Mshambuliaji wa timu ya Simba,Ulimboka Mwakingwe (kulia) akitajaribu kumtoka beki wa timu ya Red Sea ya Eritria,Flimon Tsegay katika mchezo wa mashindano ya Kagame-Castle Cup uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa.hadi mwisho wa mchezo si Simba wala Red Sea walioweza kuona lango la mwenzake na kufanya matokeo kuwa 0-0.
 Nassor Chollo wa Simba (kulia) akitaka kumtoka beki wa Red Sea ya Eritrea katika mchezo uliopigwa jioni ya leo wa kukamilisha hatua ya mzunguko.hadi mwisho wa mchezo Simba 0-0 Red Sea.
 Mshambuliaji wa Simba.Mussa Hassan Mgosi,akiwa na mpira huku Beki wa timu ya Red Sea akitaka kujaribu kumzuia bila mafanikio.
 Beki wa timu ya Red Sea ya Eritria,Flimon Tsegay (katikati) akimzuia mshambuliaji wa timu ya Simba,Rajab Isihaka (kulia) huku kipa wa timu hiyo ya Red Sea,Daniel Goitom akiangalia.
 Mashabiki wa timu ya Simba wakiishangilia timu yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2011

    Katika mwaka ambao Simba tumeboronga katika usajili ni mwaka huu! Sijui viongozi wetu wana malengo gani na timu! Kwa mtazamo wangu, sidhani kama CHUJI, na ULIMBOKA ni mbadala sahihi wa SAMATTA na OCHAN. Nasikia pia wanafanya mazungumzo na VICTOR COSTA! Mambo mengine ni ya ajabu kweli! Hivi wachezaji makinda wote hao tulionao nchini, kuna haja gani ya kusajili wachezaji ambao wameshacheza ligi kuu zaidi ya miaka mitano! Wanasaikolojia katika masuala ya soka wanasema unapocheza soka kwa muda mrefu, hamu ya mafanikio hupungua. Na mbaya zaidi baadhi ya wachezaji hao nidhamu yao ni mbovu. Na hili limethibitishwa na makocha zaidi ya mmoja. Tunaomba viongozi muangalie upya suala la usajili kabla dirisha halijafungwa. Nimekuwa nikihudhuria michezo ya Kagame, sioni chochote timu inachofanya. Tulitakiwa tufanye vizuri zaidi ya sasa kwa sababu mashindano haya yamekuja wakati tumetoka kushiriki michuano ya CAF. Mpaka sasa wachezaji ambao kwa mtazamo wangu naona wanauwezo wa kuichezea Simba mliowasajili ni CHOLO na BOBAN, basi! Msituletee janga kama la mwaka 1988 tulipotaka kushuka daraja tukabebwa na watani.

    ReplyDelete
  2. MATANGALUJuly 04, 2011

    "WEKUNDU WA TERMINAL MWANZO MWISHO"

    Hivi hayo maneno maana yake ni nini? Maana sijaelewa chochote hapo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 05, 2011

    Hata Boniface Pawasa pia anakuja, poor Simba. Tatizo ni kwamba waliouza wachezaji ni watu binafsi na hela wametia mifukoni mwao. Club haina mchezaji wala hela ya usajili hivyo wanawarudisha wazawa ili waokoe jahazi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...