Mheshimiwa Godbless Lema Mbunge
Jimbo la Arusha Mjini -Chadema
Mheshimiwa Spika, kwa maslahi ya umma wa Watanzania, napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwepo hapa leo, kuwasilisha Maoni na Mapendekezo ya Kambi rasmi ya Upinzani, kuhusu Wizara ya Mambo ya Ndani, kwa mujibu wa kanuni ya 99(7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la mwaka 2007.
Mheshimiwa Spika, natoa pia shukurani zangu za dhati kwa familia yangu, Mke wangu Neema Lema, watoto wangu, Allbless Lema na Brilliant Lema, na wazazi wangu wote, Mzee Elibariki Jonathan Lema na Mama .
Mheshimiwa Spika, napenda pia kutoa shukrani zangu za dhati kwa wapiga kura wangu wa Jimbo la Arusha Mjini kwa imani yao kwangu. Licha ya vitisho, vipigo na mabomu ya machozi yaliyotawala kampeni na hata siku ya kupiga, kuhesabu kura na kutangaza matokeo, wananchi wa Arusha waliendeleza msimamo wao wa kutetea haki kwa kulinda kura zao kwa ujasiri wa hali ya juu. Kwa ujasiri wao, kwa uvumilivu wao, na kwa kujitolea kwao, wananchi hawa wameendelea kutukumbusha kuwa: “Ni heri ya vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu.”
Mheshimiwa Spika, ninapenda pia kumshukuru Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe, Naibu wake Mhe. Kabwe Zuberi Zitto, na Mnadhimu Mkuu Mhe. Tundu Antiphas Mughwai Lissu, kwa kutambua uwezo wangu na kunipa dhamana ya kuwa Waziri Kivuli wa Wizara hii nyeti ya Mambo ya Ndani
.Mheshimiwa Spika, nawashukuru wanachama, viongozi wa ngazi mbali mbali na wapenzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) popote pale walipo ndani na nje ya Tanzania kwa kutuunga mkono wakati wote wa harakati za kudai haki katika siku ngumu na za hatari zilizofuatia uchaguzi batili wa Meya wa Jiji la Arusha. Msimamo wao umeendelea kututia nguvu na ujasiri hata katika kipindi hiki ambacho kuna dalili za baadhi yetu kutetereka katika mapambano yetu ya kudai haki.
Mheshimiwa Spika, Mwanafalsafa maarufu wa Kiyahudi Elie Wiesel alisema, “there may be times when we are powerless to prevent injustice, but there must never be a time when we fail to protest.” Kwa Kiswahili, “kuna nyakati tunaweza kuwa wadhaifu katika kuzuia uovu na dhuluma, lakini kamwe isijetokea wakati ambapo tutashindwa kupinga uovu na dhuluma.” Pengine tulikuwa dhaifu kudhibiti hujuma na dhuluma tulizofanyiwa kwenye uchaguzi mkuu uliopita, lakini kamwe hatutakuwa tayari kuhujumiwa katika uchaguzi wowote ujao, ukiwemo wa Jimbo la Igunga.
Kupata hotuba kamili BOFYA HAPA
Nice speech, ifanyiwe kazi.
ReplyDeleteNaunga mkono hoja!!
ReplyDeleteyaani huyu hapa kweli hapa amekoroga. yaani ametumia hiyo nafasi badala ya kutia changamoto ya bajeti, yeye anaongelea mambo ya chama chake na injustice?
ReplyDeleteujue kuwa kiongozi unahitaji training, watu wengi wa upinzani they just spring up kwenye uheshimiwa kwahiyo ile dhana ya kukua ili kuwa kiongozi haipo. Kama waziri kivuli inabidi alete changamoto kwenye wizara ili ifanye kazi kwa ufanisi sio kulia faulo kwa kukiwa na nafasi.
- - -
buffalo,
new york
Big up Lema, kweli ulistahili hilo jina la Godbless.
ReplyDeleteNi hotuba iliyoenda shule hakuna kumumung'ya maneno umehit palepale kwenye hali halisi iliyopo mtaani na huo ndo ukweli halisi katika jamii tunayoishi sasa.Nimeipitia hotuba yote sijaona pahali ambapo watu wengi wamesema anachochea amani.
Na ikumbukwe kazi ya mbunge sio kuisifia serikali, si tumeona ya Wizara ya madini kilichotokea mpaka bajeti yao ikapigwa chini?
Tunahitaji viongozi wenye kuweka maslah ya taifa mbele,bila kujali tofauti ya chama wala dini.
Ankal usibanie haya maoni, la si hivyo kulikuwa hakuna haja ya wewe kupost hii hotuba hapa jamvini.
Mungu ibariki Afrika,mungu ibariki Tanzania.
Hakuna jipya....
ReplyDeleteWanaoguswa hawakubaliani na hotuba hii. Njii hii ama kweli cha moto tutakiona.
ReplyDeletesasa watanzania wanaelewa matatizo yakuwachagua wabunge vijana,
ReplyDeletejamani wabunge mliochaguliwa tumewatuma kutuwakilisha na siyo kivingine tafadhali sana acheni ubabe na upumbavu.
yan huyu nae anaboa mpaka basi!!watu tunataka mabadiliko lakini yeye analeta vurugu...binafsi simfagilii kabisa,hanijui simjui..sipo kwenye meli yake kabisa
ReplyDelete...ukweli una upande nyingi tu na tofauti.alichokisema Lema ni ukweli ambao upo wazi kwa watanzania wote.Matatizo aliyoyasema yanathibitika.Mfano.mauaji yamefanyika na mnajua.mahakama zetu zimewatia hukumuni askari wetu kwa mauaji yasiyo na tija.Labda la kujiuliza ni kwamba swala hili ni pana kiasi gani.Lakini huwezi kupinga kuwa hayo aliyoyasema hayapo.Kila kitu alichosema Lema kinauthibitisho mzuri tu.
ReplyDeleteUjumbe umefika ni kwenu kukubali kujirekebiisha lakini sio kukataa kwamba hayapo.kama unapinga hayo basi hukumu za mahakama za tanzania ni bure,au tume zilizoundwa nakutoa ukweli huo ni bure.Kama tunaamini hayo aliyoyasema hata kwa lugha yoyoye ile yapo kubwa ni kujirekebisha tusonge mbele.
Kukuiri ukweli si udhaifu ,bali ni ushindi wapendwa.
maoni ya kwangu.
Sijaona ubaya wa hotuba ya Lema japo Ndugai alimtoa nje. Ukweli unauma lakini.
ReplyDeletehawa ni waisrael wao ubabe tu. Sio watu wa kuwapa nchi labda tumwache mpake afike umri wa Mtei.
ReplyDeleteWasioguswa ni nyie wabeba mabox au watoto wa vibopa hamjui jinsi gani Ujambazi umekidhiri hakusema tuu ni haoa Polisi wamo pia kiukweli jela wamejaa wauza nguo machinga na wasio na hati ....MTASONYAJEEEEEE nimeguswaaaaaa...Naunga Hoja
ReplyDeleteHakuna tofauti kati ya Myahudi na mchagga, na huyu jamaa ni myahudi. Akishida, tutakoma.
ReplyDeletehamna kitu upinzani..ccm bado ni chama bora wanahitaji marekebisho tu..,chadema hamuwezi kumiliki taifa hili..,
ReplyDelete