Ankal salamaleko!
Pole na matatizo ya umemezzz. nimekuona kule FB ukilalama kwamba Ngeleja kakupiga mtama. Ndio ukubwa huo. Leo nimekuja tena kufuatia ule msemo kuwa "mficha uchi, hazai". nami kwa vile nataka kuzaa acha nianike yaliyomo moyoni labda wadau watanisaidia.
Ni hivi ankal, mie ni mwanaume, umri miaka 48, nimeoa mwaka wa sita sasa na nashukuru mola tumejaaliwa wana wawili, wa kiume na wa kike. Nafanya vijibiashara vya kule chumba kirefu (long room) kama wakala wa kupakia na kupakua mizigo bandalini. Hivyo hela ya kubadilisha mboga nnayo na nnaishi kwenye nyumba yangu mwenyewe. Nimeacha kupanga mwaka juzi, baada ya kuhamia kwangu (bado niko banda la uani maana nyumba kubwa kwisha bado, usiniulize itaisha lini maana dili zimepungua kiasi) hivyo maisha ya kawaida nayamudu na mamsapu yupo poa - ila tu labda kwa hili nnalotaka kukuelezeeni.
Ni kwamba baaada ya kukubali matokeo kwamba umri umeshaenda na sasa nitulie, mwenzangu (shemegi yenu, ambaye nimemzidi umri miaka 20) analeta za kuleta. Yaani haamini kwamba sasa nimeamua kuwa na yeye tu (huko nyuma nlishaoaga mara 2, nikaacha kwa sababu zisizoweza kuzuilika) na kwamba haamini kwamba na yeye ataondoka kwangu nilete mwingine wa nne.
Yaani ankali utanionea huruma. Nikitoka kazini na kupitia kijiweni kubadilishana mawazo na washkaji inakuwa nongwa. Yeye shemigi yenu anataka niwe narudi homu moja kwa moja toka jobu na nisitoke. Nikitoka kila dakika simu. uko wapi? Unafanya nini?? uko na kina nani?? nipe niongee nao. Yaani kero bin shida. Mbaya zaidi, ingawa kweli enzi za ujana wangu nilikuwa hodari wa mechi za mchangani, lakini sasa nimeamua kupiga mechi rasmi za neshno tu ambazo ni halali. Yeye haelewi hilo.
Yaani roho inaniuma sana mwenzangu hataki katakata kuniaminini kiasi hata hivi sasa nikikaribia homu naweka paswedi kwenye simu ili asiichokonoe kuona nimewasiliana na kina nani. Halafu tena amefikia hata kunusa na kukagua nguo zangu za ndani ili kuthibitisha nini sijui yarabi toba. mradi ni karaha na karaha tu.
Hivyo ankal naomba mwongozo toka kwa wadau wa blogi ya jamii. Nifanzeje?? kumpenda nampenda sana tu, na kama nilivyokiwisha nuia, sitaki mwingine tena na mechi za mchangani nimekomesha kabisa kabisa. jamani nifanyeje shemegi yenu hanielewe??
Ndimi mdau wa blogi ya jamii
Dabo NN
Pole sana Mdau. Ila kikubwa nacho kiona hapa ni tofauti ya Umri. Thinking yenu nitofauti sana. Angakua anasoma kwa maelezo yako angekua High school. Cha kufanya kwasababu mshazaa watoto niku jitahidi mnawalea watoto vizuri katika mfano mzuri. Pili Mshughulikie vizuri, Most women are insecure kwasababu hawatoshelezwi ukizingatia bado mdogo na damu inachemka. Anza kumtosheleza kwenye mechi atasahau kila kitu. Kwahiyo acha uvivu na mshughulikie vizuri kwenye mechi.
ReplyDeleteMsikilize na umtii mkeo, maana makosa ulishayafanya hapo awali, huwezi kuwa huru kama unavyotaka tena, ndio gharama ya dhambi hiyo kaka, huchopoki, inakuwa inakurudia rudia (what goes around comes around). Kama vipi, hasa ukuzingatia umri wako, uwe unatoka nae karibu kila mara ili umridhishe kuwa huna ishu zisizofaa tena. La msingi ni umuheshimu na kumsikiliza sana ili arejeshe uaminifu kwako. Inaonekana anakupenda sana, na wewe unampenda pia, hivyo ni kwa nini unajiruhusu kuwa chanzo cha mgogoro??
ReplyDeleteNa kwa nini uweke password kwenye simu dhidi yake?? Unapaswa umruhusu akusomee hata meseji zako pindi zinapoingia. Hivi unajua kweli maana ya ndoa kaka?? Usimfanyie mambo ya namna hiyo, sio utu wala heshima, huyo ni WEWE na wewe ni YEYE, usijitenge nae.
Unayaongelea maisha yako ya awali kama vile ni sifa. Ficha aibu zako, sio ujanja huo.
ReplyDeleteHabari kaka...hongera sana kwa maamuzi ya kutulia uliyochukua na pole sana kwa matatizo yaliyopo,inaonesha wifi yangu uaminifu kwako ulitoweka siku nyingi kwasababu ya background yako ya kuwaacha 2 waliopita...ushauri wangu ni kuwa uwe na subira sana kwa vile kujenga tena uaminifu si kazi ndogo na umueleze tena na tena kuwa umeamua kuwa na yeye vikifuatana na vitendo vyema,yaan jitahidi umsikilize( akikwambia utulie home utulie,jitahidi kurudi mapema,ukiwa na rafiki zako call her japo asalimiane nae mmoja ili wasiwasi upunguke) jitahidi na haya mpaka atakapo badilisha mtazamo wake but subira inahitajika kama nilivosema....Lakini kikubwa zaid ni kumuomba Mungu juu ya hili vile unania nzuri Mungu atakusaidia na mtapata amani ya ndoa.
ReplyDeleteNisamehe kama ntakua nimekukwaza vile mie sio mtaalam but mawazo yangu ni hayo.
Mdau
Mmm hiyo tunaita gubu unajua gubu likizidi ni kero au labda ni wewe hapo mwanzoni umemfanya asikuamini. lakini pia jitaidi kumuelimisha kwa vizuri tu ipo siku atakuelewa MDAU U.S.A.
ReplyDeletewatu humu watasema tofauti ya umri ndo tatizo. uwambie hiyo ni namba tuu.
ReplyDeleteDABO NN. POLE SANA YANAYOKUKUTA YANATUKUTA WENGI. HATA MIMI MANYANGA NILISHAWEKA CHINI NIKAONA NITULIE NA MWENZANGU LAKINI YALIYONIKUTA MUNGU ANAJUA. BAADA YA KUJIULIZA SANA KWANINI NATUHUMIWA KWA MAKOSA NISIYOFANYA NILSHINDWA PATA JIBU. SIKUMOJA NIKAAMUA KUWAULIZA KINADADA FULANI KINAMNA. WAKANIAMBIA UKIONA HIVYO UJUE SI AJABU MWANAMKE NDIE ANAYEKUZUNGUUKA. JASHO LIKANITOKA KWELI. NIKAAMUA SIKU NYINGINE NILIVYOKUA NATUHUMIWA NIKAMUOMBA MAMSAPU AFUNGUE E-MAIL YAKE NILYO YAKUTA HUMO NDANI MUNGU ANAJUA. NIKAMWAMBIA UNANINYANYASA KWASABABU UMESHANIPA TARAKA YA KIROHOROHO AKAKOSA JIBU. NIKAMWOMBA AONDOKE AKANZA KULIA KUPIGA MAGOTI SASA NIMEMPA NAFASI YA MWISHO. AFADHALI YA WEWE MWENZIO MDOGO KWAKO MIMI TUNALINGANA YAANI NATAMANI HATA KUMPELEKA MILEMBE. AFADHALI YAKO WEWE WAPITA SALIMIA JAMAA MIMI NANYWEA NYUMBANI TENA HATA KUPIKA NAPIKA. CHAKULA CHAJIONI NATOA MPAKA ANASHINDWA MWENYEWE SASA HATA SIJUI HII DUNIA VIPI LEO. NAKUSHAURI USIWEKE PASSWORD KWENYE SIMU IKIWEZEKANA MPE ASOME HATA HIZO MSG LABDA ATAZOEA. HUYU WANGU BAADA YA KUMGUNDUA NAONA NIMEPATA AFUENI KWASABABU AMESHUSHUKA. NANIMEMPA RUHUSA YA KUFUNGUA HATA MAIL ZANGU NA SIMU HATA KUPOKEA SIMU MIMI SINA WASIWASI KIZAIZAI NI KWAKE TUU.
ReplyDeleteNaomba nikuulize maswali mawili matatu wewe double N:
ReplyDelete1.kwani ni lazima kwenda kubadilishana mawazo kijiweni na hao unaowaita washkaji?je ni kila siku?
2.Mkeo anafanya kazi au la?
3.Kwani haiwezekani kwenda nae huko unakokuita kijiweni? dili gani hizo msizoshirikisha wake zenu? hatuombei mabaya lakini kutomshirikisha mkeo kunaweza kuleta madhara endapo utatangulia kufa halafu mke na watoto wasijue kama ulikua na biashara au investment partners. ni vizuri kuwa muwazi,kama vitu sio haramu,basi mpeleke kwenye hayo madili yenu.au siku nyingine waalike hao washkaji zako nyumbani ili muongelee hapo nyumbani na sio kijiweni.
ukweli ni kwamba,wanaume wengi wa TZ hawaoni umuhimu wa wake zao au niseme culture imewaharibu na kuona kuwa mwanamke ni wa kukaa nyumbani na watoto wakati mwanaume anapuyanga mtaani akidai anafanya dili na washkaji. ulaya / marekani vitu kama hivyo hakuna. mwanaume anatoka kazini anaenda home straight na ndivyo inatakiwa kuwa kwa TZ. rudi nyumbani,muone mkeo na watoto.kama ni kitu cha muhimu toka lakini huwezi kuniambia kila siku kuna madili ya kuongea na washkaji. Ndo maana hiyo ni ndoa yako ya 3.
kaa chini ufikirie. hakuna mwanamke atakayeamini kua mumewe hana kimada wakati harudi nyumbani baada ya kazi badala yake anaenda kijiweni.
na ukishaoa mke wa 4 utapata faida gani? sana sana utapata kimeo kitakachokuchezesha rumba la kisawa sawa.wahenga walisema mkataa pema,.......
hayo ni mawazo yangu.subiri wengine nao wakupe mawazo yao
Umepata mwenza anayekujali safari hii, waliopita walikuwa hawakupendelei mema. Jaribu kufanya atakavyo mwenza huenda ukawa na furaha nyingi kuliko hizo za vijiweni na neshno. Vijiwe zaidi ya kusengenya na umbea hakuna zaidi. Mechi za neshno zaidi ya kuchunwa hakuna chengine utakachopata. Ughaibuni huku ni kila mtu na mwenza wake hakuna ndugu wala rafiki wala mpira na yeye ndiye next of kin.
ReplyDeleteMlime talaka ya kwanza kama appetizer..ili ajiweke sawa
ReplyDeletemdau hiyo ni rahisi tu. tafuta mtu wake wa karibu kama dada au shioga yake ambae wanaelewana sana na humsikiliza sana. mpe malalamiko yako na muombe aongee nae ili apunguze kidogo wivu. naasema apunguze sio aache maana wivu ndio mapenzi. akishaongea nae najua kutakuwepo mabadiliko.
ReplyDeletelakini kwa upande mwengine acha kulalamika sana maana ana haki kukuulizac upo wapi muda huu? au kuwa na mashaka iwapo umechalelewa kurudi home. punguza vikao visivyo na maana rudi home mapema. huyo ni mkeo nae ana haki zake. jee na yeye akiamua kuwa kiguu na njia utamuelewaje?
fikiria pande zote mbili sio kkwa kuwa ni mwanamme ndo ujipe mamlaka makubwa ya kufanya upendavyo.
nakushauri kijana
Huo ndio ubaya wa umalaya unakuwa uwaminiki.. Jiulize toka lini shetani akawa malaika shenzi mkubwa? Haya soma Muongozö mtoe out sehemu nzuri ongea nae mpe ukweli wako atakuelewa tuu..
ReplyDeleteBy Ukuni
Kwanza kabisa Mdau unatatizo la kiswahili sio shemegi ni shemeji .
ReplyDeletePili mambo yako na mkewe mmalizane wenyewe sio mpaka utangazie umati wote dunia. Pumbavu sana ! Huo ni uzahifu wa hali ya juu; Eti ananusa nguo zangu za ndani" Pumbavu tena. Mnafikiri umalaya ni sifa " eti enzi zangu nilikua hodari wa mechi za mchangani" Pumbavu tena! Unaacha kutafuta hela unajisifia umalaya ! Shenzi ! Jibwa wewe! Yani ningekua nakujua ungenitambua. Huwezi tumia media kizembe zembe!
Fanya kazi acha uzembe ! Eti umejivua Gamba . Nyoka ni nyoka tu hata kama akijivua gamba sumu ni zilezile! Tapeli wa mapenzi wewe.
Namalizia kwa kukuambia pumbavu mara 7!
Pole sana kaka yangu kilicho kuponza ni huo umalaya wako wa zamani sasa shemeji yangu anakuwa hakuamini sasa wala usitafute mchawi ni wewe mwenyewe kuwa muwazi na muonyeshe uwaminifu na zidisha upendo tu shemeji mwenyewe atakuamini na utakuwa huru.
ReplyDeleteMdau
kisiju pwani
Dabo NN,
ReplyDeleteWaraka wako bado unaonyesha wewe ni mtaalam wa mechi za kimataifa za kupimana nguvu kwenye uwanja wa ugenini (a.k.a MANG'ELA).
Kosa kubwa mnalofanya watu katika maisha/mapenzi ni kuwa mnataka kuaminiwa, huwezi tu aminiwa, ni lazima uandae mazingira ya kuaminiwa.
Kama nilivyosema hapo juu, wewe bado mtundu, na kuthibitisha hili umesema kuwa unapokaribia nyumbani unaweka simu password. Sasa kwa nini unamuwekea mkeo password? ina maana kuna "vikuyu" umeisha wasiliana navyo au unawasiliana navyo na unataka kutafuna ushahidi.
NAOMBA NIKUSHAURI, ACHA KABISA UTUNDU, ACHILIA MBALI UJANJA UJANJA NA NJIA BORA ZAIDI YA KUMALIZA HILI TATIZO NI KUFUATA ANACHOTAKA MKEO, VINGINEVYO KAMA BADO UNAONA KERO BASI NILETEE MIMI HUYO MKEO MAANA NIMEISHA TULIA.
Kama wewe ulivyokuja kuomba ushauri kwetu, hujui yeye kamuomba ushauri nani, itakuwaje atakapoomba ushauri kwa mpumbavu naye akamwambia, "SHOGA PRESSURE YA NINI, NAWE GAWA TU!" Huoni hapo utakuwa umeelekezwa kibla?
TULIA LEA NDOA YAKO, HUU SIO WAKATI WA WEWE UKITOKA KAZINI KUPITIA VIJIWENI, NENDA KWA MKEO HUJUI ANAKUMISS?
Wasalaam,
MZEE WA PLENTY
Anaogopa UKIMWI bado kijana hataki kufa na mapema. Mhakikishie kwamba mchezo umeacha la sivyo na yeye ataanza nje!
ReplyDeleteWEWE TULIA TU KAMA UNAMPENDA KWELI KWANI HATA YEYE MWENYEWE ATACHOKA TU KUKUFUATILIA AKIJUA KAMA UMETULIA.
ReplyDeleteDabo NN,
ReplyDeleteushauri wangu unafanana na wa mdau mmoja hapo juu,kuwa mpe mkeo security,mhakikishie kila siku kwamba wewe umefika Kigoma tayari na kuwa huko kijiweni ni washkaji tu na kama anataka na yeye hata mara moja moja aje ajionee na apate moja baridi, akipiga simu pokea mtulize na mpe washkaji waongee nae pia. Pia hakikisha jioni ambazo unawahi straight nyumbani ni nyingi kuliko zile unazopitia vijiweni,wewe familia yako iko kijiweni au nyumbani?acha ujinga sasa una miaka 48 au?watoto wanam-miss baba vile vile sasa unataka wanao pia wasahau hata sura yako?mwenzako yalishamkuta siku moja anarudi home mwanae akamuuliza mama yake ni njemba gani hii imekaa mezani?kumbe ni baba mwenyewe, watoto hata sura hawaikumbuki.
Sasa ukishaaminiwa uhakikishe huyo ndio mtu utakayezeeka nae... mara moja moja ukicheza mechi za mchangani hakikisha mipira kibao...hapo najua mwanaume malaya atabaki tu na hulka yake,kwa hiyo usikonde cheza tu mara moja moja lakini mipira mbele na pilipili ibaki shambani... maana yake mkeo asijue ushenzi huo...
Ni mimi msemakweli ninaowajua wanaume wa kibongo,sketi ikipita lazima wageuke, Bisheni sasa...
wewe kuacha wawili unaona sifa. mnatesa watoto wawatu mioyo, mnawaharibia maisha yao na kama mmezaa nao ndio kabisa mmeharibu maisha ya watoto wasio na hatia au kuombwa kuzaliwa duniani. sasa wewe kwa kuwa una watoto hataki utese watoto kama wengi wanavyotelekeza familia zao au kupata vvu inayoweza waacha watoto matesoni. wakina kaka, ndugu zangu, baba zetu mbadilike. Kubadilisha wanawake na kutelekeza watoto na wake na kubadilisha kila siku ni aibu kwa jamii na ujinga wa iana yake wa kutesa watoto wasio na hatia duniani.
ReplyDeleteyep, ankal leo umenifurahisha sana kwa kuweka hii hoja..
ReplyDeleteglob yetu naona imerudi upya sasa.. kama enzi zileeee za MANKA!
Mwambie akizidi kukuchachamalia kwa mazuri unayotenda,Utarudia misri tena ili ndipo akome zaidi.Huyo anakufanyizia mwenyewe hebu mchunguze sana.
ReplyDelete