![]() |
Naibu Waziri Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Lazaro Nyalandu |
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
SERIKALI imesema kwamba suala la kubatilisha hatimiliki za mashamba ya mkonge yaliyopo mkoani Tanga na kuwagawia wananchi kama ilivyo ahadi ya Rais Jakaya Kikwete litafanywa baada ya taratibu za kisheria na mfumo mahususi utakaotumika kukamilisha azma hiyo.
Hayo yalisemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Lazaro Nyalandu wakati akijibu swali la kwanza la Mbunge wa Viti Maalum(CUF),Amina Mohamed Mwidau lililokuwa linauliza kuwa utaratibu wa kuwagawia wananchi mashamba hayo utaanza lini.
Akijibu swali hilo , Naibu Waziri huyo alisema katika kutekeleza azma hiyo Wizara ya Kilimo ,Chakula na Ushirika imeanza mchakato huo wa kuyafuatilia mashamba yote ya mkonge yaliyotekelezwa kwa kushirikiana na bodi ya mkonge.
Aliongeza kuwa tayari imebainika kwamba mshamba mengi ya mkonge yamevamiwa kiholela na kutumiwa kwa kilimo cha mazao mchanganyiko.
Akijibu swali la pili la mbunge huyo, lililouliza kuwa je ni mkakati gani utatumika kuhakikisha kuwa mji wa Tanga unakuwa mji wa viwanda zaidi ilivyo kuwa zamani.
Naibu Waziri huyo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na uongozi wa mji wa Tanga wametenga eneo lenye ukubwa wa hekta 1,363 katika kata ya Tangasisi kwa ajili ya ya uwekezaji wa viwanda vinavyolenga maeneo maalum kwa mauzo nje na maalum ya kiuchumi(EPZ/SEZ).
Waziri Nyalandu aliongeza kuwa eneo hilo litawekewa miundombinu ya msingi kama vile maji, umeme, barabara, mfumo wa maji taka ili kuwahasisha wawekezaji wa ndani na nje ya kujenga viwanda mbalimbali hususan viwanda vya kuongeza thamani mzao ya kilimo, madini, kusindika nyama, maziwa na vinginevyo.
Alisema uwepo wa eneo lenye miundombinu ya msingi kutavutia wawekezaji wengi hivyo kuufanya mji huo kuwa na viwanda vingi kuliko ilivyokuwa awali.
Aidha alisema wizara yake kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) imepata eneo jingine lenye ukubwa wa hekta 50 katika eneola Kange ambalo kwa kushirikiana na wawekezaji wa ndani na nje litaanzisha eneo la viwanda kwa ajili ya miradi mbalimbali.
Aliongeza kuwa michoro muhimu ya kuonyesha matumizi ya ardhi na mipaka yha mkandarasi wa kujenga miundombinu ya umeme na maji katika eneo hilo unafanywa nia ni kuwavutia wawekezaji na kuhakikisha kuwa uwekezaji unaanza kabla ya mwishoni mwa mwaka 2011.
Michuzi tuwekee Breaking News za Rostam Aziz kujivua Gamba kwa kujiuzulu ubunge na kwenye NEC.
ReplyDelete