Rais wa kampuni ya Ahmed's Moving Express,Inc Bw Ahmed Issa akizungmza na wanahabari Alhamisi usiku baada ya kuwasili katika uwanja wa KIA. |
Mkuu wa CAMDEN hosptality group ,Bw Munir Walji akizungumza na wanahabari baada ya kuwasili katika uwanja wa KIA. |
Mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha umeme ya PIKE Electronic corporation,Bw J,Eric Pike akizungumza na wanahabari baada ya kuwasili uwanja wa KIA. |
Afisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw Suleiman Saleh akizungumza jambo na mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha umeme ya PIKE,Bw J,Eric Pike. |
Afisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw Suleiman akizungumza jambo na mmoja wa wageni hao ambaye ni mke wa rais wa kampuni ya Ahmed's Moving Express Inc Bw. Ahmed Issa. |
Picha na Habari na Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii,Arusha.
Ujio huo, ambao umeandaliwa na ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, unafahamika kama V.I.P Safari ambapo kundi la kwanza la wakurugenzi hao limewasili majira ya saa 5:00 Jumatano usiku katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) na kulakiwa kwa shangwe na wenyeji wao.
Waliowasili ni pamoja na mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha umeme ya PIKE Electronic Corporation ,Bw J.Eric Pike na mkurugenzi wa kampuni ya CAMDEN Hospitality group inayojishughulisha na masuala ya mahoteli ,Bw Munir Walji.
Ugeni mwingine ni Bw Ahmed Issa,rais wa kampuni ya Ahmed’s Moving Express,Inc ambayo pia ni wakala wa kampuni ya Wheaton World Wide Moving ikijishughulisha na masuala ya usafirishaji.
Ugeni huo utakuwa nchini kwa muda wa takribani siku 10 kuzungumza na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.
Ujumbe huo Alhamisi mchana umepata chakula cha pamoja na wafanyabiashara mbalimbali nchini kwa jina Business Lunch mjini Arusha.
Leo ugeni huo umekula chakula cha jioni na mkuu wa mkoa wa Arusha kabla ya kutaendelea na safari ya kuelekea jijini Dar es salaam na kisha kuhitimisha safari hiyo kwa kutembelea Zanzibari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...