Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete Jumatatu tarehe 25/07/2011 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya kumbukumbu ya Mashujaa itaayofanyika kitaifa Naliendele, Mtwara.

Kwa mujibu wa ratiba ya Maadhimisho iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Rais akiwa katika uwanja wa kumbukumbu ya mashujaa wa Naliendele, atawaongoza viongozi wenzake kuweka silaha za asili katika mnara wa mashujaa.

Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Rais ataweka Mkuki na ngao, wakati Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama ataweka sime. Kiongozi wa Mabalozi nchini ataweka shada la maua, Meya wa Manispaa ya Mtwara- Mikindani ataweka upinde na mishale na Mwenyekiti wa Tanzania Legion ataweka shoka.

Baada ya tukio hilo, kutakuwepo na sala kutoka kwa viongozi wa dini akiwemo Sheikh kwa niaba ya Waislam, Mchungaji kwa niaba ya C.C.T na Padre kwa niaba ya Roman Catholic.

Aidha gwaride la majeshi ya ulinzi na usalama litatoa heshima kwa Mhe. Rais na kupiga wimbo wa Taifa kabla ya Rais Kikwete kutembelea makaburi na nyumba ya makumbusho ya Naliendele.

Sherehe hizo zinazotarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...