Bw.Naeem Gire
 --
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam,imemwachia huru Naeem Gire aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kughushi na kuwadanganya serikali kuwa mitambo ya Richmond ina uwezo wa kufua megawati 100 za umeme.
Gire ametoka kizimbani akichekelea baada ya hakimu wa mahakama hiyo, Mh. Waliarwande Lema , kutamka kuwa anamuona hana kesi ya kujibu kutokana na ushahidi uliofikishwa mahakamani na serikali  kushindwa kumridhisha ili amuone kuwa na kesi ya kujibu.

"....Baada ya kupitia ushahidi katika vipengele vyote nimeona kuwa hakuna ushahidi wa kutosha uliowasilishwa  kuridhisha kumuona mshitakiwa ana kesi ya kujibu...kesi hii ni miongoni mwa kesi kadhaa ambazo huletwa mahakamani na kisha kuitwisha lawama mahakama",alisema Hakimu  Mkazi wa Mahakama hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2011

    bongo kuna kazi saana! inabidi itawaliwe na waisrael kama miezi sita hivi!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2011

    bonge la changa la macho! ama kweli Tanzania ni chukua chako mapema!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2011

    Vipi akina nguza na mtoto wake?Hakuna lawama za mahakama?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...