Ankal, 
Mimi ni msichana wa kitanzania naishi tanzanianafikiria kwenda America kitongoji cha michiganHolland, sijawahi kwenda America au kuishi hukokama mtu anajua homepage ya  chama cha watanzaniawanaoishi mji huo naomba mnisaidie angalau niwe naidea kidogo kuhusu mji huo na kipindi ambacho nitakuwahuko niweze kukutana na watanzania wenzangu.
asante sana.
upendo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2011

    Usiwe na wasiwasi dear, ughaibuni huhitaji kujua mtu, unachohitaji ni pesa na lugha!!! Na ukishafika pia hivyo havihitajiki!!!! Pia ujuwe kuwa waTz mwisho ni kwenye mnuso baada ya hapo kila mtu kivyake. Na kwenye mnuso wanakwenda wale wenye makaratasi!! Jaribu zaidi kujihusisha na ulichokiendea!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2011

    Mdau wa kwanza ameninyanganya tonge langu. Ameongea ukweli kabisa fuata ulichoendea watanzania wakishakuwa nje ya nchi wanabadilika. They are not reliable. Uzuri ni kwamba nchi zilizoendelea kila kitu kinajieleza chenyewe huhitaji mtu wa kukuongoza. Kama unaenda kusoma bila shaka chuo unachokwenda wamefanya maandalizi ya kukupokea.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2011

    Hi usitegee sana ndugu huko. kila kitu kinawezekana tu bila ya mtu kukushika mkono. Cha mhimu ni kuwa na hivyo vinavyo kupeleka huko. Utapata wenyeji baada ya kuwa umefika na ume-settle, huyu unayetaka akusaidie kabla haujafika anaweza asiwe rafiki mzuri. Hauwajui. Mchangiaji wa kwanza na wa pili wamesisitiza hilo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2011

    TUMIA GOOGLE, WIKIPEDIA UTAPATA HABARI ZOTE MPAKA PICHA KWENYE GOOGLE IMAGES. ACHA UVIVU.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 29, 2011

    Ni kweli wadau walichokisema, Watz usipende kampani yao nende kwenye misiba, sherehe wakikuambia, wasipokuambia achana nao. Mi niko ughaibuni na nilipofika mkoa niliofikia sikuupenda nikaomba nihamie campus nyingine kwenye mkoa mwingine hapo shuleni alikuwepo Mtz akampigia Mtz wa kule nilipokuwa nahamia ili anipokea tu na kunionyesha hapo kwenye accomodation. Weee ninajutaga sana kwanini alikuja kunipokea kwani maneno anayosemaga hadi leo msipende kujua. So kama unajua unakoenda jaribu kuwa wewe kama wewe,maanake mi chichemi. Ila kama unapenda maneno usifuate ushauri wetu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 29, 2011

    Pia uwe mwangalifu watu wamichigani watakusaidia if they are interested in you, na wengi wao baadae utawasikia nilimsaidia huyu alipokuja mara hivi mara vile, kuwa mwangalifu nasema haya kutokana na experiance niliyoiona hapo. Na hao ni watu wazima kabisa na watakutumia

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 29, 2011

    Watanzania! Michigan! Unatafuta balaa wewe!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 29, 2011

    Upendo fuata huo ushauri mzuri kutoka kwa wadau hapo juu.Thanks wadau

    David V

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 29, 2011

    Hii Kali...

    Usitake ncheke mie yani unavyo ulizia hicho chama kama vile unatoka MAHENGE kuja Dar... Kifupi na agree na hao wadau yani kama una Address huitaji kujua watanzania wanakaa sehemu gani... by the way mi nina ndugu ila nahofia usije ukamzukia home kwake ikawa balaa...

    Enjoy your trip to America..

    I am out...

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 29, 2011

    Haipaswi kuendelea na matatizo watu wanayopata kwa kisingizio kwamba watu waliowengi wanafanya. Kimsingi ukipata mtu anayejua maisha ya huko anaweza akasaidia. Namuomba mtoa mada aweke email yake mimi nitawasiliana nae kupitia email na nitamsaidia kumpa contact ya Mtanzania ambaye anaishi huko.

    Watanzania tubadilike kwa maana tusiendeleze vitu ambavyo havina tija kwetu badala yake tunapaswa kuanzisha mtandao ambao utatusaidia sisi na vizazi vyetu. Nchi nilipo wenzetu Wakenya, Wazimbabwe, Botswana n.k wanamitandao yao kiasi kwamba mgeni akija anapokewa na kuonyeshwa njia vizuri mpaka mambo ya kazi tayari wanamitandao lakini mtanzania atakupeleka Disco au sehemu nyingine za starehe badala ya kukupa michongo ya maisha. Inaboa

    ReplyDelete
  11. mtafute Maija bintio Abdallah kwa anwani ifuatayo bestamaija@yahoo.com naye atakusaidia. Yeye kaolewa huko

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 29, 2011

    Kweli kabisa ,ukiwa nje ya nchi bora upate rafiki wa kizungu mtaelewana.Watanzania wakiwa nje ya nchi hawasaidiani kabisa kila unayejaribu kuwa nae karibu anafikiri unataka pesa kwa hiyo wanakimbiana.Nimeishi nje kwa miaka miwili ikanitokea hiyo mwisho nikaamua kuwa na marafiki wa kutoka China na Indonesia ambao tulielewana sana.Fuata ulichoendea

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 29, 2011

    Dada wewe unatafuta KUPAKATWA KAMA SIMBA. Am sure not long before you will be able to understand me.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 29, 2011

    Kusema kweli watnzania wa ughaibuni sina hamu nao. wengi ni wanafiki na kama alivyosema Anony mmoja hapo juu, wengi wao wanapenda usengenyaji kuliko kusaidia. Yuko tayari akudanganye ukosee kitu ili apate cha kuksengenyea. Kwnye pati ni wazuri sana wa kualika wenzao lakini kwenye fursa za masiha hakuna anayetaka kusaidia.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 29, 2011

    WEWE UNAWATAFUTA WATANZANIA WA MICHIGANI?KWA TAARIFA YAKO USIMUANI MBONGO YOYOTE,HATA HAO WANAKUPA NAMBA ZAO HUKU UKAWATAFUTE ANGALIA SANA.MIMI NILISAIDIWA TU NAWENYEJI KABILA YA KUWAFAHAMU WABONGO,KWENYE KILIO AMBAO MAJIBU YAO NIYA MKATO KUSEMA LAKWELI WENYE KUSAIDIA NI 2 KATI YA 10.WEWE NENDA ILIMRADI UNAIJUA LUGHA NAKUTAKIA MAISHA MEMA NASAFARI NJEMA YA MICHIGAN.MIMI MDAU KUTOKA EUROPE.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 29, 2011

    Yaani wadau hii ni kweli, hata kwenye hizo sherehe mnazokutana mjaribu kuliongelea hili Watanzania. Mimi nipo mji fulani UK, Watz hawana mshikamano hata kidogo, kila mtu kivyake, hata ukiwa na simu zao au email addr zao, huwezi kuwasiliana nao maana utakapofanya hivyo wanajidai wako busy kuliko kawaida. Wanapenda kutembelea miji mikubwa, starehe, na pia ukijaribu kuwabefriend utashangaa wanavyokukwepa. Tofauti na wa-Nigeria, Wachina, Wakenya, na wengineo. Jamani waTz ughaibuni badilikeni. Mimi mwenyewe hapa nimejikuta niko mwenyewe tu, kuna watu km 6 hivi nawajua hapa jirani yangu, nimejaribu kuwaalika kunitembelea ila wako busy, wala karibu hakuna. Duh, kweli kazi tunayo! Wewe Dada nenda, ishi km ukipata mtu mzuri haya, ufurahi tu.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 29, 2011

    Karibu dada hiyo web hakuna huku labda nenda mwanakijiji.podomatic utapata za state nyingine.Dada unaitwa nani?

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 29, 2011

    upendo nakushauri kama unavijipesa vyako wala husimkopeshe mtu kabisa, nipo nje nilimsaidia dada Laura taruka usd300 basi akazuga simu yake kapoteza kwenye tax tukawa tunachat tu, kwenda kuchukua akaniomba sana kuwa akifika dar tu atanitumia, basi sikutaka fujo nikamuamini maana nilimuheshimu kama sister na wala sijawai hata kumtamani lakini sijui alitaka kunitega tu, kwenda dar hajibu messege za facebook, nikasaka no zake nikampata kumpigia akasema ndiyo anaenda kutuma hadi leo hii simu hapokei na fb kaniblock ndugu zangu wakimpigia anasema atatuma, huku sina kazi anajua naishi kwa shida yeye mtoto wa kigogo mimi masikini, sasa anataka kunipa dhambi gani sijui, maana nilitupiwa vitu nje na mwenye nyumba nimepoteza cameras,simu, ipod na vitu vidogo vingi tu, na sasa natafuta nauli niende likizo nimuangalie sura yake ikoje.so wabongo kama humjui husitafute kumjua kabisa maana laura na business yake nilimkopesha pesa za kuongeza mtaji hana shukurani

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 29, 2011

    May be Huko Us na Kwingineko lakini Watz tunaoishi Uturuki 90% tunajuana na tunatembeleana hasa wakati wa Summer kwani wengi wetu ni wanafunzi. Tatizo watz sisi ni wavivu na tunapenda sana kudoea vya wenzetu. Sasa kama mtu anaishi ughaibuni na ana maisha magumu halafu ww uende kwake huna kazi na wala huna mwelekeo unategemea nini? Wewe dada nenda huko fuata issue yako iliyokupeleka ukishatulia ndio may be uwatafute hao watz. Hao wanao-comment hapo juu wengi wao wako huko na ndio wenye experience. Usithubutu, maana kama wewe ndio mwenye unafuu watakugeuza chambo.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 29, 2011

    march mwaka huu mie pia nilipata bahati ya kupita Marekani. Kwa kumbukumbu za watu wema niliowafahamu ktk kupita nchi nyingine hapa duniani nilizowahi kupita, niliweka ombi langu hapa. 90% ya watu walinisagia hapa. Ila nilipata watu wachache ambao walinisaidia sana pale DC, Va, MD, NYC na hata Fl. Pamoja na kuwa nilikuwa na per diem bab kubwa na 5 star hotel, watanzania hao walifanya stay yangu US iwe brighter. Nilipelekwa African Village, maduka karibu yote niliambiwa na nilipewa info muhimu nyingi tu (mfano hotel ilikuwa Rosslyn, jamaa wakanishauri nichukue Metro bus 5A toka Dulles kwa $6 badala ya TAXI around 65$. Ushauri wangu: mbongo mbaya hata geto ni mbovu. Iwapo mtu amekua vyema Ulaya/US haitamuaribu. Ila kumbuka: pesa huku ni ngumu kama vile vile afrika hivyo msaada unaohitaji usiwe mzigo kwa wenyeji.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 29, 2011

    Mimi niko US na bahati mbaya siko Michagani lakini niko Minnesota.Kusema ukweli wapo watu wema na wabaya.Na huko Michigani nina ndugu zangu lakini nagopa kuku-indroduce kwao kwa sababu nisije kukuingiza kwenye mdomo wa simba.Muhimu ni kwamba kama walivyosema wengi pale juu huna haja ya kuogopa huku mambo yanajiseti tu mradi una uhakika na kile ulichojia na vilevile una mahali ulipoandaliwa kufikia na pesa yako ipo kujikimu basi.Hao wabongo utakutana nao tu huko njiani ndiko mjuane. Ungekuwa unakuja Minnesota ningekuambia Jumapili uende kanisa la Kiswahili Minnesota huko ndiko utakutana na watu wengi tu na wengine wenye moyo mzuri.dada karibu sana US.

    Mdau US

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 29, 2011

    It is good to know people from your country, but I would suggest that you put all your trust in God and he will direct your path. Do not worry about the future or what you gonna do without Tanzanians. You have to know that God is the one who hold your future so trust him only; come here with your sound mind.
    All the best and God bless you.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 29, 2011

    nyie mnaosema watanzania wa ighaibuni hawasaidiani acheni unafiki. mbona ndugu zenu wakifa mnatuchangisha na tunachanga hadi nauli za wasindikizaji wa mwili kama huo si msaada ni nini? kutwa mnaitisha michango kama vile ni lazima halafu mnasema hatusaidian! mnataka tuwe hadi tunawaogesha ndo mjue tunawasaidia? mtu akifungwa jela michango, mjomba akifariki kijijini mchango na hiyo hiyo michango watu wamenunua hadi nyumbas na magari. kwa hiyo kama mnaona watanzania wa ughaibunu hawafai acheni kutoa matangazo yenu ya michango!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 29, 2011

    Maoni yaliyotolewa yote yana ukweli na mengine yana njonjo.Ni kweli kuwa watanzania wengi hawataki kumpokea mtu baada ya kupata matatizo nao kwa hiyo tusiwalaumu sana.Kwa mfano kuna mtanzania alimpokea mtu mtu toka nyumbani akamsaidia kila kitu kama Kumpeleka shule for 3years na kazi kwenda na kurudi hadi akawa sawa, akahamia kwake na akapata mtu wa kumuoa na kupatata makarasi.Sasa huyu jamaa aliyempokea akamuomba huyu mtu amuoe ili nae apate makaratasi lakini huyu mtu alimwambia kuwa siwezi nataka kumwoa mtu mwingine na yeye ndugu yake atamwoa mdogo wangu.Sasa niambie mtu kama huyu atakubali kumpokea mtu tena?

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 29, 2011

    Watz hawana mpango, mimi niko ughaibuni nasoma nakaa family house za university, majirani zangu ni kutoka Nigeria na Zimbabwe, huwezi amini watoto wetu wanacheza kama wako uswahilini, nyumbani kwangu wanaingia na kutoka na wakwangu wanaingia kwenye nyumba zao na kutoka. Mmoja wetu akihitaji mtu wa kuchunga watoto wakati anatoka, anasema tu tunawachunga, yaani sio kucheza tu hata wakikuta chakula mezani wanakula. Nina marafiki kutoka Kongo, Angola, US, Ghana, Sudan, UK, Malawi na Gambia pia, na dada mmoja wa kipemba ambaye yeye anakaa mtaa mwingine mbali na kwangu, lakini wajameni she is my sister, anaweza kuja na samaki wake akasema hebu kaanga tusonge ugali tule, maisha yanaenda. Na dadaangu mwingine akaa mtaa wa mbali kabisa tunatazamana kama ndugu wa damu.

    Na hiyo ni kwa sababu naishi kijijini, ndio Watanzania wapo nimeshakutana nao lakini kwa vile wananiona mimi masikini wala hawanisogelei na mimi naona ni good riddance, utajiri ntaupata wapi wakati mie mwanafunzi?

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 29, 2011

    HATA KAMA NINGEKUWA NI MIE SIPOKEI TENA MTU TATIZO LA WATANZANIA AKIWA NA SHIDA ANAKUWA NI MTU MNYENYEKEVU SANA ILA AKISHATIMIZA MAHITAJI YAKE NA YAKE YASHAMYOOKEA WALA HAKUTHAMINI TENA

    HUYO DADA AMEONESHA KWAMBA YEYE SI MTU WA SHUKURANI KABISAAA KUMFADHILI KOTE HUKO UMEMSAIDIA MANGAPI MIAKA MITATU MTU ANAKUPELEKA SHULE NA KAZI ANAKUPELEKA NA KUKURUDISHA UTAPATA NANI KATIKA DUNIA HII AKUFANYIE HIVYO HATA NDUGU YAKE MWENYEWE LAZIMA AKUSIMANGE SANA .

    YANI HUYO WEWE MPE KUBWA MUAMBIE TU UKWELI UMESHASAHUA FADHILA ZANGU? M MUNGU ATANILIPIA , MALIPO HAPA HAPA ATAMUOA HUYO MTU NA WATA MDINAI HAHAHAH

    NJOO NIKUOE MIE KAMA UNASIFA NINAZOTAKA

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 29, 2011

    Holand kwa taarifa yako hakuna mtanzania hata mmoja wewe ndio utakua wa kwanza ndio utaanzisha na hiyo website, kama jina linavyosema wenyeji wa hapo wametokea Holand Netherlands, ndoa yangu bado changa naogopa kukufahamu samahani,ila jihadhari na watanzania, ujumbe fata kilichokuleta kama unapenda sana watanzania baki huko huko uliko

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...