaidi,sasa hapo tukiambiwa watanzania wavivu tutakataa kweli wakati hali inajionyesha kabisa mziki kazini ndg zangu? hiyo imekaa vibaya haijatulia.
hakuna haja ya ugomvi au kulipiza kwa kasda. Mwambie aache maana watu wengine hawafanyi makusudi bali wananogewa na dini zao. Mshauri atumie headphone na kama una uwezo mnunulie - "plse use this" Mambo ya kwenda kwa bosi hayana maana bali yanaweza kuharibu zaidi kama bosinaye kaegemea upande fulani.
ReplyDeleteMimi nilipata situation kama hiyo. Nilimwambia mwenzangu aache - akaendelea kwa siku kamatatu halafu akaacha. Nilimwambia tu "unajua tuko watu wa imani tofauti hapa ofisini? naomba uache kupiga miziki yako ya kidini tafadhali" Alivyoendelea nilinyamaza kimya nikaendelea na kazi zangu.Nadhani baadae alijiona mjinga au aliona aibu.
Mtoa hoja ana Mapepo yanaogopa kwaya! hahahahahahah
ReplyDeleteukumbi ni wenu waislamu na mnavyojua kuongea midomo mirefuuuu. tutaendelea kupiga kwaya mpaka mpasuke.
ReplyDeleteukumbi ni wenu waislamu na mnavyojua kuongea midomo mirefuuuu. tutaendelea kupiga kwaya mpaka mpasuke.
ReplyDeleteKWANI WAISLAM NAO WANASHINDWA NINI KUAMSHANA KWA ALARM ZA SIMU BADALA YA KUPIGA ADHANI SAA 11 ASUBUHI?
ReplyDeleteMBONA HATA WASIOKUWA WAISLAM WANAKEREKA HIZO KELELE? ALARM ZA SIMU NI KIMYAKIMYA KILA MTU NA KWAKE, ADHANA KUNA WENGINE HATA KUISIKIA HAWAISIKII.
TUBADILIKE TUACHE KERO MTAANI
Wadau asante kwa mawazo mazuri ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi ila kuna baadhi ya wachangiaji wamejaribu sana kuchafua hali ya hewa humu ndani,nilivyomwelewa mtoa maada kinachomchukiza ni nyimbo za kwaya.
ReplyDeleteMbona sisi wakristo tulishazoea kuswalishwa swala tano lakini tumekaa kimya(SWALAAAA SWALAAA SWALAAAAA) tena kwa vipaza sauti hatulalamiki,huko si kuhubiriwa dini bila kupenda? Asubuhi tunaamshwa kwenda KUSWALI japokuwa sisi si waisilamu tumekaa kimya tu.
USHAURI WA BURE:
Kwani ukisikiliza kwaya au kaswida unahofia kuikana IMANI yako? Cha msingi muziki unaosikiliza usiwe wa matusi tu au usikupunguzie ufanisi wako kazini.
HOJA YA MSINGI:
Makelele sehemu yoyote ile hayatakiwi.
Fanya kazi kwa bidii uliokoe taifa lako.
kuna watu wameanza kuleta utani,mmoja anasema waislam waamshane kwa alamu za simu muda wa sala, nataka nimwambie hivi, UISLAM NI TOFAUTI SANA NA UKIRSTO..TARATIBU ZA KIISLAM HAZIBADILISHWI KWA MATAKWA YA WATU KAMA WANAVYOFANYA WAKIRSTO..UISLAM NI UTARATIBU MAALUM WA MAISHA YA KILA SIKU YA MWANADAMU AMBAO UMETOKA KWA MUNGU. SASA HUWEZI KUUBADILISHA KAMA AMBAVYO WAKIRSTO WANAVYOBADILISHA HATA HIYO BIBLIA..KWA HIYO ZINGATIA NA TAFAKARI HILO MCHANGIAJI ALIYETOA WAZO LA KUAMSHANA KWA ALAMU...tunachokijadili hapa ni kero za kidini hususan ktk ofisi za umma...kama ni ofis ya mtu binafsi inawezakuwa hiari yake..wewe uliyeona tangazo la vua viatu, ilikuwa ofisi ya umma?, si rahisi na pia lengo la kuvua viatu lilikuwa ni kwa sababu gani..TOA MAWAZO YANAYOISHI ILI YAISHI HATA UKIFA ACHANA NA MAWAZO YALIKUFA ILIHALI UNAYEYATOA BADO UKO HAI...ASANTENI
ReplyDelete