Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimtwika ndoo ya maji bi.Zainab Yusuf Lidandi wakati Rais alipokagua na kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Nyundo wilaya ya Mtwara vijijini jana jioni.Rais Kikwete yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi kukaguana kuzindua shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mtafiti wa zao la Korosho katika kituo cha utafiti wa Mazao na mafunzo cha Naliendele Mtwara, Dr.Peter Masawe akimpa maelezo Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais kikwete alipokitembelea kituo hicho jana mchana kukagua maendeleo ya tafiti za mazao mbalimbali.Baadaye Rais kikwete alikutana na uongozi wa kituo hicho na kujadili namna ya kuboresha shughuli za kituo hicho muhimu.
Mtafiti wa Muhogo na jamii ya viazi Dr.Geofrey Mkamilo(kulia) akimwonesha Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muhogo ulozalishwa kwa kutumia mbegu bora ya Naliendele wakati Rais alipotembelea kituo cha Mafunzo na utafiti wa mazao huko Naliendele,mkoani Mtwara jana mchana.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nyundo Mtwara vijijini jana jioni muda mfupi baada ya kukagua na kuzindua mradi wa maji kijijini hapo.Mradi huo unafadhiliwa na shirika la AMREF(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2011

    Maji tunataka majumbani sio kubeba ndoo kichwani kila siku!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2011

    hii so called miradi ya maji ingekuwa inafanya kazi hakuna mtanzania angekuwa na uhaba wa maji.Viongozi wetu waache siasa wafanye vitu kwa maendeleo ya taifa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2011

    Usituambie anasalimiana na wananchi sema WATOTO! Ebo!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2011

    Wewe anony wa kwanza umenivunja mbavu leo..nimecheka hadi basi.

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...