Wanafunzi wa kike katika shule ya msingi Manda wilaya ya Ludewa ambao wanasubiri kufanya mtihani wa Taifa wa Darasa la saba wakitoka kuokota kuni porini mida ya masomo baada ya kufukuzwa kwa kushindwa kulipa mchango wa shilingi 600 ili wapate kufanya mitihani ya kujipima ya kata mzigo wa kuni kama huu wamekuwa wakiuuza kwa kiasi cha shilingi 100.
Mwanamke mkazi wa kijiji cha Iwela wilaya ya Ludewa Bi.Anna Nkwera akitoka kutafuta maji katika mabonde umbali wa kilomita 5 kutoka nyumbani kwake huku akiwa amebeba mtoto mkononi,sehemu kubwa wanawake wa vijijini wamekuwa na majukumu zaidi ya kazi katika familia huku wanaume wakiishia kushinda katika vijiwe vya pombe(picha na Francis Godwin)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2011

    What a shame to our country! Yaani mtu anashindwa kulipa ada ya sh 600/= hadi anafukuzwa shule? halafu tunaambiwa kuna viongozi wa serikali wanalipana sh laki mbili na zaidi kama sitting allowance. halafu wananchi bado tunaendelea kuwapa madaraka watu haohao. Tafakarini ndugu zangu watanznia. Huko tuendako tutakuja kujutia maamuzi yetu.

    ReplyDelete
  2. Kaka,

    Hao wanafunzi jumla wako wangapi, yaani nataka kujua jumla wanadaiwa shilingi ngapi nione uwezekano wa kuwalipia?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2011

    Vp nchi yetu inaelekea wapi? Mbona sielewi mambo yanavyoenda jamani!
    Narudia tena Nchi yetu inaelekea wapi wajameni? Kwann hizo pesa za posho kwa wabunge zisitumike kuwalipia hawa watoto ada yao ya shule!
    Serikali Hamuoni hili mnakaa kizembezembe tu! Pumbavu zetu ! Hawawatoto wanatakiwa wawe shuleni wanasoma ! Pumbavu walimu wakuu na viongozi wetu. pumbavu mara 7

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2011

    SHAME ON YOU ALL THE SO CALLED VIONGOZI WA SERIKALI. Shame, shame,shame hata kwa hao majibaba waiojua wajibu wao ni nini hwen it comes to raise a family kwa kuwatupia mzigo kina mama.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2011

    MBUNGE WA LUDEWA UPO WAPIIIIIIIIIIIIIIIIIIII?????? SHAME.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2011

    SISHANGAI MBUNGE WAO WA WILAYA YA LUDEWA KUSUTWA LEO BUNGENI (REF:PICHA HAPO JUU - KTK BLOG HII): SURELY, KUNA SERIOUS ISSUES LUDEWA. NI KAMA YUPO 'OUT OF TOUCH'.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2011

    Nilikuwa na maoni exactly kama yenu. Inauma sana unapoona watoto wadogo wanavyoteseka lakini Serikali yetu haijali. Waliwahi kusema watoto wasifukuzwe madarasani kwa jambo lolote la kuhusiana na hela lakini hakuna kinachoendelea. Hivi viongozi wetu hawana watoto ? Ningependa kujua kama mtoa hoja wa pili kujua kama viongozi wetu watashindwa kufanya lolote basi tujulishwe ni kiasi gani tunaweza kuwasaidia hawa watoto ambao wanaendelea kuteseka badala ya kujiandaa na mitihani.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2011

    Watani wangu wa manda ludewa mko wapi kazi kukoga,kuvaa masuti kuchangiana miharusi na kunyweshana mipombe tu nendeni mkawachangie hao watoto wasome.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 27, 2011

    mdau wa mwanzo ingawa nakubaliana nawe lakini umekosea kidogo, kwani hiyo sio ada bali ni malipo ya chakula cha walimu watakaokuja kusimamia mitihani yao. Hili ni tatizo sugu, badala ya serikali kushindwa kuwalipa walimu posho ya kufika hapo shuleni, wanafunzi ndio wanalazimishwa kulipa. suali ni jee wakati serikali ikiwalipa huko mbeleni na wao watawarudishia pesa wale waliolipa.

    Vyovyote vile hii ni aibu kubwa mno!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 27, 2011

    Sh 600 hata nusu ya dola 1 haijafikia. yani ni kama cent 40. or 0.40$ Mtanzania wa karne ya 21 anashindwa kuilipa na kufukuzwa shule. no comment.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 27, 2011

    Shilling 600 ni kama 35p sterling
    Yaani hao watoto kumi hivi kwenye picha wahitaji £5 sterling.
    And I cant help them.I feel sick

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 28, 2011

    tupatie mawasiliano ya hao watoto wanaodaiwa na idadi yao hata kama kuna wengine zaidi ya hao nipo tayari kusaidia serikali kuwalipia watoto wote wanaodaiwa mashuleni

    shame on serikali yetu inayopokea mabilioni ya misaada kila siku

    kila goti litapigwa siku hiyo ikifika kilio chetu mungu anakiona malipo hapahapa duniani hao mafisadi wataishia kujinyonga wengine kufia magest

    mdau mwenye machungu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 28, 2011

    WADAU HAPO JUU: NAOMBA TUELEWE TU KUWA SUALA SI KIASI KIDOGO TU KAMA HICHO CHA PESA NA SENTI NGAPI UKILINGANISHA NA PESA ZA KIGENIILA NI PRINCIPLE. NA NDIO MAANA NIKAULIZA MBUNGE WALIOMTEUA KWA SHANGWE (MAJORITY) YUPO WAPI? LAKINI INAONYESHA KUWA HATA MBUNGE MWENYEWE HAYUPO CONNECTED NA KHALI HALISI YA JIMBO LAKE. HIVYO KAMA MBUNGE WA LUDEWA ANGEWEZA KUFUATILIA HILO NA KUWAWAJIBISHA WALIOFANYA WANAFUNZI HAO WAZUILIWE MITIHANI INGEKUWA MFANO MZURI. NA JE, SINA UHAKIKA KAMA SERIKALI ILITANGAZA KUWA SUALA KAMA HILO HALITOTOKEA UNDER IT'S WATCH, JE, IMEKUWAJE?

    ReplyDelete
  14. DO WE REALLY HAVE A GOVERNMENT? Serious question.
    Kama commenter number 1 alivosema, watu wanapewa ya laki mbili, meanwhile tuna watu wanaoishi hivi. I think we need to look at how much our leaders are being paid. How about you get paid based on performance? Mishara mikubwa,private vehicles,houses,and for what? Sisemi kuwa viongozi wetu wasiruhusiwe kuwa na maisha ya kifahari. Ninachotaka kuona ni maendeleo. Tunahitaji watu wenye uchungu wa nchi, na si watu wanaotaka madaraka. Kuna wanaopenda madaraka lakini si majukumu, na viongozi wetu ndivo walivyo. Plain and simple. JK aneenda kufungua mahoteli ya kifahari huko Serengeti Kempinski, does that make any sense? Nyerere ungeweza kumuona anaenda kukata utepe kufungua hoteli Serengeti? Nyerere alikataza kuharibu mbuga zetu. Leo hii JK anajenga barabara kupita Serengeti. Serengeti is a UNSECO world heritage site.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 28, 2011

    mimi nimemuonea huruma huyo mama hapo daa maisha mateso sana sehemu nyingine za nchi yetu. Hiyo ya kubeba kuni na kufanya kazi kwa walimu daa hiyo tumefanya sana wengine enzi zetu da lakini baadhi yetu tumetoboa. Nashukuru mungu na tuendelee kumuomba Mola siku za baadae haya mambo yaishe

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 28, 2011

    Je huyu mama mwenye kubebeshwa ndoo na mtoto tunasemaje?! Kwanini wanaume ambao ndio wenye nguvu wakae nyumbani badala ya kutengeneza toroli wakawasaidia wake zao kwenda 'kusaka' maji?! Si hivyo tu, huko alikoenda kuchota maji yaelekea kisima kilikauka kwani hao watoto wengine wamerudi na ndoo kavu; na akifika nyumbani anategemewa kupika na kupakua na watu wale ...What is going on Tanzania?!!!! Kweli machozi yananitoka, especially ninaposikia wabunge wetu wanapodai kuongezewa posho... for doing what?!

    Terry

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 28, 2011

    OOOh my poor country Tanzania
    Natamani kulia machozi nikimwangalia huyo mama hapo juu hali duni alionayo.Mbunge wao ni juzi tu nlimwona akipigia watoto hao hapo juu magoti leo tena anasutwa nje ya ukumbi hii inaonyesha mbunge huyu hawajali kabisa wapiga kura zake,hata kisima cha maji ameshindwa kuchimba,wanafunzi wanaacha masomo kwenda kuokota kuni ndipo wasome.
    Nchi hii inaelekea wapi-ujinga umaskini maradhi ndio yanazidi.
    Nchi hii ni tajiri mno ubinafsi wa watu wachache ndio uliotufikisha hapa.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 28, 2011

    You ask where the men are, for not helping wakina mama.
    I will tell you what
    They have gone for pombe to drown their miseries
    When you feel so bad and powerless, sometimes you go for a drink to console your soul

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 28, 2011

    Umeona sasa ndio maana mbunge wao anasutwa,hana lolote
    yaani mie nahisi wilaya imekosa kabisa mbunge

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 29, 2011

    When you feel bad and powerless, the answer is to drown your sorrows and let your family suffer? NO. If akina mama wangekuwa wanafanya hivyo si kijiji chote kingekuwa kimwekwishaa.
    When life gives you lemons, make lemonade. Mpaka vitoto vidogo vinaenda kuchota maji na mama wakati baba kaenda kunywa. that doesn't make any sense! Baba angekuwepo kumsaidia mama, kugawana majukumu, angalau ugumu wa maisha ungepungua. Instead, baba gives up na mama hata siku moja hawezi acha familia ishinde njaa. And this is our weakness as women. Ukipata partner mbaya asiyekuwa na ushirikiano hata siku moja hautaweza kuondokana na umasikini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...