Baadhi ya wanachunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (U-DOM) wakiwa wamepanga foleni ya kuchukua fomu za kiapo cha kutofanya mgomo wa aina yoyote na kufanyiwa usaili pamoja na kupatiwa vitambulisho ili waweze kurudi chuoni na kuendelea na masomo.shughuli hiyo inaendelea kufanyika hivi sasa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
 Wanafunzi wa U-Dom wakiendelea kupanga foleni kwa maafisa wa chuo hicho ambao walikuwa wakipitia malipo ya wanafunzi hao na kuona kama hakuna deni lolote wanalodaiwa na baadae kupewa kitambulisho chake na kuruhusiwa kurudi chuoni kwa kujiandaa na mitihani inayotaraji kuanza kufanywa jumatatu.hali hii imekuja kutokana na hali ya vurugu na migomo kwa wanafunzi hao iliyopelekea kufukuzwa kwa wanafunzi wote na Chuo kufungwa kwa muda majuma kadhaa yaliyopita.
 Askari wa Jeshi la Polisi akiwataka wanafunzi hawa warudi katika sehemu zao ili shughuli ya usaili iweze kufanyika kwa utaratibu mzuri na amani kabisa.
 Baadhi ya Wanafuzi waliochelewa kuchukua namba ya kuingia kwenye usaili huo,wakichungulia kwenye moja ya mageti ya uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
 Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakiendelea kusubiria utaratibu wa viongozi wao leo kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Wengine waliochelewa kuchukua namba wakiwa nje ya geti kuu la kuingilia kusubiria taratibu ya viongozi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 30, 2011

    hapo serikali wanapoteza muda tu. Mgomo hauna kiapo ni njia ya kutatua matatizo yao. haitapita miezi 3 bila mgomo labda watekeleze yale ambayo wanafunzi wanataka.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2011

    Taabu kweli kweli democrasia ikowapi sasa apo eti watu wanapewa fomu ya kujaza ili wasigome tena? Hii sio demokrasia ata kidogo, kwa sababu wanafunzi wanagoma wanapoona kuwa hawasikilizwi na hakuna anae pay attention kutatuta matatizo yao.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 30, 2011

    Walala hoi mpo,maana watoto wa vigogo mnaowalalamikia hawasomi hapo,wapo ulaya na US-A tena wapo summer vacation,sisi tutabakia na migomo isiyokwisha no one care any more.
    Nenda shule elimika nawewe ujichukulie chako ktk nchi hii isiyokuwa na mwelekeo,acheni migomo(maana hakuna wa kutatua -ubinafsi umezidi). Hii migomo inawapotezea mda wa kuwahi nafasi za kazi ktk nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...