Kocha wa Timu ya Taifa ya Vijana,
Kim Poulsen
KOCHA Mkuu wa timu za Taifa za vijana, Kim Poulsen leo ametangaza kikosi cha wachezaji 30 wanaounda timu yenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya michuano mbalimbali ya kimataifa.

Poulsen ambaye kwenye anasaidiwa na Adolf Rishard amesema timu hiyo pia itashiriki michuano ya Kombe la Uhai itakayofanyika Novemba mwaka huu.Michuano ya Uhai inashirikisha U20 za timu za Ligi Kuu ya Vodacom.

Amesema Ngorongoro Heroes  itakuwa ni ya kuingia na kutoka kwa wachezaji kwani kigezo kikubwa cha kuchezea timu ni kiwango cha mchezaji, hivyo anatarajia yatakuwepo mabadiliko ya mara kwa mara.

Kocha huyo amesema lengo ni kuwa na wachezaji 50, hivyo ataendelea kuteua wengine kupitia michuano ya Rollingstone inayofanyika Arusha na vilevile wachezaji watakaosajiliwa katika timu za pili (U20) za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom ambazo usajili wao unafikia tamati kesho (Julai 20 mwaka huu).

Poulsen amesema timu hiyo kama ilivyo U17 itakuwa inafanya mazoezi ya wiki moja kila mwezi, kuanzia Agosti ambapo pia itakuwa inacheza mechi moja ya kirafiki.

Amesema angependa U17 nayo ishiriki michuano ya Kombe la Uhai, lakini uamuzi juu ya hilo unabaki kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Pia amesema U17ambayo ilishachaguliwa kupitia michuano ya Copa Coca Cola inatarajia kushiriki mashindano ya CECAFA yanayotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu Nairobi, Kenya.

Poulsen amesema mahali popote ambapo kutakuwa na mchezaji anayefaa kwa timu hizo anaomba afahamishwe ili aweze kumfuatilia kabla ya kuamua kumchukua au la.

Wachezaji walioitwa Kilimanjaro Boys ni makipa Juma Ally Seif (Kombaini ya Ilala), Saleh Malande (TSA) na Jackson William Wandwi (Azam). Mabeki ni Hassan Khamis Kessy (Mtibwa Sugar), Khamis Mroki (Mtibwa Sugar), Yassin Omary (Polisi Dodoma), Andrew Kassembe Mathew (Simba), Issa Rashid Issa (Mtibwa Sugar), Ally Feruzi Teru (Simba), Said Ruhana Samir (Kagera Sugar), Samuel Mkomola (Azam),Eric Mawala (Moro United) na Amani Kyata (TSA).

Viungo ni Madenge Ramadhan (JKT Ruvu), Frank Damayo (JKT Ruvu), George Mtemahanji (Italia), Seme Omega Sunday (Yanga), Ibrahim Rajab Juma (Azam),Abdallah Kilala Hussein (AFC Arusha) na Rajab Zahir (African Lyon). Washambuliaji ni Ayoub Saleh Kitala (Ruvu Shooting), Atupele Green Jackson(Yanga), Thomas Ulimwengu (AFC Sweden), Michael Victor Mgimwa (Mtibwa Sugar),Jerome Lambele (Moro United), Simon Msuya (Simba), Ramadhan Suzana Singa (Simba), Alex Joseph Setty (Majimaji), Renatus Leopold Patrick (Polisi Dodoma) na Edward Christopher (Simba).

Boniface Wambura
Ofisa Habari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...