Kampuni ya umeme Tanzania (Tanesco) imetoa mikakati yake juu ya uboreshaji wa umeme nchini ili kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Afisa Mchambuzi wa Maswala ya Fedha wa kampuni hiyo ndugu Mathew Maduhu katika maadhimisho yanayoendelea ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika viwanja vya Mnazi mmoja.

Bwana Maduhu amesema mikakati hiyo ni ile ya muda mfupi ya kati na ile ya muda mrefu,ambapo mikakati ya muda mfupi ni ujenzi wa mitambo ya MW 100 Ubungo jijini Dar es salaam ambao utakuwa unatumia gesi asili,

Alitaja mipango mingine ni pamoja na ujenzi wa mitambo ya MW 60 eneo la Nyakato mkoani Mwanza na kununua umeme wa kampuni ya Symbion Power wenye uwezo wa MW 100.

Mikakati mingine ni pamoja na mradi wa Kinyerezi wa MW 240 unatumia gesi ya asili , Mradi wa Kiwira wa MW 200 ambao unatumia makaa ya mawe na mradi wa umeme wa Singida wa MW 50 unaotumia nguvu ya upepo.

Aidha Bwana Maduhu ametaja baadhi ya mikakati ya muda mrefu kuwa ni ile ya mradi wa Songwe Mbeya wa MW 650 unaotumia joto ardhi ,mradi wa Mchuchuma wa MW 600 unaotumia makaa ya mawe na miradi ya Ngaku wa MW 400 unaotumia makaa ya mawe.

Naye Mjiolojia Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini ndugu Habass Ng’ulilapi ameeleza kuwa utekelezaji wa mkakati huuo unahitaji fedha za kutosha hadi ukamilike , na kuisisitiza serikali itupie macho suala hilo ili kufanikisha mkakati huo.

Aidha bwana Habass amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia wananchi kuepukana na adha ya tatizo la umeme nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2011

    Mheshimiwa Rais, tunaomba mwezi mtukufu wa Ramadhan na siku za Eid na Krismas tunaomba umeme wa nguvu bila ya mgao, angalau tupate ladha ya Uhuru wetu wa miaka 50. Hongera kwa miaka 50 ya Uhuru.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2011

    TANGU MWALIMU RAISI WA NCHI HII MIPANGO YA MUDA MREFU WA KATI NA MREFU WA TANESCO IMETANGAZWA NA KURUDIWA KTANGAZWA.

    TUMECHOKA NA MANENO NA MIGAO

    TUNATAKA VITENDO

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2011

    huyo afisa ni mtu mdogo sana kauli yake haiwezi kupewa uzito wowote. tunataka kauli ya rais, waziri , naibu waziri au katibu mkuu. kauli za maafisa ni usanii tu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2011

    Waheshimiwa Tanesco, mtakapomaliza mikakati ndio mje na majibu. Tumekuwa tukisikia mikakati na huu ni mwaka wa 50, mje na vitendo sasa shaaa!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2011

    HII MIKAKATI INAENDELEA TU KUTANGAZWA, UKIJUMLISHA MIRADI YOTE HIYO ALIYOITAJA BWANA AFISA, UTADHANI SASA TZ INAINGIA KIPINDI CHA NEEMA. TUMECHOKA NA MIPANGO YENU YA MAKABATINI, TUNATAKA MTUELEZE HIYO MIPANGO ITAANZA LINI NA MKO HATUA GANI, SIYO MNAONGELEA MIPANGO TU. TZ TUNASIFIKA KWA MIPANGO MIZURI KILA MAHALI ISIPOKUWA UTEKELEZAJI WAKE HUWA NI SIFURI. HAYO YOTE ALIYOYASEMA AFISA MIMI NAONA NI MANENO MANENO TU TULIYOYAZOEA KUSIKIA. ACHENI KUTUPUMBAZA NA SIASA ZENU, TUNATAKA VITENDO. KUTAJA TU HAPO HIZO MEGAWATI-NAONA TAYARI NI MABILIONI YA HELA, SASA TZ HIZO HELA ZIKO WAPI? ZINAENDA KWA MAFISADI TU. HAKUNA KITU, TUNATAKA VIONGOZI WENYE KUJITOLEA KUTUMIKIA WANANCHI NA WENYE USHUJAA, NDIPO TUTAANZA KUONA HARUFU YA MAENDELEO.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2011

    Hii mikakati ilikua inasubiri mpaka bajeti ya wizara husika ikataliwe? Wizi mtupu!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2011

    Maskini Tanzania, hata wataalamu wetu wanakuwa wanasiasa hatuwezi kuwaamini. Tungojee tu kudra za mwenyezi Mungu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2011

    WATAALAAM WOTE MNABABAISHIA TUUU, UWEZO HAMNA ILA KAZI MNAING'ANG'ANIA TUUUU.

    1. MBONA NI RAHISI SANA. MUWEKE BWAWA KUBWA KABLA YA MTELA ILI MAJI MENGI YAKAE MUWE MNAFUNGUA MAGETI TARATIBU SIO MNAACHA MAJI YANAENDA BAHARINI TUU.

    2 PLANT YA KIHANS PROJECT ILIKUWA NA TABAN TATU MBILI ZILIKUWA FOR FUTURE WAZUNGU WALIWEKA NAFASI YA KUONGEZEA MBONA SIONI MAELEZO YAKE AU MMESAHAU MNAFIKIRIA MIPANGO YA MBAALI NYIE VIPI? MPAKA 2015 TABAN 2 ZIONGEZEWE SPACE IPO ILIACHWA WAZI VP WATAALAM IMEFANYIKA

    3. MZUIE BALB ZISIZO NA WATT KUBWA KUTUMIKA KTK KUTAKA MWANGA WA NDANI.

    4. MNAMATUMIZI MAKUBWA MNO NDIO MAANA HAMNA MUDA WA KUJUA BIASHARA YENU IENDE VP MATUMIZI MAKUBWA KULIKO MMNACHOKIPATA. CHARGE YA KUWEKA UMEME WIZI MTUPU UMEME WENYEWE UTAPELI TUU. CHUO CHA KIDATU MMEFUNGA VISHOKA NDIO WANAOUNGANISHIA WATU UMEME, HAMUELIMISHI WATU JINSI YA KUTUMIA UMEME, UELEWA MDOGO OVYO SANA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...