Ankal pole na kazi.

Leo mimi ningependa kutoa ushari kwaa wale wakina Mama waliokatika ndoa, ambao wanawakatalia waume zao kupata chakula ya usiku  kwa kisingizio kuwa wamechoka.

Naomba waache kabisa tabia hiyo maana wajue kabisa wanahatarisha maisha yao. Maana mwanaume anaponyimwa mlo huo  kila mara kwa kisingizio cha kuchoka au kinginecho, basi huamua kutafuta mama ntilie ambako huko akinogewa huacha kutumia 'dawa ya penzi', matokeo yake anajikuta analeta maambukizi ya UKIMWI nyumbani.
Hivyo kina Mama jitahidini sana kuwapa  waume zenu mapochpocho husika kila mara, kama si kila siku, na bila hiyana. Uwe Mama wa nyumbani au unafanya kazi jitahidi kutoa chakul;a ya usiku, ili kuokoa familia zenu. Kama mume wako anapendelea sinai mbili kwa wiki, au tatu au nne, basi jitahidi kwenda na mdundo ili kuokoa familia, la sivyoo familia nyingi sana zitaangamia.
Asante Ankal, ya kwangu leo ni hayo tuu.
Anti Yako

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2011

    na akina baba tunaomba mtoe chakula cha kutosha. maana hizo robo kilo siye hatushibi ndo maana tunaamua kusema tumechoka. akina baba jitahidini kuweka spice na ndimu kwa wingi kwenye hicho chakula ili kiweze kuwa kitamu zaidi siyo mambo ya mchemsho tu. vile vile akina baba tunaomba muache matumizi ya kutosha kukisafisha hicho chakula, siyo unaacha shilling 10 halafu unategemea chakula mezani kila siku. least but not last, akina baba jifunzeni kusaidia kazi za ndani kupunguza machovu ya sie a akina mama

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2011

    kwani akina baba wenyewe wanatakiwa kula tu hawatakiwi kutoa chakula? haya ndo tunaita mawazo ya mwaka 47!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2011

    Haswaaaaa, wanawake wanaofanya kazi hasa kwenye maofisi wanajidai kuwa wamechoshwa sana na kazi za ofisini hivyo unaambiwa chakula ya usiku utapata alfajiri wakati anataka kuanza kujiandaa kwenda kazini. Hilo nadhani huwa sio sahihi maana ukiwa na njaa na chakula kipo kwa nini usile? Unapangiwa bujeti ya chakula??????????? Hii inaweza kuhatarisha ndoa

    Mdau

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2011

    Aunt, naona unawasihi kina mama kana kwamba ni wajibu tu kwao kutoa chakula ya Usiku, kana kwamba wao huwa hawali. Nadhani hii inatokana na ukweli kwamba baadhi ya wanaume hudai chakula ya usiku bila kushiriki katika maandalizi ya hicho chakula. Matokeo yake ni kwamba Mwanamke anakuwa hashiriki ipasavyo kula pamoja na mumewe hivyo suala zima la chakula cha usiku kuwa usumbufu tu kwake. Ninakuhakikishia, mwanaume akishiriki katika maandalizi na kisha kujinafasi mkilishana mezani kwenu, basi hakutakuwa na issue za 'nimechoka'. Ukitia timu nyumbani tu utasikia 'Nikuandalie Chakula Mume Wangu?'

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 29, 2011

    Kusema kweli, sijawahi kusoma utumbo ktk blog hii kama huu wa leo. Nasubiri nione wengine watasemaje. Na natumaini Ankali hutozuia comments!!!

    Sidhani ama kupewa kila utakapo ndio dawa ya kuukwepa Ukimwi. Kwa taarifa yako, mtu unaweza toka pata chumbani na mkeo, na muda huohuo ukienda jikoni ukatamani ya house-girl.

    Huo ni unyanyasaji wa kijinsia. Dawa ni wanaume pia kuwa na hekima. Kunyimwa usiku haitoshi kuhalalisha utoke nje ya ndoa. Pia ujue kuwa kina mama nao wanahitaji kuwa na ridhaa ya kukupa hicho "chakula" au lah. Na pia inategemea sana unavyoomba. Sio mchana kutwa umemsahau,hata sms, alafu kufika wakati wa kulala ndio unatambua umuhimu wake. Tena kwa miguvu...!! kisa usitoke nje!!!

    Nisamehe, lakini nahisi unahitaji kuamka toka kwenye hizo zama zako za kale.

    mdau

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 29, 2011

    Kuna wanaume ambao ni wazinifu hata ukijitahidi vipi watatembea nje tu. Ndugu yangu hata ukimramba nyayo huyo jamaa ikiwa tabia yake ndiyo hiyo haiwachi. Tuombe Mungu tu atunusuru na magonjwa haya yaliyoko.

    Baadhi ya waislamu wana wake watatu ambao wamewaoa kihalali lakini bado utakuta anakwenda nje ya ndoa, huwa anatafuta nini?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 29, 2011

    Sawa je kwa wale ambao tunawapa chakula na bado anaenda kutafuta nje inakuwaje ?msaada kwa tutazz!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 29, 2011

    DU;NAONA MICHUZI HAPA NAONA WATU WANATUMIA BLOG YA JAMII VISIVYO. WATU WANAKURUPUKA NA MADA ZAO TU; NA KUJA KUANDIKA MAZAGAZAGA. KAMA MTU HANA MADA YA MAANA;NASHAURI ANGEKAA NA FAMILIA YAKE NA KUZUNGUMZIA VYUMBANI; MAANA HIZO NI MADA ZA CHUMBANI. SASA SIJUI HAPA ANAANDIKA ILI ALIYEMNYIMA HIYO CHAKULA YA USIKU AKISOMA HII MADA ATISHIKE AU?KUCHEMKA HUKO WEWE ULIYEJIITA ANTI. LABDA KITCHEN PARTY INGEKUWA MAHALA MUAFAKA PA WEWE KUPELEKA HII.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 29, 2011

    Ache usumbufu kwa wadau wa jinsia ya kike. Furaha si ya kula tu. Nenda Sinema, angalia michezo, dansi, fanya mazoezi, angalia twanga pepeta, fanya ibada, cheza karata au domino, chukua familia wakapate dinner, na mengineo. Udume sio kula kila siku bali kuangalia familia yako kwa hali na mali. Vidume wakowapi sasa, wengi wameondoka kwa huo ukimwi na kuacha familia zao kwenye majozi ya muda mrefu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 29, 2011

    Sawa na wale wenye wake wawili na bado wanakula kwa ntilie? Na wanaume wanaochoka au wenye uwezo mdogo wife nae aende kwa ntilie?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 29, 2011

    akiamua kutoka atatoka tu hata kama analishwa kila siku...

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 29, 2011

    UNAJUA KUNA KITU KIMOJA WANAUME WENGI HUWA WANAKOSEA KUHUSIANA NA SWALA LA CHAKULA CHA USIKU. HAITAKIWI UMWAMBIE MKE WAKO DIRECT KWAMBA NATAKA CHAKULA CHA SIKU. HAPO KAMA MWANAMKE ANAHISI UCHOVU MOJA KWA MOJA ATAKUAMBIA AMECHOKA.KUOMBA CHAKULA CHA USIKU KINAHITAJI UTAALAM NA HATA KAMA MWANAMKE AMECHOKA VIPI ATAKUPATIA TU.KAMA UNAHITAJI CHAKULA CHA USIKU MWANAUME KWANZA KABISA INABIDI UWE SOFT KWAKE MUONGELESHE KIULAINI NA KWA MAHABA, MFANYIE FANYIE MASAJI, UNAMBUSU MBUSU, UNAMPETI PETI SEHEM ZAKE AMBAZO UNAJUA NI SENSITIVE NK. YEYE MWENYEWE MWANAMKE ATAPATA HAMASA NA HISIA ZILIZOCHOKA ZITAAMKA NA MTAFAIDI CHAKULA CHA USIKU. YOU JUST TRY TO HAVE SOME KIND OF FUN BEFORE THEN ALL OF U WILL GET STIMULATED. MFANO MIMI PIA MWANZONI MKE WANGU ALIKUWA HAPENDELEI KULA CHA KULA CHA USIKU MARA KWA MARA, LAKINI SASA HIVI IMEFIKIA HATUA MIMI NDIO NACHOKA NA YEYE ANATAKA ALMOST THE WHOLE TIME. KWAHIYO WANAUME WAWE CREATIVE NA SIO KUOMBA CHAKULA CHA USIKU NA KUANZA KULA MOJA KWA MOJA BILA HATA MATAYARISHO YA KUNAWA MIKONO, NK. NA UKWELI NI KWAMBA KAMA MWANAMKE ANAENJOY CHAKULA CHA USIKU HAWEZI KUKATAA HATA SIKU 1 BALI WEWE MWANAUME NDIO UTASHIBA MWENYEWE KWA JINSI KITAKAVYOKUWA KINGI.
    NAWAKILISHA. This is reality.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 29, 2011

    Naona kina Mama wanatoa maoni kwa jazba. Ukweli ndio. Huo, mkijirekebisha. Mtafurahia. Matunda. Yake.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 30, 2011

    jaman aunt katoa mada nzuri sana ila kuna wapiga puli wengine wanaona kama anaandika uchafu!!najua kuna wababa wengine wana mijimama mikorofi akisema No ndo imetoka so nahisi ndo hawa wanaona kama hii mada ni utumbo wakati tunashare ideas za kuwasaidia watu waweze dumu kwenye ndoa zao.kama huna point nyamaza kuliko kuandika kuwa ni utumbo.Kwan aucle hajaiona mpaka akaiweka humu?!Mijitu mingine bana!!

    Mdau
    manchester

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 30, 2011

    Mimi nafikiri ni muhimuzaidi kama wanandoa wote wakatumia busara zao binafsi kwasababu unaweza ukawa unampa mumeo au mkeo kila siku kwa manjonjo na ujuzi wote still akakuletea magonjwa ya zinaa na ukimwi,jumlisha na watoto wa nje na vile vile akaendelea kuwa na mpango wa kando(kimada)heshima na busara ndiyo muhimu katika familia na ndoa ili baadaye kutokuja kuwaacha watoto au mwenzi mmoja wakiwa na maradhi ya kujitakia kwaajili tu ya tamaa.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 30, 2011

    wewe anonymous wa fri jul29;26;00pmni kama ukeninyanganya tonge langu mdomoni yaani kuna wanaume wakishatoka katika maulevi yao wanakuja tua basi akijisikia anakuparamia bila maandazi utafikiri gari lilikatika breki basi likapamia mti au kitu chochote hii kitu inaudhi sana hili jambo likizungumzwa kwa undani inamapana na marefu sana hii mada ni kali sana na pia haswa kwa wanawake wanaoiishi kijijini ndio balaa kabisa hawana pakusemea ni kimya na huku wanaumia sana yaani tendo la ndoa kwao ni kama adhabu haina raha kwao fikiria kijiji baadhi ya watu wengine haswa wanaume hawaajibiki katika kutafuta maisha anamwachia mama kila kitu mwanamke aende shambani kulima n mtoto mgongoni akimaliza kulima abebe kuni yakupikia chakula na ndoo ya maji na mtoto mgongoni nyumbani inaumbali bado atatembea mwendo mrefu katika jua kali au baridi inategemea na msimu akifika nyumbani aanze na kupika chakula na shuhuli zingine za nyumbani baba kuanzia asubuhi yeye yuko kilabuni akinywa mataputapu akitosheka kunywa anaenda nyumbani anajua kuna mtumwa wake baba hela ya chakula hajaacha baba kusaidia kazi nyumbani hataki akifika kutoka ulevini kitu cha kwanza kuuliza hivi leo hakuna chakula akipewa chakula ale ajuii kimetoka wapi akimaliza kubugia anaanza kumparamia mke anataka tendo la ndoa kweli huyu mwanamke atajifeel kweli au nikama msumari unapigilia katika kidonda jamani wababa mshirikiane na wake zenu kwa kila kitu huku muowa aje kuwa mtumwa wako ni mbaya sana mjirekebishe

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 30, 2011

    Wewe kama kweli ni aunt ulietoa mada hii, ungealia pande zote mbili, wewe ni mtu wa zamani enzi zile za wabibi wetu? sio wanaume tu wanaohitaji chakula cha usiku, mie nahitaji kula hata kila siku lakini mwezangu anakuwa hoi mara anapoonja tu! yaani anaweka tonge mdomoni tu kashiba na wala hajali kama na mie pie nataka kula, tena akila hanawi hata mikono anakuja tu na kusema naomba nile! sasa na mie nikale wapi? Halafu anakuwa mkali kunifuatilia kama naenda kutafuta chakula nje. je wewe aunt sina jazba hapa niandikapo ni kwa upole tu, unafikiria ni wanaume tu ndio wanatakiwa kula? wanawake hawawezi kwenda kutafuta nje kama hawapati chakula ya kutosha na kusabaisha huwo ungonjwa? Nakushauri aunt siku nyingine utoapo mada ufikirie na uwe na busara, wanawake sio wanyama mtu akija tu unampa chakula hata bila upendo, kwanza chakula bila matayarisho kinaumiza kutokana na maumbile yetu wanawake. Labda wewe aunt unaweza hayo!

    mdau bila jazba.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 30, 2011

    Wewe Anonymous Fri jul 29. 10:26pm,
    Yaani umenigusa kabisa hisia zangu! Umesema kweli kabisaaaa, hebu wafundishe wanaume wenzio katika hili jambo! Naomba uandike kitabu ili wote wanawake na wanume tufaisike katika hili jambo tuokoe jamii.
    Once again BRAVO!!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 30, 2011

    Mada hii ni muhimu sana katika kuelimishina lakini nashangaa wengine wanaiponda. Kwa kweli wengi wamechangia maoni mazuri tu ukiacha hao wachache wanaoponda. Tendo la ndoa sio tendo lenye fomula. Wakati mwingine linatawaliwa na saikolji ya mtu. Mnajua kwamba binadamu tunapitia masahibu mengi na haya yanaweza yakakutoa kabisa nje ya mfumo wako wa kawaida wa kufikiri. Kumbukeni tendo la ndoa ni tamu kama mmoja wa wanaolifanya hayuko kwenye stress (msongo wa mawazo).

    Msongo wa mawazo unaweza ukampata mwanmke au mwanaume. Na mtu anaweza kuwa katika stress kwa sababu za kujitakia kama vile kulazimisha kuwa na vitu vilivyo nje ya uwezo wenu au hisia mbaya kwamba mwenzako katoka nje ya ndoa. Pia stress inaweza ikasababishwa na mambo yaliyo nje ya uwezo wa mhusika, mfano changamoto za kazini, mitaani ambazo mara nyingi wanazipata wahusika walioajiriwa.

    Kwa hiyo ni vema mkavumiliana pale ambapo mmoja wenu hayuko katika mood ya kufanya hilo tendo. Jipeni muda kwani stress ni kitu cha kupita. Ukiacha kula hiyo kitu mara moja au mbili kwa wiki hautakufa na wala hutaumia mahali popote.

    Lakini kama wengine walivyosema, maandalizi ni kitu muhimu sana kabla hujaamua kukata tamaa ya tendo hilo kwa siku hiyo. Muandae mwenzio ili ujue ni kiasi gani amesongwa na mawazo. Na hii itakusaidia wewe ili usikimbilie kuweka hisia zako kwenye tendo kwani atakapokukatalia kabisa utajisikia vibaya na utamchukia.

    Mimi nimeoa na nimekaa kwenye ndoa kwa miaka kadhaa sasa na tuna watoto. Mimi ni muajiriwa katika sekta fulani hapa dsm lakini mke wangu ni mama wa nyumbani. Kukaa kwake nyumbani kunamfanya asiwe na stress za mara kwa mara na hivyo anajikuta akihitaji hilo tendo kila siku. Lakini mimi wakati mwingine nachoka kwa sababu ya hizo stress za kazini. Ofisi yetu iko bize sana na kazi zina changamoto nyingi. Kwa vile mke wangu analijua hilo, amekuwa akiniandaa kabla ya tendo hasa pale anapoona siko katika mudi nzuri. Sitawaeleza ni jinsi gani ananifanyia kwani ni mambo yetu ya ndani. Lakini cha muhimu ni kwamba akishanifanyia hayo manjonjo yake najikuta stress zinaisha na ninampa kipigo cha uhakika hadi anaongea lugha za ajabuajabu. Tukitoka hapo wote tumefurahi ila yeye anakuwa amefurahi zaidi kwani baada ya hapo analala usingizi mzito kiasi kwamba hata ukimfinya hakusikii. Na asubuhi yake nikijaribu kugusia tena anakataa kwani hamu ilishamuishia.

    Kwa kumalizia tu nawaombeni sana, jitahidini kufanyiana maandalizi kabla ya tendo. Na hao wakina dada wanaotanguliza maslahi ambayo uwezo wenu haupo mjue hilo ni sumu pia kwenye ndoa na linachangia kuchukiwa na mumeo. Tuendelee kuelimishana kwani tendo hili ni msingi mkubwa wa amani katika ndoa hasa kama uaminifu na usikivu vipo. Ndoa yenye amani ni msingi mzuri wa jamii yenye maadili.

    Kwa mtu atakeyehitaji kupata mafundisho ya jinsi ya kumuandaa mwenzi wake tafadhali iandikie kwa email adammloka@y7mail.com ili nimpe vidokezo. Ila ujitambulishe kama wewe ni mwanamke au mwanamume.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 30, 2011

    Du!tumefika naona! sasa nyinyi mbali ya kula chakula cha usiku jambo jingine hamfikirii tu? ndio maana nchi inadidimia, mmeoana sio kwa ajili ya kula chakula, bali kwa ajili ya kujenga familia! kama unanjaa ya kula chakula bora usioe nenda kanunue, wapo kibao kwa ajili ya kazi hiyo!
    kidume

    ReplyDelete
  21. Jamani mada hii ni tamu sana, hasa kwa wanandoa ambao wasingependelea kwenda kula kwa Mama ntilie, lakini wanaona hawapewi nyumbani chakula cha kuridhisha. Anonymous Fri Jul 29 10:26pm na Sat Jul 30 07:26am mmetoa mchango mzuri sana wakusaidia ndoa ziweze kudumu, hongereni sana. Kiukweli baada ya kusoma maoni yenu, inabidi nijitafakari upya maana nilishaanza kufikiria kwenda kutafuta chakula kwa Mama ntilie. Endeleeni kuelimisha jamii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...