Mwenyekiti wa CCM, Rais Dr.Jakaya Kikwete akiwapungia mamia ya wanachama wa CCM waliohudhuria maadhimisho ya kuzaliwa Chama Cha TANU zilizofanyika katika  Makao Makuu ya CCM na baadaye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam jana usiku . Shoto ni Mama Salma Kikwete.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dr.Jakaya Mrisho kikwete akiteta jambo na Katibu Uenezi na Itikadi CCM Nape Moses Nnauye wakati wa sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Chama Cha TANU zilizofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam jana usiku.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kuimba wimbo maalum wa sherehe za kuzaliwa TANU pamoja na wasanii wa bendi Vijana CCM wakati wa maadhimisho ya kuzaliwa Chama cha TANU zilizofanyika katika katika viwanja vya Mnazi mmoja jana usiku jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa CCM,Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuwasha taa maalum kuashiria uzinduzi wa sherehe za kumbukumbu ya Kuzaliwa chama cha TANU mnamo mwaka 1954,zilizofanyika jana katika ofisi kuu ya CCM,Mtaa Lumumba jijini Dar es Salaam jana usiku na baadaye sherehe za mkesha katika viwanja vya mnazi mmoja.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara),Pius Msekwa (kushoto),Katibu Uenezi na Itikadi CCM Nape Nnauye (pili kushoto),Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mkama pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkowa wa Dar es salaam John Guninita. 
Mwenyekiti wa CCM,Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na muasisi wa Chama cha TANU mzee Constantine Milinga wakibonyeza kitufe maalum jana kushiria siku na saa ambapo chama cha TANU kilipozaliwa Tarehe 7 mwezi wa 7 mwaka 1954.Wengine katika picha kutoka kushoto ni katibu mwenezi CCM Taifa Nape Nnauye, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa, Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mkama.
Mwenyekiti wa CCM,Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mke wake Mama Salma Kikwete wakisalimiana na wadau mbali mbali waliohudhulia hafla hiyo iliyofanyika jana usiku kwenye viwanja vya mnazi mmoja.
Mwenyekiti wa CCM,Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mahojiano na mmoja wa waandishi wa habari  Hawla Shante waliokuwepo katika hafla hiyo.
umati mkubwa wa watu ulihudhulia katika sherehe hizo za kukumbuka kuzaliwa kwa TANU.
Kapten John Komba akiongoza safu yake katika kunogesha sherehe hizo kwa kwaya nzuri kabisa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2011

    TANU kimeshaungana na ASP sasa kinasherehekewa nini? Au kuna mpango wa kukirudisha tena?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2011

    Hivi bado tunahitaji 'mabodigadi' waliovalia hizo sare?.Mbona marais wengine wana 'mabodigadi' waliovaa kiraia hadi wanapendeza..na siyo rahisi kuwa-notice!.Serikali ilifanyie kazi hili.Michuzi usiibane hii

    David D

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 07, 2011

    Hongera wana CCM kusherekea kuzaliwa kwa chama kilichotuletea uhuru wa Tanganyika. Tuko pamoja na tuawatakia sherehe njema. Kilichobaki sasa mbele yetu ni mapambano na maadui wa taifa letu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini. Baba wa taifa alitufundisha kwamba ili tuendelee tunahitaji watu (ambao ni watanzania tupo), ardhi (ipo), siasa safi (???) na uongozi bora (???). Hivyo ni wajibu wetu sasa kuhakikisha kwamba tunayatekeleza hayo yote kwa kurekebisha siasa safi na uongozi bora kwa manufaa ya watanzania na Tanzania kwa ujumla!!
    Mdau

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 07, 2011

    Hongera TANU, Hongera CCM na Hongera JK.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2011

    mi sielewi, tunasherekeaje kitu ambacho kilikufa na kuundwa ccm, sasa na wenzetu washeherekee ASP? haya kwangu maajabu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...