Mwanafunzi wa Kidato nne wa Shule ya Sekondari Mzumbe ,Josephat Mafung’a ( wapili kushoto) akitoa maelezo ya vifaa vinavyounda na kufanya kazi katika Kompyuta ,mbele ya Mgeni rasmi , Kaimu Ofisa Elimu wa Mkoa wa Morogoro, MaryRose Lyimo , ( watatu kulia), wakati wa siku ya Kiingereza , Julai 23, mwaka huu, Shule 10 za Sekondari za Morogoro zilishiriki kwenye shindano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Sekondari Mzumbe.Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kilakala ya vipaji maalumu , akijenga hoja za msingi katika kutetea umuhimu wa taaluma yake ya Uandishi wa Habari mbele ya wanafunzi wenzake wakati wa siku ya Kiingereza , julai 23, mwaka huu ,Shule 10 za Sekondari za Mkoa wa Morogoro ,zilishiriki shindano hilo katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mzumbe.Umati wa wanafunzi wa shule 10 za Sekondari zilizopo Mkoa wa Morogoro pamoja na Walimu wao na wageni wengine wakiwa ndani ya ukumbi wa shule ya Sekondari Mzumbe, wakati wa siku ya Kiingereza , Julai 23, mwaka huu, wanafunzi wa shule hizo walishindanishwa mada mbalimbali zilizohusiana na masomo Walimu wa kigeni wanafundisha masomo mbalimbali katika Shule ya Sekondari za Serikali , Mkoani Morogoro wakijumuika na walimu wenzao na wanafunzi wa shule 10 za Morogoro , wakati wa siku ya Kiingereza iliyofanyika Julai 23, mwaka huu, mada mbalimbali zilishindaniwa na wanafunzi hao katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mzumbe.Mwanafunzi wa Kidato cha sita mchepuo wa HGL wa Shule ya Sekondari Morogoro , Da' Gwantwa Atilio ,akinogesha muziki mbele ya wanafunzi wenzake na waalimu siku ya Kiingereza Julai 23, mwaka huu ambayo hushindanisha mada za masomo mbalimbali, Shule 10 za Sekondari za Mkoa wa Morogoro ,zilishiriki shindano hilo kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mzumbe, Wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro. Picha na habari na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro
Home
Unlabelled
SIKU YA KIINGEREZA KWA WAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI ZA MKOA WA MOROGORO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...