Kijana huyu alipotea maeneo ya Chang'ombe karibu na keko ambapo alikua anakaa kwa bibi yake Mama Sabina Lujuo kwenye nyumba zilizoko karibu na ofisi za TRA, Changombe karibu na Keko Kijana huyu alikuja Dar toka Arusha kuja kwenye matibabu ambapo alikua anapata kwenye hospitali ya Muhimbili.

Kijana huyu alikua ana tatizo kidogo la uelewa hivyo hata kuzungumza anazungumza kwa shida kidogo na hata uelewa wake ni mdogo pia Kijana huyu alipotea wiki iliyopita ambapo alitoka nyumbani kama anatembea kidogo na hakurudi tena mpaka leo hii Taarifa zimetolewa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na hata polisi bila mafanikio

Wajihi wake
Anaitwa - Edward Stevin
Jinsia - Mwanaume
Rangi - Ni mweusi, mrefu kidogo
Umri - kati ya miaka 21 na 22
Nguo alizofaa - Suruali ya jeans blue, T.shirt ya Blue (yenye maandishi Thunder crazy)
Viatu - raba nyeusi (za reebok)
Alama - ana alama kwenye paji la uso (kovu dogo jeusi) kwenye shavu la kushoto
Yeyote atakayemwona tunaomba atoe taarifa kituo chochote cha polisi
Au apige simu zifuatazo
0754-270952, 0715- 270952

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...