Wanafunzi wa darasa la saba ambao wanajiandaa na mitihani ya taifa ya kumaliza elimu ya shule ya msingi Manda wilaya ya Ludewa wakivua dagaa katika ziwa nyasa muda wa masomo baada ya kufukuzwa shule kwa kushindwa kulipa mchango wa shilingi 600 kwa kila mmoja kwa ajili ya kuchangia chakula cha walimu wanaofika kusimamia mitihani ya kujipima ya kata ya manda ,hali ya uchumi duni ya wananchi wa vijijini ni chanzo kikubwa cha wazazi wao kushindwa kulipa kiasi hicho cha fedha(picha na Francis Godwin)
Home
Unlabelled
Wanafunzi waamua kuvua Samaki baada ya kufukuzwa shule kwa kutolipa mchango
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hii mbona aibu sana, utamfukuzaje mwananfunzi shule ati kwa kushindwa kulipa pesa ya chakula za walimu? kwani hao walimu hawalipwi mishahara na serikali? Bungeni huko serikali inatoa ati posho ya vikao kila siku zaidi ya sh. 200,000 kwa wabunge zaidi ya 300 badala ya pesa hizo kutumika kusaidia taasisi za elimu na afya, Halafu hata viongozi wa mkoa nao wanafanya kazi gani? Mbona mnachafua jina la nchi namna hii, yaani hapa nilipo nina hasira mbaya sana we acha tu.
ReplyDeleteeti ni nini? jee hi si sawa na ile issue ya bungeni ya yule alodai pesa zilipwe kwa wale wanaokwenda bungeni kufuatilia bajeti ya wizara yake?
ReplyDeletekwa ninavyokumbuka mimi walimu hulipwa na serikali gharama zao zote, sasa leo inakuwaje wanafunzi wawalipie walimu kwa mlo wao? Kama serikali imeshindwa kuwalipa gharama zao tunategemeaje wazazi kuweza kulipa? na kwa nini mtoto ateseke kwa kosa ambalo hata sio lake?
Hivi jamani ndivyo Tanzania tunavyoandaa taifa la kesho?
Wajameni hizo hela ni ghali sana kama kila mwanafunzi ni shs 600 na kwenye kila darasa kuna wanafunzi 30-40 na darasa lina mikondo a,b,c na waalimu watakao kuja kusimamia ni watatu pigeni hesabu hizo zitakuwa shs ngapi na wao wanafunzi watakula wapi? aliyepiga mahesabu arudie tena is a lot of money mlo mmoja tu wa mchana maana still hao waalimu wataenda makwao kula dinner. This is not fear at all. Ikitegemea ni shule ya kijijini. mmmmhhhhhhhhhh. sijakubaliana na hii 600
ReplyDeletejamani hii ni laana kwa viongozi wa tanzania, wao kila kitu wanapata na watoto wao wanasoma shule za hali ya juu, wanapata posho za hali ya juu lakini hata kusema wawasaidie watoto wa shule zao huko vijiji hawawezi ni wabinafsi kupita kiasi, wanajidai eti utawasaidia watu wangapi? Mungu tusaidie Tanzanie tuache ubinafsi
ReplyDeletemungu wabariki hawa watoto na wazazi wao. hii ni aibu. inatiaa huzuni, inakasirisha kiasi sina hata msamiati mzuri wa kueleza dukuduku langu. Walimu wote watakaokula hicho chakula wajue kua wameiba haki za watoto wadogo. Nyie walimu muone aibu na muanze utamaduni wa kujitegemea na sio kunyonya malaika wa mungu
ReplyDelete