Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Ramadhan Khalfani (kushoto) akijadilina na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Mh. Meck Sadiq (kulia) kwenye viwanja vya maonyesho ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya kutembele mabanda mbalimbali ya wafanyabiashara.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Mh. Meck Sadiq (kulia) akisalimiana na mbunifu wa mavazi kutoka Ghana,bibi Delight Forkuoh (kushoto) kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere vya Dar es salaam wakati Mkuu huyo alitembelea banda hilo kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiq (wa pili kushoto) akiangalia masharti kwenye banda la mbunifu wa mavazi hayo ambaye ni raia wa Ghana,Bi. Delight Forkuoh (kushoto) kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere vya Dar es salaam wakati wa maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea.Wengine Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Ramadhan Khalfan( wa pili kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara,Masha Hussein(kulia).
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiq (kushoto) akisikiliza maelezo ya utengenezaji wa masharti kutoka kwa mbunifu wa mavazi hayo ambaye ni raia wa Ghana,Bi. Delight Forkuoh (kulia kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere vya Dar es salaam wakati wa maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea.

NA JOSEPH ISHENGOMA,DAR ES SALAAM

Manyabiashara mmoja ametoa wito kwa serikali kutoa mikopo rahisi ya vifaa vya kufanyia kazi kwa wahitimu wa vyuo vya ufundi ( VETA) ili waweze kutumia kwa vitendo elimu yao na kukuza uchumi wa taifa.

Wito huo umetolewa leo kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (Said Meck Sadick) na Mkurugenzi wa P.M.Tito's (TWINS) Bwana Paul Michael katika viwanja vya maonesho vya Mwl Nyerere.

Kaimu Mkuu wa mkoa amefanyaziara ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho katika viwanja vya Mwl Nyerere ili kuangalia bidhaa mbalimbali zilizo kwenye maonesho hayo.

"Serikali ianzishe utaratibu wa kutoa mikopo ya vifaa kwa wahitimu wa mafunzo ya ufundi ikiwemo VETA. Isipotoa fanya hivyo, muda wa wahitimu wa vyuo hivyo utakuwa unapotea bure kwasababu wengi wao hawana uwezo wa kununua vifaa vinavyotakiwa kutumia taaluma yao, " amesema.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, kushindwa kuwawezesha kwa kuwapatia vifaa vya kazi wa hitimu wa vyuo vya VETA kunachangia kudorora kwa uchumi wetu kwani pamoja na kupata elimu ya ufundi, umaskini wa kipato walionao unawafanya washindwe kutumia elimu waliyonayo kujiongezea kipato.

"Tatizo kubwa walilonalo vijana wahitimu wetu wanaotoka katika vyuo vya ufundi sio uwezo wa kufanyakazi ni mitaji ya kununulia vitendea kazi," ameeleza.

Bwana Michael ametoa mfano jinsi yeye pamoja na wenzake waliopata elimu ya ufundi miaka ya 1980 walivyokopeshwa vifaa na Shirika la Viwanda Duniani (UNIDO) na kuwawezesha kutumia elimu yao na kukuza uchumi kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali zinatotokana na malighafi kutoka kwa wakulima wetu.

"Nilipomaliza madomo yangu ya ufundi miaka ya 1980, UNIDO walinikopesha vifaa kkwa masharti nafuu, nililipa kidogo kidogo mpaka deni lilipoisha. Sasa hivi nina vifaa vya kutosha kutengeneza vitu mbalimbali na nimeweza kutoa ajira kaw baadhi ya vijana ninaoshirikiana nao," amesema.

Kampuni ya P.M.Tito's inatengeneza vitu mbalimbali ikiwa kwa kutumia malighafi zinazozalishwa na wakulima hapa nchini zikiwemo mikanda, mikoba ya akina mama na akina baba na viatu.

Bwana Sadick ameridhishwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya bidhaa mbalimbali zilizoshirikishwa katika maonyesho hayo na kuwataka walioshiriki kwa mara ya kwanza kutosita kuendelea kushiriki katika maonyesho mengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...