Mazembe Peter Joseph Nyerere
11/7/ 1974 - 17/5/2011
Familia ya marehemu Joseph Kizurira Burito Nyerere na Ukoo wa Nyerere wanachukua nafasi hii kuwashukuru kwa dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na majirani wote walioshiriki kwa hali na mali wakati wa msiba wa mpendwa wao Mazembe ambaye Bwana alimwita katika makao ya milele tarehe 17/5/2011 na kuzikwa kijijini kwao Butiama mkoani Mara tarehe 21/5/2011.
Shukrani za kipekee ziwaeendee wafuatao, marafiki zake wapenzi (MIBS), wauguzi na wafanyakazi wa hospitali zifuatazo, TMJ, Hindu Mandal, Agha Khan ya Nairobi na Dar es Salaam, Hospitali ya Appollo ya India, na Hospitali ya Taifa Muhimbili. Pia Kanisa la Mt. Immaculata la Upanga Dar es Salaam na Kanisa Katoliki Butiama kwa utumishi wao wa kiroho.
Kwa kuwa sio rahisi kumtaja kila mmoja hapa, tunaomba mpokee shukrani zetu na kumuomba mwenyezi mungu awape neema zake baraka na kuwazidishia upendo.
Kutakuwa na misa ya kumbukumbu ya Jumamosi tarehe 9/7/2011 saa 5 asubuhi nyumbani kwa marehemu upanga, Dar es Salaam.
Wote mnakaribishwa
Poleni sana.
ReplyDeleteSiamini Mazembe??RIP.
ReplyDelete