Tunatangaza nafasi za masomo kwa vyuo vikuu katika nchi za Ukraine ambapo ada ya masomo ni nafuu sana na elimu ni bora
Kozi zifuatazo zinatolewa pamoja na nyingine nyingi ambazo inawezekana hatukuzitaja.
1. Medicine
2. Pharmacy
3. Stomatology
4. Dentistry
5. Paediatrics/Nursing
6. Biomedical/Chemical Engineering
7. Automobile Engineering
8. Road and highway construction engineering
9. Computer Engineering
10. Information and Technology (IT)
11. Aeronautical and aviation engineering
12. Flight, Navigation, and Piloting
13. Machinery construction Engineering
14. Mechanical & Electrical Engineering
15. Economics
16. Accounting and Business Administration
17. Tuarism and Hotels Management
18. Judiciary Laws
19. Ecology/Mining industry and Environmental Technology
20. Theatre, Music Arts
21. Agronomy
22. Oil and gas Engineering
23. Marine and Sailing etc...
Msimu wa masomo unaanza Tarehe 01 September ya Kila mwaka.
wahi ujisajili kwa nafasi bora, rahisi na nafuu.
Tangazo hili limetolewa na Dasprom Company (T) LTD na Scholarship Agency
MAWASILIANO
+255788269951
+255717020866
+255767494907 Zote Tanzania...
Adress Ukraine
Tel: +380935348972
web adress: www.scholarshipp.com.
au
--
huuu ni utapeli tuuu yaani mpaka leo 2011 bado mnawafanya watu wajinga,kila kitu kipo kwenye net kwa nini m2 afanye usaji kwa kupitia kwako?we ndo nani?ujinga huuuu,mimi nimekuja kusoma ulaya bila kusaji kwa m2 yeyote bali ni kujisajili kwenye website husika.
ReplyDeletemaoni yangu kwa watanzani ni kuwa makini na matapeli kama hawa bali ni muhimu kufatilia mwenyewe.
ni hayo tuuuu
Niko Ukraine kimasomo.Tafadhali muwajulishe hali halisi ya kimaisha hapa kuliko kuwaleta hapa na kuwatia wazazi wao hasara.Hakuna kazi, maisha ni ghali, Baadhi ya ufundishaji mzuri lakini katika sehemu nyingine ni ovyo.Tfadhalini fanyeni utafiti kabla ya kuja Ukraine.
ReplyDeletemshikaji hapo juu umeropoka bila kuchunguza maoni yako yana value gani..mimi pia nimeweza kuja huku kwa kupitia agency kama hizi na watu binafsi..nimefanikiwa kwa kupitia makulilo ambaye ana dili na ishu kama hizi za kuwasaidia watu wakasome usiwakatishe tamaa jamaa kwani akili zao ndo zitaamua kuwa ni matapeli au la
ReplyDeleteWadau nadhanani huu si ubishani na kunadi maisha ya wanafunzi haooo watarajiwa mie nimekula nondozzzz 6 huko na sasa niko home..ki shule ni pazuri sana hakuna vishawishi vya kazi na wala usiote kufanya kazi,ila kubaliana na haya ubaguzi,maisha magumu,na hali ya hewa ni baridi katika msimu wa baridi,Unaweza soma iwapo utakuwa na source ya hela nzuri kwa kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki kila mwisho wa mwezi at least 300usd,na pia unaweza bahatika soma kwa lugha ya kirusi,kiukraine,kingereza..shule ipo sana tu.Mkizingatia hayo mnaweza kuja ila usiweke maisha kama bahati nasibu hapo hakuna hii karata ni nyeusi au nyekundu tu.Kuwa makini na maisha yako.Mtu kwao kuinusuru nchi yake niko home napunga upepo baada ya nondoozzz 6 katika level ya masters mambo ya Cybernetics.
ReplyDeleteuje kwa kupitia agent au mwenyewe cha muhimu ni kufanya utafiti juu ya sehemu unayotaka kwenda...tatizo la ma agent wengi wanaweza kukupamba kwa maneno mazuri bila kukuonyesha kwamba huko uendako kuna tatizo A B C wao wakipeleka wanafunzi kwenye chuo fulani kuna hela wanalipwa so usiwaamin mia kwa mia bali fanya utafiti binafsi na kama unaweza apply direct kwenye chuo husika,...mimi nipo UK mwanzoni nili apply kupitia agency fulani ipo dar wakawa wananing'ang'aniza kunipeleka vyuo wanavyopata faida kubwa wao walivoona sikubaliani nao wakazusha mada mpya kuwa hicho chuo ninachokitaka inabidi nisome pre masters kwa pound 5000 kwenye ka college gani sijui then ndio nije tena kulipa ada ya masters yenyewe kwenye chuo ninachokitaka nikaona hawa wasanii nika apply direct kwenye chuo husika nikapata na nimeanza masters moja kwa moja ,,nimeokoa pound 5000 kwa kufanya utafiti binafsi ..kwa hiyo ndugu zanguni fanyeni utafiti ma agent sio wa kuamini sana ingawa wanasaidia kwa kiasi fulani...
ReplyDeletejamani kwani google na w.w.w kazi yake ni nini?usiwe mwoga kutafuta masomo au maisha,jiamini,wengi wetu hatujiamini, tumia mda kufanya uchunguzi wa kila unalotaka-utaokoa pesa yako
ReplyDeleteKwa mtu ambaye yupo serious anataka kusoma, ni kweli akija huku atafanikiwa, kuhusu maagent mi wala sijui maana mi nilipitia katika post za serikali, kitu kingine wala nisiwadanganye maisha ni magumu tena sana kwa wanafunzi huku si sawa na nchi nyingine ambazo waweza soma na kufanya kazi huku kazi ni kama hamna na hata kama zipo ukifanya basi ujue mahudhulio yako shuleni yatakupelekea kufeli mitihani maana ratiba ipo tight sana na shule ni ngumu sana. Kikubwa sana ni ugumu wa maisha yaani kila kitu ni gharama unatakiwa minimum uwe na 500-700 kwa mwenzi katika kulipia bweni, chakula, nauli, vitabu na mambo mengine. So kama wajiweza karibu sana
ReplyDeleteMdau Moscow-Russia
Kweli nchi hizi kwa kusoma ni nzuri ila jihadhalini na maagent na nisingemshauli mtu atafute chuo kupitia internet maana huko wamejaa matapeli wa kihindi na kipakistani kwa kugeuza website za vyuo kuwa zao,hivyo waweza kuwa unadhani unawasiliana na chuo kumbe ni mhindi au mpakistani tapeli ambapo huchukuwa pesa nyingi. Ushauli wangu kwa wanafunzi wanaotaka kuja kusoma nchi hizi ni vizuri kuwasiliana na Ubalozi wetu Moscow nchini Urusi hapo unaweza kupewa watu husika wanaoweza kukusaidia kupata nafasi ktk vyuo bila kutapeliwa na utakuwa na uhakika wa kupata maelezo kamili na mazuri kuhusu vyuo vikuu Urusi na Ukraine.
ReplyDeleteKAMA UNATAKA KUSOMA, SHULE IPO. KAMA UNAKUJA KUSOMA NA KUFANYA KAZI, KAA HOME, HAKUNA KAZI.
ReplyDeleteKama uko Tz kwa nini usiende kwenye ubalozi husika ukapata habari za vyuo vya huko?Kila ubalozi kuna kitengo cha habari za nchini husika.Mfano UK utapata habari pale British Council, etc
ReplyDelete