Shindano la kumtafuta Mrembo wa Kanda ya Ilala linafikia kilele ijumaa wakati Walimbwende kumi na saba watakapo panda jukwaani kumenyana wakishindania Taji la Redds Miss Ilala ikiwa ni kwenye mchakato wa kuelekea kumpata Mrembo wa Tanzania.
Kila kitu kiko tayari kwa ajili ya Mashindano haya ambayo yatafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja. Warembo wamekamilika, maandalizi yote yako sawa sawa ikiwa ni kubadilisha kabisa maandhali ya viwanja vya Mnazi mmoja kutoka katika hali ya kuwa vya mikutano ya hadhara na kuwa katika hali ya viwanja vya starehe na burudani.
Michoro ya jinsi viwanja vitavyo onekana imetokana na Taman min Indonesia park iliyoko katika jiji la Jakarta na tunategemea kuwa kila atakayefika mahala pale atapata burdani tosha na kumfanya kuweka shindano la mrembo wa Ilala mwaka huu kuwa kumbukumbu kwake.
Bendi ya African Stars Twanga Pepeta itaanza kutumbuiza kuanzia saa moja kamili jioni na kutoa burdani kwa watu watakaokuwa wanaingia uwanjani hapo. Burdani pia itaporomoshwa na Mwanamuziki wa ngoma za asili Wanne Star na Warembo walioingia fainali katika Shindano la Vipaji.
Zawadi zitakazo tolewa kwa warembo ni kama ifuatavyo:
1. Redds Miss Ilala atapata Tshs 1,500,000/=
2. First Runner Up atapata Tshs 1,000,000/=
3. Second Runner Up atapata Tshs 850,000/=
Hawa watapata pia tiketi ya kuwakilisha Miss Ilala katika shindano la Vodacom Miss Tanzania.
4. Third Runner Up atapata Tshs, 500,000/=
5. Fourth Runner Up atapata Tshs. 500,000/=
6. Kifuta Jasho kila mmoja atapata Tshs 200,000/=
Shindano la mwaka huu la Miss ilala lilikuwa na pilika pilika nyingi ambazo si za kawaida ikiwa ni pamoja na kufanya ziara ya kimafunzo na utalii katika majiji ya Nairobi na Arusha. Kama ambavyo Miss Ilala imekuwa ikiweka rekodi katika mambo mbali mbali katika urembo mwaka huu tumeweka rekodi ya kuwapeleka warembo nje ya nchi kwa mafunzo na kuongeza ufahamu wao.
Warembo watakaoshiriki shindano kesho ni
1. Augostina Wilhad Mshanga
2. Jenifer Jonathan Kakolaki
3. Lilian William Makanza
4. Priscilla Adolf Mchemwa
5. Nasra Salim Ishebabi
6. Williet Wilson Rwechungula
7. Diana John Zakaria
8. Meryvine Peter Nkenzia
9. Godriver Bahaye Mashamba
10. Edna Gesura Mnada
11. Salha Isreal Kifai
12. Alexia William Rwabitara
13. Ritha Cuthbert Mvungi
14. Mariam Shabaan Manyanya
15. Lilian Paul Ibrahim
16. Mara John Mrema
17. Faizal
Mashindano ya Redds Miss Ilala 2011 yamedhaminiwa na Redds Original, Vodacom Tanzania, Paradise City hotel, Michuzi blogspot, Habari leo na dailynews, Paris Pub, Maisha Club, Fabak Fashion, Channel Ten, TV Sibuka, 88.4 Clouds FM, Syscorp Group, Mariedo Boutique na Papazi entertainment.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...