Ugumu wa maisha umenipelekea kufungua 'kiduka' ili kupunguza makali ya maisha. Nimemwajiri mtu wa kuniuzia hilo duka lakini nahisi ananiibia kiaina, Lakini kimahesabu nimeshindwa kulithibitisha hilo.
Kuna mtu akanishauri niwe nafanya stock taking kila mwisho wa mwezi ili kujua kilichoingia na kilichotoka.
Nimefanya hivyo kwa kuthaminisha mali zote kwa bei ya kuuzia kwa mwanzo wa mwezi na mwisho wa mwezi. SWALI: ntawezaje kukokotoa kujua kama naibiwa? Angalizo: mahesabu shuleni yalinipitia kushoto. Naomba msaada wenu wadau.
Wako Mdau
Kama hujui kuhesabu maana yake hutaweza kujua maana hata ukiajiri mtu wa kukuchukulia mahesabu naye atakuibia maana utamlipa na pengine akiona kuna pungufu kubwa atamtonya muuzaji ili apewe kitu kidogo alizime. Hii ndio maana TZ hawakamatwi maana wanakwiba na wakija auditor wanagawana kitu kidogo linazimwa! Jifunze hesabu kama unapesa, ita mwalimu nyumbani, ni kujumlisha na kutoa tu.
ReplyDelete1.Kama unaweza nunua online security camera,unaona live movement,especially pale juu ya cashier,
ReplyDelete2.Jamaa anaweza kuwa anauza vitu vyake kupitia dukani kwako,hivyo stock yako inakuwa paleple ila mauzo hupati,yeye ndio anakuwa anapata faida.
Babu kwakua inajulikana kuwa hali ya maisha ni ngumu lakini haimaanishi kuwa kila mtu ni mwizi.Hizo ni hisia zako tu kwamba usijiamini kupita kiasi ila kwaha hata siku ukiibiwa KWELI, usishindwe kung'amua.Kama Stock take yako ina-balance baina ya urari wa kuanzia na ule wa kutimiza kisha ukabakiwa na faida yako baada ya kutoa manunuzi ,hapo kila kitu kipo poa.Kuibiwa huwezi kukwepa kwakua uibaji pia una mbinu mbalimbali.Bidhaa inaweza ongezwa bei(cha juu) na bado wewe hesabu zako zisibadilike.....Ushauri wa bure ni kuwa kama hesabu zako zinaenda sawa basi hicho cha gizani usichokijua mwache nae kimsaidie kujikimu kimaisha maana huenda naye anategemewa....
ReplyDeletekiutaalamu stock taking inatakiwa kila siku.ni too confusing ukifanya kila baada ya muda mrefu.endelea kutake risk ukijiinvolve kisawasawa utaicontrol tu.usiogope kuibiwa ila dhibiti kwa kiwango kikubwa.wabongo issue.
ReplyDeletewajanja sana hao wanaleta bidhaa zao zinazofanana na zako wanauza za kwao wanachukua mshiko kiulainii, wee umali yako inadoda hata ukipiga mahesabu unaoa vitu vipo unadhani mali haiuziki kumbee! na mapharmacy ndio wana huu mchezo sana!
ReplyDeleteHutoweza kujua unaibiwa na wala huibiwi ila jamaa anauza mali za kwake kwenye duka lako,wewe kila ikiangalia stock imejaa na wateja kibao,jamaa ndio kapata mlango wa bure na unamlipa kuuza vitu vyake na sio vyako.
ReplyDeleteNimevumbua excel system ya kukuwezesha kucontrol business yako yaani rekodi ya stock, mauzo, faida, hasara, onezeko au kupungua kwa mtaji n.k kwa kila siku. Lakini unapaswa uwe na kompyuta. wasiliana nami kimwerihps@yahoo.co.uk
ReplyDeleteUnahitaji maombi!
ReplyDeleteNadhani jambo la msingi ni kufanya biashara kwa faida na mafanikio. Ukitaka kuchunguza kila mwenendo nadhani utajikuta unalazimika kuuza mwenyewe. Siri kubwa ni hii, wauzaji huongeza bei ya bidhaa na huweka kumbukumbu za mauzo kwa kuonyesha viwango mlivyokubaliana kwa kila bidhaa nakuweka mfukoni ile ziada. Kwa jinsi hiyo, wao pia hupata fursa ya kuendesha maisha yao pasipo kuathiri biashara yako. Kununua biadhaa zinazofananana na zako kwa weza kutokea lakini ni rahisi kutambua kuwa bidhaa ina doda.Wengi hawatumii njia hii maana wanajua kuwa italazimu mwenye biashara kuanza kulipa mishahara kutoka mfukoni badala ya mradi kuji-sustain.
ReplyDeleteIkiwa mtu anambinu za kupata mapato ya ziada pasipo kuathiri matarajio yako ni bora kuliko atakaye kula moja kwa moja kilichopo, maana hatimaye kitaisha.
Mimi pia nilikuwa kwenye same situation ka wewe, Nami nlihisi hivyo hivyo naibiwa. Wateja wananunua vitu na nina uhakika ila mauzo hafif. Mi nlimsimamisha kazi mfanyakazi nkamuomba wife asimamie kwa mwezi. The truth is Sales improved ka mara 3 ya nliyokuwa napata baada ya mwezi. Ila wa kwanza alikuwa anaiba na sijui ilikuwaje nlikuwa sijui hata baada ya kuchukua stock. Wife likizo imeisha nimeuweka mwingine Huyu mauzo yamekuwa mabaya kuliko hata yule wa mwanzo sijui nifanyaje???????
ReplyDelete