Mpendwa kaka Michuzi na wadau wote wa blog. Kama nilivyoelezea hapo juu, nina mpwa wangu ambaye amepotelea katika makundi mabaya. Tumefanya kila njia ya kumsaidia ili aondokane na matatizo haya lakini mpaka sasa hatujafanikiwa na ndiyo maana nimeona nijaribu njia ya mwisho kupitia kwako au kwa wadau ili wanisaidie kama wanafahamu institution yoyote Dar au nje ya Dar inayo wasidia vijana wetu kuepukana na ulevi.

Mpwa wangu huyu amekulia katika mazingira yenye heshima kijijini na alikuwa anapendwa na watu wote. Hata mpaka leo mbali ya ullevi, bado ana tabia nzuri ya kuwaheshimu wakubwa siyo kwenye family tu, hata majirani. Anajaribu kufanya vibarua mbali mbali na wala hachagui kazi, lakini akipata pesa yote inaishia kwenye pombe kiasi kwamba hawezi kufanya chochote cha maana katika maisha yake.

Family imejaribu kila njia ili aepukane na tibia hii mbaya lakini imeshindikana. Anaonyesha nia ya kuacha, tukiongea naye anasikiliza na anakili kwamba ana matatizo na ataacha pombe. Inaweza kuchukua kama week mbili bila kulewa lakini ghafla anaanza tena. Hapo tena anakuwa hajitambue kabisa.

Tatizo naona liko kwenye mazingira anayoishi na marafiki alionao. Akikutana nao wanamshawishi anywe kidogo kisha anarudi pale pale. Mimi naishi nje nimeishaona jinsi watu wa Ulaya wanavyosaidiwa kuachana na ulevi lakini kupitia kwa wataalamu, na kufungiwa mahali ambapo hawawezi kupata pombe au kukutana na walevi wenzao. Mara ya mwisho nilipokuwa nyumbani (Dar) nilisikia kuwa kuna kituo kimoja Kinondoni kinachowasaidia vijana kama hawa.

TADHALI SANA KAKA MICHUZI NA WADAU KAMA MNAFAHAMU WAPI HIKI KITUO KILIPO AU MAHALI POPOTE TANZANIA NAOMBA SANA UNIJULISHE KUSUDI NIMOKOE MPWA WANGU KABLA HAJAISHIA PABAYA.

NATANGULIZA SHUKURANI ZANGU KWENU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2011

    kwanza pole sana na kweli ni tatizo kwa kijana na inauma sana ila nakushauri ufuatilie kwa zanzibar kwani najuwa ipo sehemu wanakuwa wanafungiwa watu kama hao ila sijui iko wapi

    chakufanya sasa liweke jili tangazo kwenye web ambayo inatembelewa sana na wazanzibar pengine atatokea mmoja wao anakujuwa na atakupa contact zake ingia www.mzalendo.net

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2011

    Jamani na mimi naomba msaada wa kumsaidia ndugu yangu mwenye PEPO LA WIZI......Nianzie wapi jamani kwani naona hata jela hakusaidii kitu.

    ReplyDelete
  3. Mdau kwanza pole sana kwa tatizo la mpwa wako. ila mi kuna jamaa yangu ambaye amekuwa na tatizo lake lakini familia yake iliweza kutafuta kituo kimoja kiko mbarara uganda na ndo ikampeleka huko nasikia kituo hicho kiko chini ya mapadre wakatoliki na ni kizuri nikipata jina lake basi ntakutumia mara moja.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2011

    Pole ndugu, mpeleke Lutindi mental rehabilitation centre, ipo korogwe tanga ni ya kanisa la KKKT ila inaongozwa na wajerumani, google lutindi mental hospital utapata details , mbali ya kupata matibabu wanafundishwa kazi za mikono kama vile kuseketa mikeka na carpets n.kPole ndugu, mpeleke Lutindi mental rehabilitation centre, ipo korogwe tanga ni ya kanisa la KKKT ila inaongozwa na wajerumani, google lutindi mental hospital utapata details , mbali ya kupata matibabu wanafundishwa kazi za mikono kama vile kuseketa mikeka na carpets n.k

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 29, 2011

    Suleiman Mauly sober house Zanzibar....0782000426. Lakini hii sober house, wanashughulikia watu wanaotumia madawa ya kulevya...hebu ulizia hii ya Uganda.
    Mdau Zenji

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 29, 2011

    Issue hapo ni kumtenganisha na hayo mazingira tu. Kama kijana ni msikivu na anaweza mwenyewe kuacha pombe mpaka wiki mbili zikapita, sioni haja ya kumtafutia kituo maalum. Mtafutieni shughuli maalumu mbali na hao marafiki uchwara, kisha mumpe ushirikiano wa karibu ili shuguli yake ifanikiwe. Ushiriki katika masuala ya kidini unaweza kumsaidia pia.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 29, 2011

    Nikusaidie Kaka Kwa kutatua tatizo la mpwao, nikweli Zanzibar kipo kituo cha aina hiyo maeneno ya Tomondo Mjini magharibi na kinaendeshwa kijana Suleiman aliyeachana kabisa na madawa ya kulevya. Kwakweli kinapata support kupitia miradi ya afya na ofisi ya makao wa rais (VP1). Lakini hiki kituo kinadili zaidi na waathirika wa madawa ya kulevya, lakini kwa tatizo la mpwao ni ulevi wa pombe kwahivyo sina taarifa za kutosha kwa tatizo hilo.
    Jaribu kutafuta kituo hiki ili upate maelezo zaidi M/Mungu atakusaidia.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 29, 2011

    Kuna dawa ya kienyeji anapewa na kunywa. Kila akigusa glasi yenye pombe anasikia kutaka kutapika. Hivyo pombe inakuwa adui yake. Baada ya hapo anaacha kabisa kutokana na kuhofia kutapika.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 29, 2011

    Mtu mzima anapojiingiza kwenye upumbavu wakati akijua ni kitu kibaya ni wa kuachwa tu. Asiwanyime usingizi. Kazi yenu ilshakwisha kwa kumsihi kuacha hiyo tabia na kumuonesha kuwa mnampenda lakini ameendelea kunywa mipombe. Mwacheni afanye atakavyo kwani kadiri mnapomhangaikia ndivyo atakavyowasumbua.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 29, 2011

    Nasikia (eti)....tafuta maziwa ya mwanamke anayenyonyesha...mtilie TONE kwenye pombe akiwa hajui.........That will be HIS LAST GLASS!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...