kapteni wa siku hiyo na mfungaji wa goli pekee Machupa akikabidhiwa Kombe.
Jumamosi ya tar 23 July,Timu ya watanzania waishio Sweden ifahamikayo kama Kilimanjaro Club imefanikiwa kuchukua kombe la waafrika waishio Sweden kwa mara ya pli mfululizo baada ya kuwafunga Ivory Coast kwenye semi final kwa bao 4 kwa 2 na baadae kutinga fainali ambayo tulikipiga baina ya watani wa jadi Kenya na mara hii walileta upinzani wa hali ya juu kwa kudifensi vizuri sana licha ya kuwachezea nusu uwanza lakini walifanikiwa kulinda lango lao kwa juhudi zote mpaka kipindi cha pili kinamalizika ilikuwa bila kwa bila. Kipindi cha pili kilianza kwa kilimanjaro kushambulia kwa nguvu zote na ilikawia mpaka dakika ya 22 ndipo mshambuliaji machupa alipopachika bao pekee na la ushindi. Hongera Kilimanjaro club. KUTOKANA NA USHINDI HUO KILIMANJARO ITACHEZA NA KIKOSI CHA PILI CHA TIMU YA DJUR GÅRDEN ambayo iko kwenye daraja la kwanza Sweden ni nafasi ya wachezaji wetu kuonyesha vipaji vyao. Mechi itafanyika kwenye viwanja vya SKARPNÄCKS SPORTFÄLT. WOTE MNAKARIBISWA KUISHANGILIA KILMANJAROCLUB.
Kweli ushindi raha
Kikosi cha Watani wa Jadi waishio Sweden (Kenya).
kikosi kamili cha kilimanjaro club ambacho ni kikosi bora cha watanzania waishio ughaibuni.
Kikosi cha kili kikiingia uwanjani tayari kutoa fundisho kwa watani wetu wa jadi.
ANKAL
ReplyDeleteSisi hatujui kujifagilia. matokeo yangekuwa kinyume chake ndio ungejua hakuna dogo.