Kikosi cha Simba kilichoifunga timu ya Bunamwaya ya Uganda mabao 2-1 na kuingia
nusu fainali ya michuano ya kombe la kagame
Mashabiki wa Simba wakimshangilia mnyama

Matokeo baada ya dakika 90
 Mshambuliaji wa Timu ya Simba,Haruna Moshi "Boban" akichuana vikali na beki wa timu ya Bunamwaya,Ronald Seku katika mchezo wa Robo fainali ya Mashindano ya Kagame-Castle Cup unaoendelea hivi sasa katika uwanja wa Taifa jijini Dar. Hadi mapumziko bao ni Simba 1-1 Bunamwaya na mpira unaendelea kwa kipindi cha pili cha mchezo. Mwisho Simba kashinda 2-1
Kiugo wa katikati wa timu ya Simba,Mohamed Banka akiachia shuti kali langoni mwa timu ya Bunamwaya huku beki wa timu ya Bunamwaya,Ronald Seku akijaribu kuuzuia mpira huo bila mafanikio.
Kina Ras Makunja wakiwasindikiza waamuzi wa mchezo huo kueleka katika chumba chao cha mapumzio.
Sehemu ya mashabiki wa timu ya Simba wakiwatukana waamuzi wa mchezo huo kwa madai kuwa wanachezesha mchezo huo kwa upendeleo.
hivi ndivyo hali ilivyo mpaka hivi sasa katika uwanja wa Taifa wa Jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2011

    mpira ni mchezo wa mapenzi au hamani ukipenda. ni wakati nchi za africa kutotumia ma police wenyewe silaa ndani ya uwanja, inaonesha picha mbaya . au wadau wenzangu mnasemaje kuusu hilo swala.
    mdau paris

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2011

    Inaonekana huo ndio mwisho wa uelewa wako ndugu yangu. Kwenye mpira huwa kuna watu wenye hasira mbaya sana na hao waamuzi ambao katika hali ya kawaida huwa huwa hawana upendeleo. Lkini kutokana na ushabiki na hasira za baadhi ya watu, waamuzi hao wanaweza kuhatarisha maisha. Hivyo suala la ulinzi ni muhimu sana, nenda popote huo ndio utaratibu. WEWE UMECHEMSHA, naona utasema kwanini kumna waliznzi hata maofisini au majumbani wakati kuna amani. Wewe!!!!!.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 07, 2011

    Mkuu hii picha ya mashabiki wa Simba haikupaswa kuwapo hapa kwani ina matusi mabaya hasa kwa Wamarekani. Pia nahisi hii tovuti inaheshimika sana na inaangaliwa na watu wa hadhi tofauti. Sasa I can imagine mtu mwenye hadhi yake kuangalia picha kama hiyo itaitoa thamani hii blog yako tukufu. Nakuomba kwa heshima na taadhima iondoe hii picha. Baadhi yetu tunaitumia hii blog kuwapasha wanafunzi wetu habari za kwetu bongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...