JK  akifurahi  na Mbunge wa Kigoma Kaskazini  Mh. Zitto Kabwe akiwa katika vazi la asili ya kabila la Waha wakati wa sherehe za uzinduzi wa barabara Mwandiga-Manyovu yenye urefu wa km 60. Picha na John Lukuwi
------------------------
‎'Msikubali atakayenirithi awe wa rika langu. Kizazi chenu sasa kijiandae'-JK 
to David Kafulila and I (Zitto Kabwe) when launching the construction of Malagarasi Bridge



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2011

    Huyu mheshimiwa Zitto Kabwe amesahau vazi la asili la kiume la Waha? Sio mlumba kama kwenye picha bali ni MPUZU na pia angempa raisi mrehe na rungu.
    I grew up in Kasulu enzi za ukoloni
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2011

    tunashukuru kwa kupata serikali sikivu

    ReplyDelete
  3. Hii kauli ya "Msikubali atakayenirithi awe wa rika langu, kizazi chenu sasa kijiandae-JK" Nimeipenda sana na ni ya msingi kufanyiwa kazi. Pia ushirikiano wa kuleta maendeleo ya nchi bila kuangalia tofauti ya kisiasa(Vyama) ni nzuri sana. Napupongeza kwa hilo JK

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 05, 2011

    Watanzania wote tumchague ! KIKWETE
    Jamaa !eh! KIkwete !
    Akina mama wote tumchague ! KIKWETE
    Akina baba wote tumchague !KIKWETE
    Tanzania! Kikwete
    Nakumbuka baadhi ya mistari ya lile sebene lake
    kutoka kwao vichaa ffu wa ughaibuni

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 05, 2011

    Kusema hivyo anaogopa umri wa Dr Slaa maana anajua marafiki zake wote waliofisadi nchi watakuwa hatarini.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 05, 2011

    Mimi bado sijaridhika kama balabala ya kigoma kwenda Mwanza bado ni tope!!Ila ni nafuu kwasababu hili ni lakutuunganisha na wenzetu warundi.
    Lakini mheshimiwa Zitto au kafulila piganeni chini juu na hilo lakutoka Kigoma kupita kasulu,makele,kibondo....mpaka Mwanza liwe la lami.
    Mdau wa The Hague.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 05, 2011

    Wenye umri wako waachwe unamaanisha URAIS UNAMWACHIA MAKAMBA? Maana kuna kila dalili za kumwandaa. Usimzuge Zitto.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...