Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dr. Asha Rose Migiro akiwa katika mahojiano na Mtangazaji wa Kiongozi wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa,Bi. Flora Nducha.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dr. Asha Rose Migiro akiwa katika picha ya pamoja na Mtangazaji Flora Nducha.
Umoja wa Mataifa umesema utaendelea kulisaidia bara la Afrika kutimiza malengo ya kulijenga vyema taifa la kesho ambalo ni vijana. Kauli hiyo imetolewa mbele ya wakuu wan chi na serikali za Umoja wa Afrika wanaokutana mjini Malabo Equatorial Guinea kwa mkutano wa sikuu mbili unaomalizika Julai Mosi .
Mada kuu ya mkutano imekuwa ni kuwawezesha vijana kwa ajili ya maendeleo stahimilivu au endelevu, lakini suala la Libya na mengine ya amani na usalama yamechukua nafasi kubwa katika mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro ndiye aliyebeba bendera ya Umoja wa Mataifa na ujumbe maalumu unaojumuisha nia ya Umoja wa Mataifa kuendelea kuisaidia Sudan Kusini na kusaidia juhudi za Umoja wa Afrika kupata sluhisho nchini Libya, lakini kubwa zaidi ni ujumbe wa kuwawezesha vijana wa Afrika katika kuchagiza maendeleo kama alivyomweleza mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha.
Kusikiliza mahojiano haya maalumu bofya
AU
AU
AU moja kwa moja kwenye mahojiano yenyewe
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...