Wazalendo,
Leo Jumapili tarehe 24/07 kama tulivyowataarifu awali, tulipeleka rambirambi zetu kwa familia ya marehemu Sekou Toure Mndeme.


Tumemkabidhi mjane wa marehemu Halima Mndeme risiti ya benki ya shs. 605,000/= toka TPN ambazo tuliweka kwenye akaunti ya mjane.


Pia kulikuwa na kundi jingine ambalo tuliungana nalo la marafariki wa marehemu ambao nao wamemkabidhi  risiti ya shs. 5,000,000/=, hivyo leo tumekabidhi risiti mbili za benki zenye jumla ya shs. 5,605,0000/=.

Mjane Halima Mndeme, Mama wa marehemu na kaka mkubwa wa marehemu  Abdul Sultan wanatoa shukrani nyingi sana kwa wote kwa jinsi mlivyoshiriki wakati wa msiba na baada ya msiba.


Nami kwa niaba ya TPN nawashukuru waote na naomba tuendelee kusaidiana na kushirikiana wakati wa shida na raha.


Tuendendelee kuwaombea wafiwa na Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi na awabariki wote.


Amina...!!!


Phares Magesa
Rais- TPN
More info: www.tpntz.org

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...